Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi

Ushindi mtamu ni ushindani katika uwanja sawa, sio ule wa mezani. Magufuli, kasi yako ni ushindi wa kishindo. Ruhusu ushindani wa haki, sawa na wazi

Pascal wakati mwingine huwa unanishangaza, unasema Magufuli aingilie kati suala hili wakati ndo mastermind wa tatizo? wale watendaji walipoitwa ikulu hukusikia au ulikuwa nje ya nchi? hata kama ulikuwa nje ya nchi mitandao ipo definitely habari uliipata.
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu, nilisikia tuu kuwa ma VEO na ma WEO waliitwa Ikulu na mkutano ulikuwa live, lakini mimi sikuwepo nchini ns wala sikuwahi kufuatilia waliutiwa nini, ila just by ordinary common sense, na VEO na ma WEO ndio shina la The Executive, hivyo yeye kama Mkuu wa Mhimili huu has all the rights kuwaita kukaa nao, kuzungumza nao, kusemezana nao, kuwasikiliza changamoto zao na kuwapa maelekezo yoyote halali kwa mujibu wa majukumu yao. Kama kuna maelekezo yoyote specific kuhusu hili la uchaguzi wa serikali za mitaa aliyatoa, na ndio yamesababisha hali hii, please share maana mkutano ulikuwa live.
P
 
Nikikumbuka ule ushiondi wa 99% serikali za mitaa nacheka sana hahaha
Wewe cheka tuu, wakati wenzenu wanasherehekea ushindi huo wa kishindo, uliopatikana katika uchaguzi huru na wa haki, ombi langu, endelea kucheka ila usije humu kutulilia baada ya uchaguzi mkuu wa 2020.
P
 
Simba wanawakilisha wapinzani na Yanga wanawakilisha chama pendwa CCM. Angalia Simba siyo wamoja mwone Manara na hasa wakifungwa. Can not collect themself and come to terms with results. Hongereni sana Yanga Shishimbi et al; Hongereni CCM.
 
Wewe cheka tuu, wakati wenzenu wanasherehekea ushindi huo wa kishindo, uliopatikana katika uchaguzi huru na wa haki, ombi langu, endelea kucheka ila usije humu kutulilia baada ya uchaguzi mkuu wa 2020.
P
Hakuna la kufanya.Mwizi kawazidi nguvu.

Sana sana ni kujipa moyo kuwa siku za mwizi ni 40 tu.
 
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu, nilisikia tuu kuwa ma VEO na ma WEO waliitwa Ikulu na mkutano ulikuwa live, lakini mimi sikuwepo nchini ns wala sikuwahi kufuatilia waliutiwa nini, ila just by ordinary common sense, na VEO na ma WEO ndio shina la The Executive, hivyo yeye kama Mkuu wa Mhimili huu has all the rights kuwaita kukaa nao, kuzungumza nao, kusemezana nao, kuwasikiliza changamoto zao na kuwapa maelekezo yoyote halali kwa mujibu wa majukumu yao. Kama kuna maelekezo yoyote specific kuhusu hili la uchaguzi wa serikali za mitaa aliyatoa, na ndio yamesababisha hali hii, please share maana mkutano ulikuwa live.
P

Pascal ng'wanamayalla,
Hivi unajua kile kikao Cha Magufuli pamoja na VEOs na WEOs Kuna maelekezo MAALUMU WALIYOPEWA NA MAGUFULI ILI KUHAKIKISHA CCM INASHINDA KWENYE UCHAGUZI WA SM?
Ushahidi:
1. Pesa waliyolipwa ilikuwa ni "TAKRIMA" tosha ya kuwafanya walainike kutekeleza maelekezo ya Mkuu...! TAKRIMA ni lugha inayotumika ndani ya CCM badala ya RUSHWA.
2. Wakti wa kikao kuna kipindi Magufuli aliongea na Hawa jamaa akiwa OFF LINE/AIR.....! Hapo ndipo maelekezo ya kibabe yalipotolewa....!
 
Mkuu mayalla, wewe siyo mtu mdogo kwenye hii Tanzania, Hakuna siku umeona dosari za utendaji wa magufuli, na kama ulijaribu kumkosoa ni kijisafisha mbele za watu.
Duh...!.
Karibu mitaa hii ushuhudie jinsi ninavyosifu na kupongeza!.
P
 
Wanabodi,

Sitaki kuingia ndani kwenye technicalities zilizopelekea wagombea wa upinzani kuenguliwa, bali natoa wito kwa rais Magufuli aingilie kati hali hii au yeye mwenyewe kama rais wa JMT, au kupitia kwa msaidizi wake Waziri Jaffo wa Tamisemi, ayafumbie macho makosa yote madogo madogo ya wagombea wote wa vyama vyote walioenguliwa kwa sababu zozote, ziwe ni za kweli za halali au ni figisu, ayafute na watoe amnesty ya jumla kwa kila aliyegombea apitishwe tuu hivyo hivyo despite all the odds ili Tanzania tuingie kwenye Uchaguzi Mkuu mwakani kwa ushindani wa haki, uwazi na usawa kwa vyama vyote kutendewa haki sawa, kwa demokrasia kuachwa kufuata mkondo wake, hivyo waliosusa wote kwa kuweka mpira kwapani warudi uwanjani kipute kipigwe.

Ushindi mnono na mtamu wa raha ni ule ushindi unaotokana na ushindani halali wa haki unaopatikana kwa kuendeshwa kidemokrasia kwenye uwanja ulio sawa, level playing ground na sio uwanja tange, wala sio ushindi wa mezani!.



Hivyo natoa wito kwa serikali ya CCM, chini ya Jemedari wake, JPM, kiukweli labisa, hata kabla ya uchaguzi, CCM tayari imeishashinda kwa ushindi wa kishindo sio tuu huu Uchanguzi wa Serikali za Mitaa, bali hadi Uchanguzi Mkuu ujao wa mwakani 2020 kutokana na sababu za ki political social dynamics ya Magufulification nilizoeleza lakini ili CCM iweze kuufurahia huo ushindi kwa furaha ya kweli na hivyo kusheherekea ushindi huo, lazima CCM ishinde kwenye ushindani wa kweli, ushindani wa haki na ushindani wa usawa na sio kupata ushindi kwa kufanya figisu ili washindani wako wasuse, watie moira kwapani na wewe upewe ushindi wa mezani. Ushindi wa hivi sio ushindi mtamu, wala hauleti raha ya kudumu kwasababu karma itaingilia kati!.

Nakuomba Rais Magufuli jifanyeni kama mnacheza na watoto, wafungulieni njia watoto wote washindane kwa haki, washiriki kwenye uchaguzi huu na wa haki kwa uhuru na kwa haki sawa kwa vyama vyote despite mapungufu walionayo ili hata uchaguzi Mkuu wa mwaka kesho, wakati Watanzania watakapo irejesha Tanzania kwenye mfumo wa Chama kimoja CCM, iwe ni Watanzania wenyewe ndio wameamua kuichagua CCM kwa kishindo cha haki kupitia uchaguzi huru na wa haki ulioendeshwa na Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi ulioendeshwa kwenye uwanja sawa na tambarare wa ushindani, na sio CCM ishinde katika ule ushindani wa kugombea kisu cha makali kuwili, huku mshindani mmoja ameshika kwenye mpini na mshindani mwingine kwenye makali. Hivyo CCM ishinde kihalali kwa kufuatia kazi nzuri ya rais JPM na serikali yake na sio kwa sababu CCM ndio iliyokamata mpini!.

Hivyo Tanzania tukiamua kufanya uchaguzi huru na wa haki, unaofusta mfumo wa uchaguzi wa kidemokrasia ya ukweli, tunaweza. Mimi naamini kabisa kwa mambo makubwa na mazuri ya Rais Magufuli anayoyafanya, we have nothing to lose rais Magufuli akiruhusu demokrasia ikashamiri, akatoa haki sawa kwa vyama vyote kufanya siasa ikiwemo kuondoa zuio batili la mikutano ya siasa, bado rais Magufuli anaweza kuyaleta maendeleo yote aliyokusudia at the same time huku akiruhusu demokrasia nayo ikashamiri, ila ukweli utaendelea kubaki ni ukweli daima kwa katiba hii, Tume hii, sheria hii ya uchaguzi na kasi hili ya rais Magufuli, CCM bado itaendelea kutawala Tanzania milele.

Naomba nimalizie kwa ile kauli ya thread hii
"Ushindi Mtamu ni Ushindi Unaopatikana kwa Ushindani Wa Haki Kwenye Uchaguzi Huru na Wa Haki, Unaendeshwa na Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi na Unaofanyika Kwenye Uwanja Sawa wa Ushindani wa Kisiasa, Sio Ushindi wa Mezani!. Mheshimiwa Rais, Dr. John Pombe Magufuli, aka.JPM, Kasi Yako ya Maendeleo ya Tanzania Unaoifanya, Utailetea CCM Ushindi Kishindo Katika Uchaguzi Wowote, Tunakuomba Please Please Please, Ruhusu Tuu Ushindani wa Haki, Wazi na Usawa Kwa Vyama Vyote,
Utabarikiwa Zaidi na Zaidi, na Tanzania Tutabarikiwa.

Paskali
Japo kampeni zimeanza, its not too late ushauri wa bandiko hili ukifuatwa na haki ikatendeka hata kwa wasio stahili.
P
 
Pasckal kiaina bado unalilia teuzi.

na kiufupi ukishakuwa fisiemu haupaswi kuwa na hurumahuruma

ndio maana ulikatwa:hawakuelewi uko upande gani

Mayalla a.k.a Njaa yuko Kama Bundi!
Wakija ndege anadai naye Ni Ndege!
Wakija Wanyama naye anadai ni Mnyama.....🤣🤣
 
Hahaha ccm washindane?! Wote walishazoea kuteuliwa kushindana hawawezi.

mi nashangaa wewe ulipata kura moja ukaachwa kawe, Katambi anagombea, Gwajima anagombea, au nawe unasubiria kuteuliwa?!
 
Back
Top Bottom