Kuna watu wanaishi maisha ya ajabu sana, na wao wanaona ni sawa.
Kuna sehemu nilienda wakaanza kuandaa chakula, mara nikaona mpishi anapika mara akafutia sufuria na kanga aliyojifunga, nikasema tobaa hiki chakula siwezi kukila tena.
Usafi ni muhimu sana kwa mpishi kwani ukizingua kwenye usafi magonjwa ya milipuko kama kipindupindu hakiwezi kukuacha salama.
Ushawahi ona ushafu wa aina gani kwenye kuandaa chakula ukashindwa kula?
Makubwaaaah [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Daaaa? Kuna siku nilikuwa safarini nikafika stendi moja hivi nikawa nasubiri kuunganisha basi jingine. Njaa ilinishika nikaamua kwenda kwa mama nitilie palepale stendi.
Nikaagiza wali nyama... Bwana eeee! Nilipiga vijiko viwili tu nikaibuka na bonge la mende limenona kinyama. Sikutapika. Nikajikaza nikanyanyuka nikalipa pesa yao kimyakimya nikasepa nikawaachia miwali na mmende wao.
Tena nakumbuka kisa cha mende kilinifanya hadi leo sinywi chai ya rangi katu. Nakumbuka nilikuwa darasa la sita enzi hizo. Ilikuwa wekendi hatukwenda shule. Maskani asubuhi tukakusanyika kwa ajili ya kifungua kinywa, kama kawaida kiporo cha wali na chai.
Sasa kila mtu anamimina chai kutoka kwenye mirija (watoto wa jana hawataelewa), enzi hizo chupa za chai zilikuwa kwa washua tu. Basi kumimina chai hivi ikaja na bonge la mende kutoka birikani. Sikutamani hata kula tena, na hadi leo sitamani hata kuonja chai ya rangi, naona kama nakunywa mende tu.
Kifupi mende sipendi kabisa kumuona hata karibu na chakula. Bora nione nzi nitamtoa niendelee kula.
Harufu ya K iliyo period alimbalaza kwenye sahani nikawa nasikia harufu sasa najiuliza hii harufu unatoka wapi? Kila nikipiga tongue wapi hola yaan naona kabisa nakula yale madude kwa harufu kumbe alijishika huko kunako akalambaza sahani akaweka chakula akalambaza bakuri akaweka mboga akanipa nile, nikawa najiuliza inamaana yeye hasikii hii harufu au anafanya kusudi?