Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi

Serikali na CCM lao moja. Wamejinasibu kuwa wamefanya kazi nzuri sana kwa miaka minne na wanahitaji kushinda kwa 100% ili kuuaminisha umma kuwa kweli inakubalika.

Mfanano wa dhuluma ya kisiasa inayoendelea nchini kote kwenye mchakato huu wa uchaguzi, unaonesha, kisayansi kuwa kuna maelekezo yanayofanana sana ambayo yametolewa.

Mimi nina imani kuwa ule mkutano ambao 'mtukufu' wa magogoni aliuitisha na kuufanya na watendaji wa kata zote nchini ulikuwa na malengo ya kuishindisha CCM.

Uongozi wa serikali hii umeshindwa kwa sababu ya kukubali kuendeshwa puta puta na mheshimiwa sana. CCM kimeshakosa ubunifu au ujasiri wa kumdhibiti mwenyekiti na sasa anaifanya hii nchi kama yake. Hatuwezi kuuvumilia ujinga huu kwa muda mrefu zaidi!
 
Matola,
Nadhani hili angelifanya Mufti kwa kuwa yeye ndiye anatambulika na serikali kuwa kiongozi wa Waislam wa Tanzania Bara.

Waislam wanalia na Allah kila siku katika sijda zao.
 
IDD Amini Dada aliwafanyia waganda mambo mengi ya maendeleo..

~alinunua Ndege 62
~aliingiza UG nchi za OIC
~alijenga reli,barabara
~aliwafukuza wahindi na kuwatajirish wazawa
~aliwapa vyeo jamaa wa kabila lake

*Lakini hakuheshimu katiba wala haki za wananchi

Alijifia mpweke huko uarabuni.!!
 
Demokrasia gani ili hali mwenyekiti kanyofowa kipengele cha ukomo na ukienda mahakamani unafukuzwa chama,toa boriti kwenye jicho lako kwanza!
 
Demokrasia gani ili hali mwenyekiti kanyofowa kipengele cha ukomo na ukienda mahakamani unafukuzwa chama,toa boriti kwenye jicho lako kwanza!

Bora umekuja, kama mwenyekiti anafanya hivyo kinyume na katiba hicho chama kifutwe. Hatutetei uhuni. Kisha nenda kwenye ule uzi wa 20t ukatoe majibu deni kwanini linapanda, huku miradi ni ya pesa za ndani.
 
Ziliwekwa taratibu ili zifuatwe. Ukishindwa kiziguata, unaondolewa tu. Hata Bunge la Congress la Marekani sasa liko kwenye mchakato wa kutaka kimuondoa Rais Trump madarakani kwasababu amekiuka utaratibu. Simple!
Ni Kweli Sheria Zimewekwa Ili Zifuatwe Ila Ajabu Ni Kwamba Vyama vya Chadema na A.c.t Wametangaza Kujitoa Kwenye Huo Uchaguzi, Ila Bado Waziri Wa Tamisemi Analazimisha kubandika Majina Ya Wagombea Ambao Vyama Vyo Vimejitoa Kwenye Huo Uchaguzi.

Swali:
Ikiwa Chama Kimejitoa kwenye Uchaguzi, Hao Wagombea Ambao Bwana Jaffo Anadai Bado Majina Yao Yatakuwepo Kwenye Karatasi Ya Kupigia Kura Bila Kujari Kama Vyama Vyao Vimejitoa Watasimama Kama Wagombea Wa Chama Gani?.

Au Siku Hizi Tanzania Tuna Wagombea Binafsi?.
 
Nilisema "too late" CHADEMA walipojitoa na nasema leo "too late" kumshauri Rais aruhusu wagombea waloenguliwa. Kwa CHADEMA ilikuwa too late kwa sababu baadhi ya wagombea walishapitishwa na hivyo kwenye karatasi ya kupigia kura watakuwemo na hii ndo mbinu ya chama tawala. Ni too late kwa Rais kwa sababu vyama vimeshatangaza kususia uchaguzi. Maji yakishamwagika hayazoleki. Kwa haya mengine naunga mkono hoja.
 
'Kutokana na kasi ya rais Magufuli kutuletea maendeleo ya vitu vya kuonekanika, Midege, Reli ya SGR, Mabarabara nchi nzima, madaraja ya Juu kwa Juu, Mradi wa umeme wa Stigler , Tanzania ya Viwanda, Elimu Bure, Vituo vya Afya kila kuna, etc, etc, just to mention but few, vinaipa CCM fursa ya ushindi wa kishindo cha wazi kabisa katika uchaguzi wowote nchini Tanzania kati ya sasa hadi 2025, hivyo mamlaka zinazosimamia uchaguzi huu, waruhusuni wagombea wote waliopitishwa na vyama vyao wapite tuu bila kujalisha kama wanekidhi sifa na vigezo, ili tuu kuruhusu ushindani wa haki, ushindani wa uwazi na mshindi apatikane kihalali katika uchaguzi huru na wa haki'.

Nimekuelewa vizuri mkuu Pascal Mayalla
 
Paskali wewe kama mwandishi mwandamizi nlidhani unafahamu kuwa mkuu hapendi ushindani na hawezi kuruhusu hilo jambo litokee hata kidogo
 
Matola,
Nadhani hili angelifanya Mufti kwa kuwa yeye ndiye anatambulika na serikali kuwa kiongozi wa Waislam wa Tanzania Bara.
Pascal kumradhi kidogo! nachepuka nimgutie Matola neno. Matola nenda kule ukumbini ukalianzishe, nataka kumshika Mohamed Said 'shikio'

Mohamed, huyu Mufti ukisema ni wa Bakwata, leo naona wamtwisha zigo !
Au ndio ule usemi kutoka Buckingham Palace '' Even a broken clock is right twice a day''

Waungwana Jamvini samahani turudi kwenye mada ya Pascal , ya ngoswe tumwachie ngoswe mwenyewe.

Turudi kwenye mada tafadhalini
 
Kwanza hao wagombea, maeneo mengi ambayo tumeweza kupata taarifa zao, wamepokea uamuzi wa vyama vyao wa kutoshiriki uchaguzi najisi kwa mikono miwili.

Maeneo mbalimba vyama vimewaandikia na wagombea wamekwishawaandikia wasimamizi wa uchaguzi uamuzi wa kujiondoa.

Sasa Jafo huo upuuzi wa kubandika majina ya waliojiondoa sijui anautoa wapi!
 
Mkuu kuna mambo mawili. Mosi, muda wa kujitoa. Je, walijitoa kwa wakati? Pili, mgombea kama mgombea amewasilisha barua ya kujitoa? Kama hajawasilisha barua hiyo, unamuondoaje? Kumbuka kuna kanuni na taratibu za kufuata kuhusu hili. Na hili mkuu ndilo wanalokosea Chadema. Wanafikiri kila kitu kinafanyika tu (atavism).
 
Kama wagombea wameandika barua za kujitoa "kwa wakati" nitashangaa kama majina yatarudishwa kama wagombea. Lakini, Mkuu Bams ebu niambie, kanuni zinasemaje kuhusu muda wa kujitoa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…