Uchaguzi 2020 Ushindi mkubwa wa Rais John Magufuli, utatoka kwa wanyonge na Wananchi wa kawaida kabisa

Hujiulizi kwanini WB imetuweka kwenye kundi la Lower Middle Income? Duniani sisi ndio wanyonge wenyewe sasa, hii inaleta maana gani? Maana yake ni kwamba hata kitaifa kunawanyonge pia. Mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni.

Unajisikia fresh kabisa kujiita mnyonge!!..

By the way ni maamuzi yako na nayaheshimu
 
Yaani nataka nikirudi huko Tz Disemba,nikae na wanazuoni wa pale Mlimani niwaulize tatizo hasa la kuwa na wahitimu namna hii ni nini, na kama kuna yeyote anayeweza kufanya tafiti ili tukinge kizazi kijacho na mtindio huu wa mawazo.
Sasa wahadhiri wenyewe ni kama Dr Bashiru unategemea nini?
 

Wanyonge ni mtaji wa wanasiasa, wanyonge ni futureless people,futureless people ndio uamua hatma ya Nani awe kiongozi.Wanyonge ndio rahisi kuwapropaganda
 
Ni wanyonge gani Hao..je ni wale waliokuwa wauza mandazi na kukamatwa walipe elfu 20.wakayti mitaji yao ni 200 mpaka 5000?ni wanyonge gani Hao?
 
Wanyonge gani unaona sema??? Yule meneja wa tarula Arusha aliyefukuzwa kazi kwa uonevu uliotukuka???
Prof Assad aliyedhalilishwa na kufadhaishwa kwa kusimamia ukweli?? Tundu lissu aliyepigwa risasi 16 kwa kusimamia haki na ukweli??? Au wanyonge gani unaowasema???
 
Kumbe unyonge wetu mtaji wenu, haitatokea mkatufanya imara kama unyonge wetu ni ajira kwenu
 
Labda mtoa mada nikuilize tena! Wanyonge unaowazungumzia ndo wale wakulima wa Songwe na Mbeya mliowapiga marufuku kuuza mazao yao kwa wafanyabiashara ambapo walikuwa wanauza kwa elfu 4000 kwa kilo na mmewalazimisha kuuza kwa vyama vya ushirika ambapo wanauza kwa elfu mbili kwa kilo na kuzidi kuwa maskini??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…