Ushawahi kusikia kampuni inayouza gesi ya kupikia mpaka Tsh. 1000?

Ushawahi kusikia kampuni inayouza gesi ya kupikia mpaka Tsh. 1000?

Sendaro

Member
Joined
Apr 5, 2012
Posts
58
Reaction score
28
Katika dunia ya leo suala la habari (Information) ni muhimu sana hasa kwa kutumia teknolojia ya kisasa. Ukosefu wa habari sahihi juu ya inshu fulani iwe ya kijamii, kisiasa au kiuchumi itakufanya ushindwe kufanya maamuzi sahihi ama itakuwa na athari kwako kwa namna moja ama nyingine.

Moja ya majambo muhimu katika jamii yoyote ni chakula na mapishi. Unaweza ukakwepa gharama ya matumizi yoyote lakini sio chakula. Ili upike unahitaji nishati ya joto kwa ajili ya kuivisha chakula chako, iwe ni mkaa, kuni, umeme, mafuta gesi au nyingineyo.

Katika kuchagua nishati ya kupikia watu huangalia vigezo mbalimbali kama vile gharama na uharaka wa nishati katika kuivisha.

Kati ya nishati hizo hapo juu kuna za kisasa kama umeme na gesi ambazo husemekana ni ghali na huhitaji vifaa vya kisasa (majiko) ambayo ni ghali pia ingawa ni njia za uhakika zaidi katika kuivisha. Mkaa, kuni na mafuta mbali na unafuu lakini huchukua muda mrefu kuandaa nishati na pengine sio rafiki wa mazingira.

Katika zote hizo, nishati mashuhuri zaidi imebaki kuwa ni gesi lakini changamoto yake ni gharama. Inachukua zaidi ya Shilingi 23000 kujaza mtungi mdogo na sh 58000 kujaza mtungi wa ukubwa wa kati. Pia kununua majiko ni bei kubwa. Hali hii inasababisha watu kuendelea kutumia nishati za kizamani hasa mkaa na kuni kwa ajili ya kukwepa gharama.

SASA CHUKUA HUU MCHONGO. Ebana kuna kampuni inaitwa M-Gas, hii imekuja na suluhisho ambalo litakuwa mkombozi kwa wakazi wenye kipato cha chini. Hawa jamaa wao unalipia gesi kama vile luku, kuanzia Sh 1000 (Buku). Hawa jamaa wanafunga mita juu ya mitungi yao na wanakupa kadi janja maalum ambayo ina namba zako za malipo na unalipia kwenye Tigo Pesa, Airtel Mony, M Pesa n.k na pia ili uwashe jiko ni lazima ugusishe kadi juu ya mita. Maana yake ni kuwa hata kama haupo hakuna mtu anaweza kutumia salio lililopo kwenye kadi yako. Jamaa pia mtungi ukikaribia kuisha gesi wanauona ofisini kwao na kukuletewa mwingine bure kabisa.

Pia ukitaka kujiunga na huduma zao unatoa tuu Sh 40000 na wanakupatia jiko la sahani mbili na mtungi na kukupa gesi ya kuanzia ya Sh 5000. Kama una jiko lako la sahani mbili wanakuletea mtungi wao kwa Sh 20000 na gesi ya kuanzia ya sh 15000.

Mimi na familia yangu saivi tuna enjoy, tushahau masuala ya mkaa

Wapo Dar pekee, Kama kuna mtu anahitaji au ana swali amcheki huyu mdau yupo pale ofsini kwao:
0713748763.

2cm70j0 - Copy.jpg
 
Gesi KG 6 inauzwa 23000-24000
Je nikijiunga na hiyo pesa nitapata ujazo husika?
 
Vipi mikoani kama uku Arusha na manyara
 
Gesi KG 6 inauzwa 23000-24000
Je nikijiunga na hiyo pesa nitapata ujazo husika?
Kabisa, unafuu wake ni kuwa badala ya sh 23000-24000 unaweza kununua kidogokidogo kwa viwango vile vile
 
Tujue ujazo ni kiasi gani kwa hio pesa.......
 
Hiyo gas ya buku ujazo wake ni upi? Isije kuwa nachemsha chai pekee kisha ikakata!
Hamna inategemea na mapishi yako. kwa mfano mimi bipo single naanzia asubuhi kichai cha kishkaji, mchana labda kaugali kwangu na usiku wali na nnaweza kuanza nayo siku.maybe mchana ndio naongezea kabuku kengine
 
Hamna inategemea na mapishi yako. kwa mfano mimi bipo single naanzia asubuhi kichai cha kishkaji, mchana labda kaugali kwangu na usiku wali na nnaweza kuanza nayo siku.maybe mchana ndio naongezea kabuku kengine
Shida sio kabuku shida hadi huo mtungi unaisha hio gesi utakua umelipa vibuku vingapi?
 
Ni kama matumizi ya gesi nyingine tuu, faida yake ni kuwa unaweza kununua kidogo kidogo, kama hutaki hata laki unaweka mzee
 
Back
Top Bottom