Uchaguzi 2020 Ushindi mkubwa wa Rais John Magufuli, utatoka kwa wanyonge na Wananchi wa kawaida kabisa

Uchaguzi 2020 Ushindi mkubwa wa Rais John Magufuli, utatoka kwa wanyonge na Wananchi wa kawaida kabisa

Acha kuandika PUMBA! Kawafanyia nini wanyonge hadi wampigie kura? Hajiamini huyo na ndiyo sababu hataki kuisikia TUME HURU maana saa nne asubuhi tu atakuwa KISHAGARAGAZWA Nchi nzima.
Pusha kama wewe huwezi uelewa
 
Nyerere hakuwa hovyo namna hii tafadhali tutake radhi.

Wapinzani buanaah....

Haya mchungaji Chakwera,Rais MPYA wa Malawi MLIYEMSHABIKIA ameanza kazi....
Ameteua BARAZA la mawaziri la ajabu na kuamsha hisia....

Amejaza marafiki,ndugu,na baadhi ya wizara ameteua MUME(waziri) MKE(naibu)....

Sasa nawashangaa wamalawi waliotaka MABADILIKO halafu wanaanza kumzodoa😂😂😂😂😂

MAISHA NI ZAIDI YA KUPINGAPINGA.....
 
TAAHIRA mwingine huyu!!! Hata Mkapa baada ya kutosema chochote kile kuhusu TUME HURU sasa kauona ukweli na kwa kuwa hafurahii mwelekeo wa Nchi kaanza kuyasema yale ambayo GENGE lenu la WAHUNI linayahofia. Sauti za kuunga mkono kauli ya Mkapa zitazidi kuongezeka tu ndani ya GENGE LA WAHUNI na ZWAZWA wewe utabaki uking'aa macho.
2451446_ERFcWLLW4AIVOAq.jpg


Pusha kama wewe huwezi uelewa
 
Taka ngumu hizi! Zinahitaji dampo la kisasa kuchakatwa maana zimeanza kuoza
Yaani nataka nikirudi huko Tz Disemba,nikae na wanazuoni wa pale Mlimani niwaulize tatizo hasa la kuwa na wahitimu namna hii ni nini, na kama kuna yeyote anayeweza kufanya tafiti ili tukinge kizazi kijacho na mtindio huu wa mawazo.
 
Miaka 60 bado kuna wanyonge ukiwauliza hawa wanyonge kwanini wanaendelea kuwa wanyonge katika nchi ambayo ina rasilimali nyingi za utajiri na wachache nyinyi mnakuwa mamilionea na wengine mabilionea? Wanakosa jibu! MACCM ni JANGA linalolitafuna Taifa.

Nchi huru alafu kuna wanyonge?hivi kile chuo cha Kigamboni kinawafundisha nini siku hizi
 
Huwezi jua mbinu hizi ukiwa kilaza kama wewe
TAAHIRA mwingine huyu!!! Hata Mkapa baada ya kutosema chochote kile kuhusu TUME HURU sasa kauona ukweli na kwa kuwa hafurahii mwelekeo wa Nchi kaanza kuyasema yale ambayo GENGE lenu la WAHUNI linayahofia. Sauti za kuunga mkono kauli ya Mkapa zitazidi kuongezeka tu ndani ya GENGE LA WAHUNI na ZWAZWA wewe utabaki uking'aa macho.
2451446_ERFcWLLW4AIVOAq.jpg
 
Miaka 60 bado kuna wanyonge ukiwauliza hawa wanyonge kwanini wanaendelea kuwa wanyonge katika nchi ambayo ina rasilimali nyingi za utajiri na wachache nyinyi mnakuwa mamilionea na wengine mabilionea? Wanakosa jibu! MACCM ni JANGA linalolitafuna Taifa.
Inaona mingi jpm kawanyoosha kama rula
 
Yaani nataka nikirudi huko Tz Disemba,nikae na wanazuoni wa pale Mlimani niwaulize tatizo hasa la kuwa na wahitimu namna hii ni nini, na kama kuna yeyote anayeweza kufanya tafiti ili tukinge kizazi kijacho na mtindio huu wa mawazo.
Utoke kenya kuuza bar
 
Hahahahahaha eti mbinu. Hebu toa UJUHA wako hapa!!! Hakuna mbinu hapo ZWAZWA bali ni kutaka kuona Chaguzi HURU na za HAKI ili kumuondoa huyo dikteta madarakani. Kwani Mkapa anajua fika kwamba bila TUME HURU dikteta atang'ang'ania madarakani kama M7.

Huwezi jua mbinu hizi ukiwa kilaza kama wewe
 
Yaani nataka nikirudi huko Tz Disemba,nikae na wanazuoni wa pale Mlimani niwaulize tatizo hasa la kuwa na wahitimu namna hii ni nini, na kama kuna yeyote anayeweza kufanya tafiti ili tukinge kizazi kijacho na mtindio huu wa mawazo.
Utoke nje ya wapi hapo mbagala
 
Hawa wananchi wanyonge ni wakina nani?
Tatizo kubwa kwa sasa la vijana ni unafiki na kujipendekeza.
 
Kwakipi alichowafanyia wanyonge,kuwavunjia nyumba zao , kushindwa kuongeza mishahara, kushindwa kuajiri kwa miaka mitano,kupunguza mzunguko wa fedha,kujenga uwanja wa ndege chato kununua ndege,bila idhini ya bunge?
 
Nilipoona mwisho kuna namba za simu nikajua ni moja kati ya wale vijana ambao wapo kimaslahi zaidi
 
Ni akina nani hao wanyonge? Mbona nimekuwa nikisikia sana hii kitu wanyonge? Nchi hii kuna wanyonge na wasio wanyonge? Nani anawanyonga wanyonge hadi wanatambulika hadharani?
Hujiulizi kwanini WB imetuweka kwenye kundi la Lower Middle Income? Duniani sisi ndio wanyonge wenyewe sasa, hii inaleta maana gani? Maana yake ni kwamba hata kitaifa kunawanyonge pia. Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.
 
USHINDI MKUBWA WA RAIS JOHN MAGUFULI, UTATOKA KWA WANYONGE NA WANANCHI WA KAWAIDA KABISA.

Leo 13:45pm 09/07/2020

Niseme wazi ya kwamba,Silaha kubwa ya Rais John Pombe Magufuli ni wananchi tena wale wanyonge na wa kawaida kabisa,na ushindi mkubwa wa Rais John Pombe Magufuli utatoka kwa asilimia mia 100% kwa mwananchi wa kawaida ambaye maono yake yamebebwa na Rais John Pombe Magufuli.

Kwa nini nasema hivi, nasema hivi,kwa sababu ya namna ya uongozi wake wa kinyerere (Mwalimu Nyerere Model) ambayo inakinzana na ile tabia ya Azimio la Zanzibar ambalo lilipinga Azimio la Arusha la Mwalimu Julius Nyerere likisema Tanzania si ya Wakulima na Wafanyakazi pekee bali Wakulima, Wafanyakazi na Wafanyabiashara,

Baada ya Azimio la Zanzibar kupita tuliona Wafanyabiashara wakihodhi nafasi za Uongozi ndani ya Chama Cha Mapinduzi na Serikalini, ndipo rushwa ikaanza kuitwa takrima na ufisadi ukatamalaki, Wafanyabiashara waliingia katika Uongozi wa Chama na kuweka msuli wa pesa,ikawa bila pesa haupati Uongozi,

Kwa hiyo Azimio la Zanzibar lilikuwa na maslahi binafsi ya watu wengi ndani ya Chama Cha Mapinduzi wakati ule,hivi sasa Chama Cha Mapinduzi kimerudi katika misingi yake ya Azimio la Arusha ya kwamba Chama Cha Mapinduzi ni Cha Wananchi na sio matajiri wachache.

Lengo la mwananchi wa kawaida ni kutaka kupata Rais anayeweza kuwakilisha matakwa ya wengi walio na maisha ya kawaida kabisa.Rais John Pombe Magufuli anaweza kuwakilisha matakwa ya wengi tena hasa sisi wananchi wa kawaida kabisa,Rais John Magufuli amebeba maono ya kututoa katika umasikini na kutupeleka Uchumi wa kati ambao unaletwa na Viwanda vitakavyoleta ajira na kipato cha mfukoni,

Tumepata tunu ambayo ni kama dhahabu pale Geita, almasi pale Mwadui ama Tanzanite pale Mererani,Sisi Watanzania tunatakiwa kuikumbatia tunu hii,maana kimsingi sisi ndo wenye ilani,katiba iwe ya Chama ama Serikali.

Ningekuwa na Mamlaka ningesema aende na Urais kama Wachina walivyomwambia Xi Jimpin aendelee na Kama Warusi walivyomwambia Vladmir Pitin aendelee baada ya kumuona akienenda sawa sawa na Baba wa Mageuzi nchini Urisi Joseph Stalin,

Sasa kwa nini tuendelee kucheza upatu? Maana anaweza akaingia Rais mwingine wote tukashangaa,Nadhani, huu ni wakati mzuri wa kujifunza siasa za uwajibikaji, na kutokuoneana haya,tuite koleo koleo na kijiko kijiko na kuambiana ukweli pale tunapoona mambo hayaendi sivyo,kwa maslahi mapana ya Taifa letu la Tanzania.

Naomba nikiri ya kuwa viongozi wote wa CCM waliowahi kutokea kwenye nafasi ya Urais ni wazuri sana na kila mmoja kwa wakati wake alifanya vyema sana, ikiwa pamoja na kuandaa njia na mazingira ya ujio wa Rais John Pombe Magufuli.

Nikiri tena ya kuwa kwenye uzuri kuna madaraja ya uzuri,kwa maono yangu Rais John Pombe Magufuli ni mzuri sana kuwazidi watangulizi wake na pengine ni Rais bora kupita Marais wote waliopata kutokea katika Afrika ya Mashariki,

Hoja kubwa ni kuwa na uwezo wa kuamua kufanya jambo wakati wengine waliona haliwezekani, Pili uwezo wake wa kuwajibisha viongozi hata kama wanaurafiki wa karibu.

Kwa hayo machache sana sioni kwa nini tunawalaumu wanaosema kuwa aongezewe muda,Kama anaweza kuliko historia inavyoonyesha kwa nini asiongezewe.

Binafsi sioni shida kabisa kabisa na wala sina hila yeyote wala manufaa kwenye uongozi zaidi ya kufurahia jinsi chama changu kinavyopaa kwa hivi sasa kikionyesha Mageuzi makubwa ya kiuchumi,

-Rejea Sifa za Profesa Lumumba kwa Rais John Magufuli.

=Kwa miaka 6 tu Rais Kenyata kufikia 2019 alikuwa ameshakwea pipa Mara 92 kuhudhuria shughuli mbalimbali nje ya nchi shughuli nyingi zikiwa Ni kuaapishwa na kutafuta Mikopo kwenye mataifa ya Kibepari.

=Kwa miaka 5 Rais Magufuli katoka nje ya mipaka Mara 8 ikiwa na utofauti wa safari 84 alizokwea pipa Rais Uhuru Kenyatta kwenda nje ya Kenya.

Safari ya kwanza ya Rais John Magufuli ilikuwa mwaka 2016 nchini Rwanda,Alikutana na mwenyeji wake Rais Kagame kuzindua one stop border na kufungua Daraja la Rusumo.

Safari ya Pili, Rais John Magufuli alisafiri kwenda Uganda kwa Jirani yetu Museven. Lengo la Safari hii ilikuwa Ni mazungumzo ya Bomba la mafuta toka Uganda kuja Tanzania.

Safari ya Tatu,Rais Magufuli alitembelea Kenya kwa Jirani Mwingine hii ilikuwa safari ya Mwisho kwa mwaka 2016 ambapo alikwenda kuimarisha biashara ya Kenya na Tanzania.

Kitako cha andiko langu ni kukuonyesha umuhimu wa safari nane zenye tija alizofanya Rais John Magufuli akienda nje ya nchi tofauti na safari 92 alizofanya Rais Uhuru Kenyatta kwenda nje ya Kenya,kwa ufupi hili ni eneo ambalo tulikubaliana kwenye Ilani yetu ya Chama Cha Mapinduzi kuwa tutalidhibiti ili fedha hizi tuzitumie kuondoa umaskini wa watanzania.

-Hoja ya Kuongezewa muda,

'Term limits' zina faida zake. Na lengo na madhumuni ya term limits ilikuwa ni Watanzania kujipa fursa ya kusahihisha makosa yetu ambayo tumeyatenda kidemokrasia, hasa tukizingatia kuwa demokrasia ni uhuru wa kuchagua ikiwa ni pamoja na kuchagua kwa usahihi au kwa makosa.

Ninakumbuka kwenye Awamu ya Pili ya Mzee Mwinyu, tulikuwa na changamoto kadhaa,hata tukamuona Augustino Lyatonga Mrema akitumia staili yake ya kupiga chenga kutaja madhaifu ya Serikali,lakini "term limit" ikatuokoa.

Kwenye Awamu ya tatu ya Mzee Mkapa tuliona gharama kubwa ya kuendesha mashirika ya Umma hata tukaanza kuyabinafsisha kwa kushindwa kuyaendesha na kuwalipa wafanyakazi tuliokolewa na "term limit".

Kwenye Awamu ya nne ya Mzee Kikwete tukiendelea kula matunda yetu ya Uhuru,tukashuhudia skendo kubwa ya Richmond na Escrow zilizotokana na tatizo la ukosefu wa Umeme wa Uhakika,tukaokolewa na "Term limit".

Rais Magufuli, ni kiongozi ambaye amejipambanua kiuwezo siyo tu katika bara la Afrika, bali ulimwenguni,kusita kumuongezea muda JPM kwa mategemeo ya 'good luck' ya kumpata mwingine kama yeye haitakuwa busara. Nchi haziendeshwi kwa kutegemea 'good luck'.

Rais Magufuli amefuta karibu malalamiko yote ambayo wapinzani au nisema Taifa lilikuwa linalalamikia katika miaka 30 iliyopita,Mathalani, mambo ambayo Rais Magufuli ameyafanya katika awamu yake ya kwanza yanasomeka kama miujiza au yanaonekana kama ndoto,

Mambo makuu aliyofanya Rais Magufuli kwa Taifa la Tanzania ni mengi na makubwa yanayoajabiwa na dunia nzima. Lakini Magufuli anatumia Katiba ile ile ambayo watangulizi wake waliitumia,Hii maana yake ni kwamba tatizo letu Tanzania halikuwa katiba,bali udhaifu wa watu wanaosimamia Katiba yetu.

Imetuchukua Watanzania miaka 30 (thelathini) kumpata kiongozi wa aina ya Mh. Magufuli - Mtu ambaye ana ushujaa,uthubutu na uzalendo wa kipekee na upeo wa kujitolea usio kifani,Rais mstaafu, Alhaji Ali Hassan Mwinyi alipokiri hadharani kuwa "sisi tulikuwa waoga" wakati akiyapa tano mafanikio ya Rais John Magufuli ya mwaka wake wa kwanza alitoa ukweli mwanana.

Mimi ni muumini wa kweli ya kuwa hakuna mtu hapa duniani unaweza kuwa "indispensable" kwa maisha ya Taifa lolote. Lakini, itakuwa ni si busara kusitisha uongozi wa mtu ambaye ana uwezo wa pekee kwa sababu tu hakuna mtu ambaye ni "indispensable" kwa maisha ya Taifa letu. Aidha Tanzania itakuwa inajidanganya ikifikiri kuwa tuna akina Magufuli wengi. Hiyo si kweli,kulikoni ilituchukuwa miaka 30 kumpata huyu tuliyenaye, iwapo tunao wengi?

Kumuomba Mh Rais Magufuli akubali kuendelea kupitia kura za maoni (referendum) itakuwa ni sehemu ya Katiba; lakini kubwa kupita yote ni kwamba hii itakuwa ni kwa manufaa ya kila mwananchi wa nchi yetu ya Tanzania.

Ni kweli kuwa pamoja na mazuri yote ambayo Rais Magufuli anatufanyia Watanzania, wapo watu katika Chama chake na katika Serikali yake ambao hawapo na yeye na wanamuhujumu. Wengi wa hawa ni wale ambao mirija yao imekatwa - watu ambao walikuwa wanalifuja Taifa letu kwa manufaa yao,

Nimalizie kwa kusema baadhi ya nchi zimeamua kuwekeza kwenye tunu zao kama Urusi na China kulingana na mfumo wa nchi zao. Zipo pia nchi zilizoendelea kama zile nchi za kifalme hazina ukomo pengine ni utamaduni wao lakini cha kufurahisha nchi kama USA, wingi wa kura siyo ambao unamchagua Rais wa Marekani na mfani tu Hillary Clinton alishinda kwa kura lakini Rais Trump kachaguliwa na wajumbe wa Seneti, Hapo ujiulize maswali ya kutosha.

Nimalizie kwa kusema,tunaweza kutumia Demokrasia hiyo hiyo kufanya yaliyofanyika China, Urusi na nchi kama Rwanda, hebu wekeni karesearch kadogo kwa wananchi kawe kanauliza maswali mawili tu

1. Unadhani Magufuli anapashwa kupewa miaka mingine 10 ya ziada?

2. Unadhani Magufuli hapashwi kupewa miaka mingine 10 ya ziada?
Halafu uone wananchi watasemaje, tena maswali yakaulizwe kwenye ile mikoa yenye upinzani mkali kama Arusha, Mbeya na Kigoma.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business
-Master's in Leadership and Management.

-Research; Assessing Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
Umejitahidi kuweka number ya cm lkn ungalimshauri huyo boss wako akubali kuweka tume huru
 
Back
Top Bottom