Ushawishi wa Rais Samia Kimataifa Wawaleta Viongozi wa Dunia Dar Kushiriki Mkutano wa Nishati Safi Afrika

Ushawishi wa Rais Samia Kimataifa Wawaleta Viongozi wa Dunia Dar Kushiriki Mkutano wa Nishati Safi Afrika

Viongozi wenyewe ni wa
Niger 🇳🇪
Burkinafaso
Liberia 🇱🇷
Siera Leon
South Sudan 🇸🇸
Ivory coast
Mali
Chad
Dj wa Madagascar 🇲🇬
Na all failed states
Ukitoa Nigeria hamna nchi ya maana imeleta kiongozi
 
TANZANIA MWENYEJI MKUTANO WA NISHATI WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA

Tanzania inatarajia kuwa Mwenyeji wa Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati baada ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuridhia ombi la Benki ya Dunia (WB) na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).

Hayo yameelezwa na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Mhandisi Innocent Luoga wakati akitoa wasilisho la ujio wa Mkutano huo katika Warsha ya Wahariri na Waandishi wa Habari iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mhadisi Luoga amesema Mkutano huo utahusisha Wakuu wa Nchi 54 katika Bara la Afrika, MaRais wa WB, AfDB, Umoja wa Afrika, Mawaziri wa Fedha na Mawaziri wa Nishati.

Akielezea chimbuko la Mkutano huo, Mhandisi Luoga amesema takwimu zinaonesha kuwa, takribani Waafrika milioni 685 hawajafikiwa na huduma ya umeme hadi sasa kati ya Waafrika zaidi ya Bilioni 1 hivyo Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo Afrika wamekuja na Mpango Mahsusi ujulikanao kama Mission 300 ambao umelenga kuharakisha upatikanaji wa umeme kwa Waafrika Milioni 300 ifikapo 2030.

Ameeleza kuwa, Mpango huo unahusisha nchi zote za Afrika ambapo nchi 14 zimechaguliwa kuanza utekelezaji wa Mpango wa Mission 300 na nchi nyingine zitafuata.

Amezitaja nchi hizo kuwa ni Tanzania, Mali, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ivory Coast, Bukina Faso, Chad, Liberia, Madagascar, Malawi, Mauritania, Msumbiki, Niger, Nigeria na Zambia.
Ameeleza kuwa, Tanzania imeingizwa katika Mpango huo kwa kuwa ni nchi mwenyeji wa Mkutano kwani imeshapiga hatua kubwa katika usambazaji wa umeme kwa wananchi

Ameeleza kuwa kupitia Mpango Mahsusi wa Kitaifa wa M300 unaofadhiliwa na WB, AfDB na Wadau wengine wa Maendeleo, Tanzania itaweza kuunganishia umeme watanzania milioni 13.5 yaani karibu mara mbili ya uwezo wake katika kipindi hicho cha miaka mitano na hivyo kufanya ongezeko la wateja milioni 8.3.
=======


Mwanadiplomasia namba Moja wa Tanzania na Rais wa JMT Samia SH ameendelea kuonesha Nguvu yake ya ushawishi Duniani Kwa kuwaleta viongozi wa Dunia kuja kushiriki.mkutano wa Kilele wa Nishati Afrika yaani Africa Energy Summit ambao utafanyika Dsm.

Ikumbukwe huu ni mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika ila viongozi wa Dunia pia watakuja Kwa ushawishi wa Rais Samia chini ya ajenda yake kuu ya Nishati safi Kwa Wanawake.

View: https://www.instagram.com/p/DFQkX53OtJk/?igsh=YzlwNGsxazRtYWVn

View: https://x.com/HabariLeo/status/1882323702877974849?t=poP2DOBaVx634L-e5sUoEA&s=19

View attachment 3196370

Trump yupo? Si jing ping yupo? Putin yupo? Netanyahu yupo? Kama hawapo ujue ni mkutano wa viongozi wa ombaomba.
 
Jamani tuacheni uchawa. seriously tujipange kujitegemea. Huko tuendako siko, tujipange kutumia ubongo wetu kufikiria ni jinsi gani tutaweza kuendesha maisha bila kuwa tegemezi. Lijamaa lile huwa halitanii. Likikata misaada tutayumba sana.
 
Jamani tuacheni uchawa. seriously tujipange kujitegemea. Huko tuendako siko, tujipange kutumia ubongo wetu kufikiria ni jinsi gani tutaweza kuendesha maisha bila kuwa tegemezi. Lijamaa lile huwa halitanii. Likikata misaada tutayumba sana.
Uchawa ndio nini? Kwani Kwa Sasa tunakula vya nani?
 
Huyo mamako mwenyew hawezi kuhutubia huo mkutano kwa dakika 1 bila kuwa anasoma hotuba, bisha!!.
 
Who is Trump?
Ni wewe ndiyo umeandika huu uzi au umeandikiwa na mchambuzi maandazi?

Ulimaanisha nini uliposema viongozi wa dunia watahudhuria huo mkutano?

Acha kuleta hoja za kifala hapa

Bila hata aibu unahoji "who is Trump?"
Screenshot_20250128-132746.png
 
Back
Top Bottom