Ushawahi kusafiri kwenye basi umekaa na mtu yeye kila anachokiona njian yeye anakula tu,

Ushawahi kusafiri kwenye basi umekaa na mtu yeye kila anachokiona njian yeye anakula tu,

Umenikumbusha bana..... nilikuwa nasafiri na Rahaleo natoka Dar naelekea Tanga. Kuna mtu wa makamu tu kakaa dirishani na chupa yake ya Mango juice na keki. Tulipofika Kibaha Maili moja kanunua mayai ya kuchemsha, clips za viazi kaongeza na juice. Tunafika Chalinze kanunua mahindi ya kuchoma anakula tuuuu. mbele kidogo kapandishwa muuza korosho; jamaa anaye.... sasa watu wakaanza kumwangalia na kumshangaa, kwa kifupi alikuwa anakula muda wote vingine kaviweka kwenye vifuko. Tukiwa tunakaribia Segera ikatokea harufu mbaya sana kwenye gari; watu wa karibu wakamgeukia wakimshuku amejamba. Harufu ikazidi sana kuna jamaa akamwambia mzee umezidi bwanaaa ... jamaa akataharuki akasema unasemaje kwani mie ndie nimejamba???? Jamaa akamwambia ndio wewe umejamba.... mtu gani unakula njia nzimaa..... abiria tukacheka kwa sauti ikawa vurugu mle.. Mzee akasimama kashika siti kwa sauti akasema mie nakula nguvu zangu .... sijajamba mie... mwanionea wivu siyo? Jamaa mwingine karukia ... hakuna cha wivu hapa.... unakula mno hadi unakera ona sasa harufu basi zima. Lilizuka zogo la kufa mtu hadi konda alipokuja na kusema eneo lile lina harufu kutoka kwenye korona la katani ambalo halijatumika muda mrefu na sio ushuzi..... ndio kidogo watu walitulia lakini mzee alikuwa anafoka balaaa na watu ni vicheko tu
 
Nimecheka hadi watu wananishangaa, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Siku niko na dogo toka mkoani Arusha nampeleka kijijini Mbeya ilikua tabu.
Kuanzia ubungo ye anatafuna kila anachokiona, teremshia mimaji , chai, Coca-Cola twende.
Kufika ruvu tu kuitafuta moro alikoma.
Mpaka tufike msamvu hadi analia.
Toka pale katia adabu
Arusha Nako kunastendi ya ubungo
 
Sikunimepanda Bus kwenda Iringa toka Dom King-Kross boda mtera hapo vumbi tu kubandeki, siti ya nyuma kule nimekaa e bana mbele mbele kati hapo wakazama wamasai wagogo rundo konda kawaleta kule nyuma e bana eeh waliingia na mtindi unanuka balaa alafu wenyewe wamejipaka mafuta ya samli.
Basi unaambiwa,mara mtindi wanashushia viazi vitamu na miwa huku wanakoroganya kilugha chao,
Fikiria waplipoanza kujamba sasa plus harufu yao nilijihisi niko kandahar
Ilibidi niombe ukimbizi dere akanipa hifadhi, vinginevyo ningekufa si utani.
 
Wanakera sana, ni wasumbufu kutaka gari lisimame porini wakajisaidi a.k.a kuchimba dawa. Wengine ni wachoyo wanakula wenyewe tu hukaribishwi, hao wacho huwa wananifanya na mimi niwe huru kula bila kukaribisha mtu. Kuna wengine ukiwakaribisha wanakuambia asante tu hawali ila hununua vyao na kula. Sinaga swaga za kulakula hovyohovyo garini na kukaribisha mtu anayekataa kula changu. Bora ninunue karanga au biskuti nisukumie na maji au soda/juisi nile kimya kimya. Sipendi nikaribishe mtu halafu anikatalie
 
Mwache ale as long as hakubugdhi, binafsi sio mpenda kula njiani na zile kuku zao za juzi.

Bora safari za usiku, hamnaga kero za watu wa namna hiyo ila mchana unakuta mtu kafunga msosi toka kwake na bado njiani anakula hovyo.
Hakubughudhi vipi wakati muda wote mdomo nuka uko wazi na mara akumwagie vinywaji au chakula
 
Sikunimepanda Bus kwenda Iringa toka Dom King-Kross boda mtera hapo vumbi tu kubandeki, siti ya nyuma kule nimekaa e bana mbele mbele kati hapo wakazama wamasai wagogo rundo konda kawaleta kule nyuma e bana eeh waliingia na mtindi unanuka balaa alafu wenyewe wamejipaka mafuta ya samli.
Basi unaambiwa,mara mtindi wanashushia viazi vitamu na miwa huku wanakoroganya kilugha chao,
Fikiria waplipoanza kujamba sasa plus harufu yao nilijihisi niko kandahar
Ilibidi niombe ukimbizi dere akanipa hifadhi, vinginevyo ningekufa si utani.
Duh, usiombe kuwe na joto na majasho yanawatoka
 
Wanakera sana, ni wasumbufu kutaka gari lisimame porini wakajisaidi a.k.a kuchimba dawa. Wengine ni wachoyo wanakula wenyewe tu hukaribishwi, hao wacho huwa wananifanya na mimi niwe huru kula bila kukaribisha mtu. Kuna wengine ukiwakaribisha wanakuambia asante tu hawali ila hununua vyao na kula. Sinaga swaga za kulakula hovyohovyo garini na kukaribisha mtu anayekataa kula changu. Bora ninunue karanga au biskuti nisukumie na maji au soda/juisi nile kimya kimya. Sipendi nikaribishe mtu halafu anikatalie
Sasa mtu umekutana nae kwenye gari halafu itegemee akuamini kiasi cha kupokea chakula unachokula?
 
Nilikaa na dada mmoja safarini, wote hatuli kwenye bus. Utafikiri mabubu, wote kimyaa vichwa mbele au kusinzia kidogo. Utadhani tulikuwa tunashindana kutokula au tuna mfungo basi tulienda vile vile Hadi tunafika, ni maji tu...Ilikuwa kombinesheni matata sana.
 
Inanikumbusha miaka ya 2010s nilikuwa nasafiri kutoka Dar kwenda Mbeya kumpeleka sister shule, nilikaa na dada mmoja mi niko dirishani yeye yupo hii siti ya pembeni yangu.

Lile basi lilibeba abiria wengi njiani kuna jamaa alisimama pembeni na yule dada akawa hapitwi na chochote kila anachokiona ananunua mara mahindi ya kuchoma/kuchemsha, mayai, mishikaki nk yaani alinikera sana na ukicheki mi ndio niko dirishani na akitaka kitu ni kuja kujiinamisha hapo dirishani kununua.

Baada ya muda kwenda nikasikia harufu kali nikahisi huyu dada niliyekaa naye amechafua hewa nikakausha kama sikusikia chochote halafu muda ulikuwa umekwenda ilikuwa ni usiku wa saa 2/3 watu wengi walikuwa wamejipumzisha so, na mimi nikaekti nimelala.

Baada ya muda tena nikasikia harufu kali nikaona huyu dada ananizoea sasa nilimgeukia nikiwa na hasira moyoni nikasema binti mrembo hivi anashindwaje kujiheshimu?

Nikamwangalia kwa macho makali huku sura nimeikunja yeye akaniangalia kwa upole akasema fungua dirisha kidogo nikafungua kioo upepo mkali ukaingia nikafunga kwa haraka ile harufu ikasambaa kwa nyuma huko nikasikia miguno miguno ya chini chini.

Safari ikaendelea baada ya muda ikasikika tena harufu kali na hii ya sasa ikawa funika! Nikafungua tena kidogo kioo, Basi zima likawa linanuka watu waliosinzia ikabidi waamke kelele zilisambaa basi zima na ile harufu ilikuwa haiishi yaani ipo tu kama vile kitu kimeoza humo ndani ya basi.

Ikabidi dereva asimamishe basi yule jamaa aliyekuwa amesimama pembeni yetu wakamtoa nje kumbe alikuwa amejiharishia bhana 😃😃 waungwana wakamuazima maji akaenda kumaliza haja zake vichakani aliporudi watu wakagoma asije tena kuja kukaa kule kwetu ikabidi akae jirani na dereva safari ikaendelea. Hili tukio sitalisahau 😃
 
Kuna siku nilipanda basi kwenye siti yangu ikabaki nafasi moja, kuna bidada mmoja mwenye shep matata nilitegemea aje akae yeye badala yake akasukumwa na mbwiga mmoja akawahi siti , yani nilitamani nimnase kibao yule fala basi tu.
Ungemwambia seat umemuwekea mtu na mtu mwenyewe ni huyo bidada.
 
kuna safari nilisafiri kwenda Ddm kutoka Dar, nilikuwa nimepata siri ya dirishani, akaja dada mmoja mwenye watoto watatu, basi akaanza kuagiza vitumbua lete, karanga lete, mayai lete, juisi lete, sasa vikavurugana kule ndani, alinitapikia nilimmaindi, gari zima walimuwashia moto
Hivi wakisafiri nja huwa inaongezeka? Kwanini mtu ale kila kituo?
 
Kuna siku nilipanda basi kwenye siti yangu ikabaki nafasi moja, kuna bidada mmoja mwenye shep matata nilitegemea aje akae yeye badala yake akasukumwa na mbwiga mmoja akawahi siti , yani nilitamani nimnase kibao yule fala basi tu.
😂😂😂
 
Kuna siku nasafiri na usafiri binafsi na mama watoto. Tumefika Korogwe tukaingia mgahawani mimi nikachukua chai ya rangi na andazi tu. Yeye sasa anapenda kula balaa kasomba mazaga kibao na chai nikamwambia utavuruga tumbo hilo na tuko safarini utapata shida, anaona napenda kumsema kwenye misosi. Tumetoka hapo Korogwe tukapita Mombo hapo tushatembea kidogo kutoka Mombo tumbo likaanza kumkomesha. Na pale hakuna sehemu ya maana hadi Same. Nikamwambia hapa ni mpaka Same lakini ukizidiwa tutasimama utaingi kwenye mashamba ya katani hayo umalize shida zako. Nilikanyaga gari siku hio baada kama ya 45minutes tukafika Same akaenda msalani tangu siku hio anajifikiria kabla ya kula kula hovyo.
 
Back
Top Bottom