Pre GE2025 Ushindi wa Lissu unamaanisha nini kwa Watanzania? Tunapata picha gani Uchaguzi Mkuu 2025? Samia atapumua? Ukabila kuisha?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hii ni Nuru mpya kwa CHADEMA
 
Mimi binafsi kama mtanzania nimefurahi sana, kwanza kwa kuwa huwa sipendi unafiki kabisa na siwezi hata kuuigiza kama ambavyo viongozi wapya tunawaamini hawatatufanyia unafiki wa kisiasa ambao ndio umetamaraki katika nchi hii. Imani yetu kwao si kwa kuwa tulimchukia mbowe na timu yake bali kwa kuwa wao viongozi wapya wameyaishi yale waliyoyaamini toka tunawafahamu kisiasa.

Pili uchaguzi huu unafurahisha kwani umewaonesha wazi wanaccm kuwa kuna kitu hakiko sawa katika siasa zao zinazoliongoza taifa hili pasipo ridhaa halisi ya wananchi. Wanalo la kujifunza ama waendelee kushupaza shingo na kutufanyia sanaa na wasanii wao hadi yaliyomkuta mbowe yawakute.

Pole kwa Mh. Mbowe, kazi ameifanya ya kutosha hadi tu pale kina Boni Yai na Yeriko walipompotosha na kutufanya tuyaone makengeza yake ambayo katika miaka yote 21 hatukuwahi kuyaona kwa kuwa tulimpenda.
 
Hivi vyama vilivyo sajiliwa siku Umma ukivitaka nakwambia Siasa itapendeza sana
 
Mama abduli ajiandae psychological
Kama uchaguzi ukiwa huru na wa haki. Bitozo anashika nafasi ya nne. Tundu Lissu nafasi ya kwanza kwa 95%. Bitozo ataambulia 1%. Watu wengi mno wana maisha magumu sana, vijana wengi mno hawana ajira miaka inakwenda hawana maisha kabisa.




Ila kama kawaida yao, wataiba kura watashinda.
 

..utawazuiaje Polisi na watendaji wa serikali kuengua wagombea wa upinzani, na kufanya hujuma dhidi ya wapinzani?
 
Sina hamu na hii serikali ya bi tozo a.k.a chura kiziwi

Sijapiga kura mda mrefu ila Mhe. Lissu akigombea lazima nikampigie kura no matter what!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…