Ushawahi kusafiri kwenye basi umekaa na mtu yeye kila anachokiona njian yeye anakula tu,

Ushawahi kusafiri kwenye basi umekaa na mtu yeye kila anachokiona njian yeye anakula tu,

Wanakera sana, ni wasumbufu kutaka gari lisimame porini wakajisaidi a.k.a kuchimba dawa. Wengine ni wachoyo wanakula wenyewe tu hukaribishwi, hao wacho huwa wananifanya na mimi niwe huru kula bila kukaribisha mtu. Kuna wengine ukiwakaribisha wanakuambia asante tu hawali ila hununua vyao na kula. Sinaga swaga za kulakula hovyohovyo garini na kukaribisha mtu anayekataa kula changu. Bora ninunue karanga au biskuti nisukumie na maji au soda/juisi nile kimya kimya. Sipendi nikaribishe mtu halafu anikatalie
utakuja kuwekewa madawa ya kulevya mwisho uibiwe kwa kupenda kukaribishwa vyakula na watu usiowajua.

Kuna siku nilipanda basi na wamasai wametoka mnadani kuuza ng'ombe walikuwa na vibunda vya maana .Kumbe walipotoka kuna jamaa walikuwa wanawalia timing..mmoja akakaa na mmasai ,njiani akatoa biscuit/juice hivi akampa mmasai.. jamaa ile kubugia tu akalewa na kuzima mazima..jamaa akamchomoa kibunda kisha akashukia njiani..

mmasai kuja kuamshwa hajielewi kalewa zaidi ya mlevi wenzake wakasema huyu hanywi pombe. Kumsachi kiunoni hana hata mia mbovu.
 
Kuna siku nasafiri na usafiri binafsi na mama watoto. Tumefika Korogwe tukaingia mgahawani mimi nikachukua chai ya rangi na andazi tu. Yeye sasa anapenda kula balaa kasomba mazaga kibao na chai nikamwambia utavuruga tumbo hilo na tuko safarini utapata shida, anaona napenda kumsema kwenye misosi. Tumetoka hapo Korogwe tukapita Mombo hapo tushatembea kidogo kutoka Mombo tumbo likaanza kumkomesha. Na pale hakuna sehemu ya maana hadi Same. Nikamwambia hapa ni mpaka Same lakini ukizidiwa tutasimama utaingi kwenye mashamba ya katani hayo umalize shida zako. Nilikanyaga gari siku hio baada kama ya 45minutes tukafika Same akaenda msalani tangu siku hio anajifikiria kabla ya kula kula hovyo.
Ulimuonea sana, tumbo likivurugika msaada popote mkuu.
 
Siku niko na dogo toka mkoani Arusha nampeleka kijijini Mbeya ilikua tabu.
Kuanzia ubungo ye anatafuna kila anachokiona, teremshia mimaji , chai, Coca-Cola twende.
Kufika ruvu tu kuitafuta moro alikoma.
Mpaka tufike msamvu hadi analia.
Toka pale katia adabu
Duh uwongo njia yake fupi, unamsafirisha toka Arusha, tena kutokea ubungo anakula tu? Acha urongo
 
Back
Top Bottom