Ushawahi kushindwa kula chakula kwa uchafu wa mazingira au mpishi?

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Kuna watu wanaishi maisha ya ajabu sana, na wao wanaona ni sawa.

Kuna sehemu nilienda wakaanza kuandaa chakula, mara nikaona mpishi anapika mara akafutia sufuria na kanga aliyojifunga, nikasema tobaa hiki chakula siwezi kukila tena.

Usafi ni muhimu sana kwa mpishi kwani ukizingua kwenye usafi magonjwa ya milipuko kama kipindupindu hakiwezi kukuacha salama.

1679655658885.jpeg

Ushawahi ona ushafu wa aina gani kwenye kuandaa chakula ukashindwa kula?
 
Hata muaandaji nikiona ana kucha ndefu alafu chafu...sili.
 
Harufu ya K iliyo period alimbalaza kwenye sahani nikawa nasikia harufu sasa najiuliza hii harufu unatoka wapi? Kila nikipiga tongue wapi hola yaan naona kabisa nakula yale madude kwa harufu kumbe alijishika huko kunako akalambaza sahani akaweka chakula akalambaza bakuri akaweka mboga akanipa nile, nikawa najiuliza inamaana yeye hasikii hii harufu au anafanya kusudi?
 
Daaaa? Kuna siku nilikuwa safarini nikafika stendi moja hivi nikawa nasubiri kuunganisha basi jingine. Njaa ilinishika nikaamua kwenda kwa mama nitilie palepale stendi.

Nikaagiza wali nyama... Bwana eeee! Nilipiga vijiko viwili tu nikaibuka na bonge la mende limenona kinyama. Sikutapika. Nikajikaza nikanyanyuka nikalipa pesa yao kimyakimya nikasepa nikawaachia miwali na mmende wao.

Tena nakumbuka kisa cha mende kilinifanya hadi leo sinywi chai ya rangi katu. Nakumbuka nilikuwa darasa la sita enzi hizo. Ilikuwa wekendi hatukwenda shule. Maskani asubuhi tukakusanyika kwa ajili ya kifungua kinywa, kama kawaida kiporo cha wali na chai.

Sasa kila mtu anamimina chai kutoka kwenye mirija (watoto wa jana hawataelewa), enzi hizo chupa za chai zilikuwa kwa washua tu. Basi kumimina chai hivi ikaja na bonge la mende kutoka birikani. Sikutamani hata kula tena, na hadi leo sitamani hata kuonja chai ya rangi, naona kama nakunywa mende tu.

Kifupi mende sipendi kabisa kumuona hata karibu na chakula. Bora nione nzi nitamtoa niendelee kula.
 
Mimi muda mwingi nashinda porini nakata mikaa so muda mwingi nakula kwa mama ntilie.

Mimi nikitaka kula kwa mama ntilie naagalia Maji anayooshea vyombo na yeye mwenyewe.

Nikikuta maji yana sabuni nasepa mazima au nikute ana kijiti kakiweka mdomoni sili kwake.

Mama ntilie ebu jifunzeni usafi ,maji ya kusuuzia vyombo inatakiwa yabadilishwe frequently sio kuanzia asubuhi mpaka jioni maji hayo hayo au utakuta muhudumu ana kijiti mdomoni anajichokonoa halafu anakitoa anakifuta na vidole then anakuja kushika vibakuli na sahani anakuwekea msosi,ukifanya hivyo sili nasepa zangu.
 
Muonekano wa muuzaji unatosha kukuonyesha chakula kimepikwa katika mazingira gani.
Mimi kwa mama ntilie sili mchuzi wa aina yoyote nitakula wali maharage au pilau tofauti na hapo hapana na hapo labda nikose kabisa chips ndi nitakula.
 
Daaaa? Kuna siku nilikuwa safarini nikafika stendi moja hivi nikawa nasubiri kuunganisha basi jingine. Njaa ilinishika nikaamua kwenda kwa mama nitilie palepale stendi.

Nikaagiza wali nyama... Bwana eeee! Nilipiga vijiko viwili tu nikaibuka na bonge la mende limenona kinyama. Sikutapika. Nikajikaza nikanyanyuka nikalipa pesa yao kimyakimya nikasepa nikawaachia miwali na mmende wao.

Tena nakumbuka kisa cha mende kilinifanya hadi leo sinywi chai ya rangi katu. Nakumbuka nilikuwa darasa la sita enzi hizo. Ilikuwa wekendi hatukwenda shule. Maskani asubuhi tukakusanyika kwa ajili ya kifungua kinywa, kama kawaida kiporo cha wali na chai.

Sasa kila mtu anamimina chai kutoka kwenye mirija (watoto wa jana hawataelewa), enzi hizo chupa za chai zilikuwa kwa washua tu. Basi kumimina chai hivi ikaja na bonge la mende kutoka birikani. Sikutamani hata kula tena, na hadi leo sitamani hata kuonja chai ya rangi, naona kama nakunywa mende tu.

Kifupi mende sipendi kabisa kumuona hata karibu na chakula. Bora nione nzi nitamtoa niendelee kula.
Makubwaaaah [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
nikiona mtu anapika na hajafunika nywele hata kwa fimbo sili, na mtu awe anavutavuta makamasi ndo nitatapika kabisaa
 
nilishindwa kunywa supu baada ya kuona maji yanayooshewa vyombo.. ni kama maji yaliooshewa tairi ya gar
 
Harufu ya K iliyo period alimbalaza kwenye sahani nikawa nasikia harufu sasa najiuliza hii harufu unatoka wapi? Kila nikipiga tongue wapi hola yaan naona kabisa nakula yale madude kwa harufu kumbe alijishika huko kunako akalambaza sahani akaweka chakula akalambaza bakuri akaweka mboga akanipa nile, nikawa najiuliza inamaana yeye hasikii hii harufu au anafanya kusudi?

IMG_1463.jpg

Harufu ya k iliyo mwezini uliisikia wapi??na lipi lilikuwa lengo la kuinusa???
 
Back
Top Bottom