Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi

Numbers don't lie
Dkt. Magufuli ameshinda kwa kupata kura 12,516,252 (sawa na 84.4% ya kura halali)

Tume imesema walikuwa na jumla ya watu 29,754,699 waliojiandikisha kupiga kura, na waliopiga kura walikuwa 15,091,950. Kura halali zilikuwa 14,830,195
View attachment 1616177
Paskali
 
JPM ameshashinda...

Ni bora wapinzani wakajipanga upya kuidai tume huru ya uchaguzi kama ile ya IECB ya Kenya then 2025 wajaribu Tena...

Hekima na busara zitawale kipindi hiki kigumu kwao....

Kila la heri JPM Katika hii miaka 5 ijayo ambayo tunaamini UTALIPAISHA TAIFA LETU..
 
Mkuu fundimchundo , nimeguswa na bandiko lako hili, mimi ni realist, ma realists wote, hata kama hau support kilichofanyika, lakini when kumetokea kitu kilichotokea, and there is nothing anyone can do to change the situation, ma realists wote tunakubali matokeo, katika muktadha wa appreciating the situation and suggest the best way forward out of the situation.

Vyama vya siasa sio mali ya watu, viongozi, ni mali ya umma, hivyo maamuzi yoyote yatafanywa kwa kutanguliza maslahi ya umma.
Kwenye hili, maslahi ya umma ni kwa wapinzani hao wachache waliopata fursa ya kuingia Bungeni, waingie waka salvage what is left of opposition in Tanzania.

Nimekuleta hapa ili kukujulisha, kuwa tulishauri pia the best way forward, ukitoa ushauri mzuri, hata kama haukufuatwa, wewe unakuwa umetimiza wajibu wako.

Mimi nimetimiza wajibu wangu.
Kama kosa langu ni kuukubali ukweli jinsi ile ulivyo, nalikubali kosa hili.

P
 
Uchaguzi ulikuwa wa haki na huru?

Umejibu hili?
Mkuu Kiranga, kwa vile wengi wanauzungumzia uchaguzi based on kilichotokea, mimi nimeanza kuuzungumzia zamani na matokeo ya uchaguzi wa 2020, niliishayajua tangu ile 2015 baada ya Jembe JPM, kuingia ulingoni.
Karibu pande hizi
P
 
Mkuu Kiranga, kwa vile wengi wanauzungumzia uchaguzi based on kilichotokea, mimi nimeanza kuuzungumzia zamani na matokeo ya uchaguzi wa 2020, niliishayajua tangu ile 2015 baada ya Jembe JPM, kuingia ulingoni.
Karibu pande hizi
P
Unafurahia na kubariki huu ubakaji wa demokrasia uliotokea 2020?
 
Mkuu Drifter, kwanza asante kwa mchango wako, very objective, kiukweli tangu nimepandisha uzi huu, wewe ndio mtu wa kwanza kunielewa, kwasababu, kiukweli kabisa, hii jf ya sasa, tuna watu wachache sana, wenye kuweza kusoma bandiko na kisha kujiuliza what is the motive behind.

Chama cha Mapinduzi ni chama cha ukweli na haki, kiliasisiwa na Mwalimu Nyerere, mpenda haki na mtenda haki. Baada ya Mwalimu, CCM ilipitia mageuzi na kuishiwa kuhodhiwa na wenye fedha, hivyo kuzalisha kada kubwa ya makada wa CCM ambao ni makada maslahi, na kwenye uchaguzi, wanakuwa wako tayari kutumia mbinu zozote kushinda uchaguzi. JPM alipoingia, amekuja kuibadili CCM kuirudisha ile CCM ya Nyerere. Sasa ndani ya makada wa CCM, kuna makada wa aina mbili, kuna "CCM Die Hard", hawa ndio wanaotaka kuhakikisha CCM inaupondaponda upinzani na kushinda kwa asilimia 99.9% kwa kutumia mbinu zozote.

Tupo sisi makada "Modern CCM" ambao kutokana na good track ya kazi nzuri ya JPM, CCM innashinda kwa mshindi mzuri safi na clear victory, kushinda kwa haki bila kufanya figisu figisu zozote.

Kwa vile Bunge letu ni Bunge la vyama vingi, mimi naamini kuna baadhi ya wana CCM very genuine, hakupenda kuona baadhi ya wapinzani wakishindwa akiwemo mtu kama Zitto!. Lakini kutokana na wapinzani kukataliwa na wananchi, ili Bunge lichangamke, zile kamati 2 za oversight committee, PAC na LAAC, lazima ziongozwe na wabunge wa upinzania ambao ni vichwa vya ukweli, kwenye hao wabunge wote sijaona watu wa kalibre hiyo ndio maana kila siku, tunamuomba Mwenyekiti wetu, JPM, katika zile nafasi zake 10, awateua wapinzani 4, Zitto, JJ Mnyika, Mbatia na kale kabinti Queen Sendiga.

Ili CCM itawale vizuri inahitaji Upinzani makini, ndio maana kila uchao, naibalasa Chadema humu na ACT Zanzibar, waache ujinga wa kususa. Ili kusasa kwa akili ni kususa kama kwa kususa huko utaachieve something, lakini kususa tuu for the sake of kususa, huku you won't achieve anything huu ni ujinga!.

Karibu tena.
P
 
Hizi post zako za nyuma ndyo zngekufanya upate teuzi. Ila ulivyoamua kuwa mnafiki hata haja ya kukupa teuzi haipo tena.

Unadhani Polepole alipata teuzi sababu ya kuongea pumba????
 
Wanabodi, mimi ni miongoni mwa wana jf, tuliandika mengi kumhusu rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hivyo kipindi hiki cha maombolezo, napitia baadhi ya mabandiko kwa ajili ya kumuaga rasmi.

Japo umetangulia, lakini kauli zako, maono yako na kile ulichokiamini, kitabaki na sisi Milele.
Sisi tulikupenda, lakini Mungu amekupenda zaidi.
Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe!.
Raha ya Milele Umpe Ee Bwana, na Mwanga wa Milele, Umuangazie, Apumzike kwa Amani...Amina x3.
RIP Dr. John Pombe Joseph Magufuli
Buriani ya kuonana...
Paskali
 
Pascal nasikitika kukuambia kuwa
Hua nashindwa kukuelewa unashindwaje kuielewa CCM jinsi inavyowatendea wapinzani kinyume kabisa na matakwa ya katiba na wewe unakaa kimya tu.
Mkuu lee van cliff , karibu mitaa hii uone kimya changu.
P
 
Kakweli Pascal Mayalla ulionya sana ndugu yako akashupaza shingo. Ona sasa
 
Japo naunga mkono hoja, ya "ukisusa sie twala...," na siungi mkono hii tabia ya kususa susa.... Swali kuhusu tabia ya kususa, kugomea au kuzira: Je, si tabia za kike, si utoto? na hapa Ujio wa Lowassa CHADEMA: Kuna kundi wamesusa, wanapanga kurejea CCM! na Kufanya kosa si kosa, kosa kurudia kosa. CHADEMA is almost dead, due to deadly mistakes! This is your only survival -- do or die. Msirudie kosa

Lakini kama wanasusa for genuine reasons za kutotendewa haki, kama tulivyo shauri hapa Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi

Najua by now wasoma trends wanajua the consequences za kutotenda haki kwenye uchaguzi, sisi washauri huru tuliisha shauri kabla Ombi Maalum, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2020, Uendeshwe kwa Ceteris Peribus, Sio Kwa Mutatis Mutandis. Tutabarikiwa! hivyo Shaka asijitape wakisusa kwa kutetendewa haki sisi twala, badala ya kula wakajikuta wao ndio wanaliwa vichwa!.

Karma haina mswalie Mtume, walishindwa kumlinda Blaza, karma ikafanya yake!, ili kumlinda Maza na karmic consequences, sisi tunao ijua karma, lazima tumsaidie Maza kwa kumweleza ukweli ili aepuke the consequences na yeye asije... hivyo kwa kuanzia tumemshauri Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
P
 
Mkuu Bishweko , asante kwa mchango wako, ila kuna watu ukishawajua ni makada wa kile chama chetu pekee, unadhani wote ni wa kereketwa au wafurukutwa, wengine ni makada wazalendo, wanasimama na haki bin haki, kada mimi ni mmoja wapo, angalia mada zangu hizi kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa 2019.
P
 
Hiki ulichokisema kura kuhesabiwa Kilatini ndicho Nape alichokisema!, kimekuwa kinafanyika, sasa watu wanashangaa nini?.
P
 
Hiki ulichokisema kura kuhesabiwa Kilatini ndicho Nape alichokisema!, kimekuwa kinafanyika, sasa watu wanashangaa nini?.
P
Tangu nimesikia ya Nape sijasema chochote! najua alichosema ndicho na mara nyingi Nape ni Mkweli.
Alisema goli la Mkono na sasa kuhusu wanavyotangazwa.

Hata hivyo nawaelewa Wananchi wanaoshangaa na waliochukizwa na kauli za Nape.
Fikiria hivi, kuna INEC ikisemwa ni Tume huru ya Uchaguzi. Upande mwingine tunasikia 4R halafu tunasikia 'Uchaguzi utakuwa wa Amani'' na mwisho '' yale ya 2020 hayatarudiwa tena.

Wananchi wanahasira kuhusu udanganyifu na aiyethibitisha hilo ni kiongozi mwandamizi kama si mwendawazimu. Wananchi walitegemea baada ya kauli hiyo CCM na Serikali wajitenge naye, lakini bado wamekumbatia. Hilo tu ndilo linawafanya Wananchi washangae !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…