Pre GE2025 Ushindi wa Lissu unamaanisha nini kwa Watanzania? Tunapata picha gani Uchaguzi Mkuu 2025? Samia atapumua? Ukabila kuisha?

Pre GE2025 Ushindi wa Lissu unamaanisha nini kwa Watanzania? Tunapata picha gani Uchaguzi Mkuu 2025? Samia atapumua? Ukabila kuisha?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wakuu,

Lissu amekuwa akiongelewa kama mtu mwenye misimamo, aliyenyooka, na siyo rahisi kuyumbishwa. Yeye na Heche imekuwa pea moja ambayo inaendana kwa kwenye misamamo na njia zao za kuongoza wote wakiongelea mabadiliko makubwa ndani ya chama na maeguzi kwenye siasa za Tanzania.

Baada ya ushindi wa Lissu kwenye nafasi ya Uenyekiti CHADEMA na Heche kama Makamu wake, inamaanisha upinzani utazidi kuimarika na kuongeza siasa safi nchini? CCM itaacha kuzembea na kuongeza nguvu kwenye kuongeza ubora wa huduma ili kuendelea kubaki madarakani?

Mchuano wa Uchaguzi Mkuu utakuwa moto na Samia kuhenyeshwa kwelikweli? Vipi ubande wa ubunge, unawaona upinzani wakipata viti vingi na kuwa na bunge lenye uwakilishi mkubwa pamoja na mchuano mkali hoja zitakapokuwa zinaletwa mezani?

Vipi ushiriki wa Watanzania kwenye masuala ya siasa? Tutegemee ushiriki mkubwa wa wananchi kwenye siasa na uchaguzi Mkuu?
Hii ni Nuru mpya kwa CHADEMA
 
Soma pia:
Mimi binafsi kama mtanzania nimefurahi sana, kwanza kwa kuwa huwa sipendi unafiki kabisa na siwezi hata kuuigiza kama ambavyo viongozi wapya tunawaamini hawatatufanyia unafiki wa kisiasa ambao ndio umetamaraki katika nchi hii. Imani yetu kwao si kwa kuwa tulimchukia mbowe na timu yake bali kwa kuwa wao viongozi wapya wameyaishi yale waliyoyaamini toka tunawafahamu kisiasa.

Pili uchaguzi huu unafurahisha kwani umewaonesha wazi wanaccm kuwa kuna kitu hakiko sawa katika siasa zao zinazoliongoza taifa hili pasipo ridhaa halisi ya wananchi. Wanalo la kujifunza ama waendelee kushupaza shingo na kutufanyia sanaa na wasanii wao hadi yaliyomkuta mbowe yawakute.

Pole kwa Mh. Mbowe, kazi ameifanya ya kutosha hadi tu pale kina Boni Yai na Yeriko walipompotosha na kutufanya tuyaone makengeza yake ambayo katika miaka yote 21 hatukuwahi kuyaona kwa kuwa tulimpenda.
 
Hivi vyama vilivyo sajiliwa siku Umma ukivitaka nakwambia Siasa itapendeza sana
 
Mama abduli ajiandae psychological
Kama uchaguzi ukiwa huru na wa haki. Bitozo anashika nafasi ya nne. Tundu Lissu nafasi ya kwanza kwa 95%. Bitozo ataambulia 1%. Watu wengi mno wana maisha magumu sana, vijana wengi mno hawana ajira miaka inakwenda hawana maisha kabisa.

Ila kama kawaida yao, wataiba kura watashinda.
 
Mambo Siyo mepesi, ila huo ni mwanzo mzuri unaoleta matumaini,

Mimi nashauri CHADEMA waelekeze nguvu kubwa kusajili wanachama wapya maana ni wazi wanachama wengi watahamia CHADEMA na hata wale ambao hawakuwa na Vyama wanaenda kushawishika kujiunga , hivyo Chama kijipange sana kuuza Kadi , hasa zile Kadi za ki electronic Ili kukiwezesha Chama kuwa na uwezo wa kifedha kwa ajili ya kujiendesha , Chama kikishakuwa na uchumi mzuri ni rahisi kufika shinani ambako haswa ndipo ulipo msingi wa Chama chochote cha kisiasa

..utawazuiaje Polisi na watendaji wa serikali kuengua wagombea wa upinzani, na kufanya hujuma dhidi ya wapinzani?
 
Kama uchaguzi ukiwa huru na wa haki. Bitozo anashika nafasi ya nne. Tundu Lissu nafasi ya kwanza kwa 95%. Bitozo ataambulia 1%. Watu wengi mno wana maisha magumu sana, vijana wengi mno hawana ajira miaka inakwenda hawana maisha kabisa.

Ila kama kawaida yao, wataiba kura watashinda.
Sina hamu na hii serikali ya bi tozo a.k.a chura kiziwi

Sijapiga kura mda mrefu ila Mhe. Lissu akigombea lazima nikampigie kura no matter what!
 
Back
Top Bottom