Mkuu
Ushimen naomba uniambie Location nzuri ya biashara ya kuchoma mahindi ukitoa area C.
View attachment 1192841
Mkuu, kwanza nikupe pole na uniwie radhi kwa kuchelewa kujibu hili swali linalo hitaji muongozo.
Kwanza nikupongeze kwa kuja na wazo, then nikusaidie kwenye umaliziaji.
1. Hii biashara inafaa sana ikiwa utaweka kijiwe pale Sheli, njiapanda ya kwenda Kisasa na UDOM kupitia Dar road. Pale karibu na wachoma kuku na wewe ukijipanga ninahakika hauto jutia.
2. Ukifanikiwa kupata eneo pale njiapanda ya kwenda Ilazo na Meriwa Dar road, nina hakika utafanya biashara nzuri sana eneo lile kwasababu pana muingiliano mkubwa sana wa watu na pia ni njia kuu inayo elekea maeneo niliyo yataja hapo juu.
Na kwakuwa kuna wapita njia kwa wingi pamoja na bodaboda, pale panafaa pia kama utaweka biashara ya mihogo ya kukaanga.
3. Panaitwa 4 ways ni njiapanda inapo gawanyika kutoka Singida road kuelekea Nkuhungu.
Pale patakufaa sana kwa biashara ya kuchoma mahindi, pamoja na Mihogo ya kukaanga kwasababu watu wengi sana wanashukia na kupita eneo lile, pamoja na boda boda wapo pale kwa wingi, bila kusahau wanafunzi.
Pale ukiwa msafi, kwahakika hauto jutia.
4. Mkuu, eneo la chako ni chako sijaona mchoma mahindi na kapilipili kwa mbaali pamoja na vipande vya liomao.
Pale chako ukipata nafasi patakufaa sana kwasababu pana mzunguko mkubwa sana wa watu na pia ukiweza kuweka muhogo wa kuchoma, nina amini utafanya biashara uzuri kabisa.
Mkuu, ebu ngoja kwanza nikamae hapa, kuna kazi natakiwa niimalize leo ili nipate pesa ya kumalizia ule mjengo kule Nala.
Na madogo wanafunga shule leo, inatakiwa niangalie sehem yenye M-Pesa ili nikawatumie nauli please