Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Prof. Ibrahim Lipumba leo ameuelezea uchaguzi wa 2020 akiwa kwenye mkutano ulioandaliwa na TCD. Lipumba ametolea mfano Pemba ambako CCM walikuwa hawapati viti lakini 2020 wakabeba viti 12 ilhali Tanzania bara kati ya viti 214 upinzani uliambulia viti viwili pekee mpaka Unyanyembe wakaja na methali 'CCM hawana haya' jinsi hali ilivyokuwa ngumu.
Lipumba amesema hadi Kilimanjaro ambapo huwa wanatoka wapinzani safari hii vyote vimeenda CCM akidai hata kama wangechukua basi wangedanganya walau kidogo.
Lipumba amedai labda mama Kate Kamba(CCM) walikuwa wanajua ajenda iliyokuwepo lakini anaamini hata kubadilisha katiba ingekuwa nyepesi na tayari kulikuwa kuna maneno tuna Rais mzuri na vipindi viwili viwekwe kando na aliyepo aendelee kama China ilivyowezekana.
Lipumba amesema uchaguzi wa 2020, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aliuita Tsunami