Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Yawezekana madai ya jimbo la Tigray nchini Ethiopia chini ya chama kikongwe cha uasi cha TPLF yakawa na mantiki katika kile wanachokitetea, hata hivyo hawana nguvu ya kupigana na serikali kuu ya Ethiopia chini ya waziri wake mkuu Abiy Ahmed.
Tigray ni jimbo la kaskazini magharibi ya Ethiopia na limepakana na nchi ya Eritrea kwa masafa marefu na sehemu ndogo imepakana na Sudan.Tangu kuanza kwa mzozo huo baina yake na serikali kuu ya Ethiopia hawaonekani kufanya mashambulizi yoyote ya maana na huenda hasa baada ya kushambuliwa kwa mahodhi makuu ya silaha ya kambi za jeshi zilizo jimboni humo.
Kibaya zaidi vijana wengi wa Tigray ambao wangekuwa askari wa kupambana na jeshi la Ethiopia wamekuwa wakikimbia kuingia nchi ya Sudan kukimbia vita.Kwa upande mwengine jimbo hilo halionekani kuwa na uhusiano mzuri na nchi ya Eritrea ambayo karibuni imerudhisha uhusiano na Ethiopia uliopotea kwa miaka mingi tangu pale Eritrea ijitenge na Ethiopia kuliko sababisha vita baiana yao.
Hivyo mzozo huu wa Tigray kwa Ethiiopia huenda ikawa ni moja ya mambo yatakayomuongezea sifa waziri mkuu Abiy Ahmed kimataifa na nchini mwake pale atakapomaliza kuzima uasi wa jimbo hilo.
Si rahisi kwa Tigray kupata nguvu ya kujitenga kutoka Ethiipia kama vile ilivyokuwa kwa Eeritrea ambayo ina kitega uchumi kikubwa cha kupakana na bahari nyekundu.
Vijana wa Tigray wakipanga foleni kukimbia vita ili waingie Sudan.