Ushindi wa Mayweather utata

Hawezi kukubali marudiano,hili lenyewe kasumbua sana.
Sijui alikua hataki/anaogopa/anadharau? Hata cjui?

Mwisho wa siku chai imeungwa chumvi,na watu wamekubali kuinywa.watafanyaje sasa!

Wajanja washapiga pesa! Hapo hakuna cha pambano la karne wala nini! Kama kweli Hilo lilikuwa pambano la karne, basi mchezo wa ngumi utakuwa umefilisika sana! Kwa kifupi dunia imepigwa changa la macho! huu ni utapeli! Pambano halikustahili gharama na sifa hizo! Dunia imeshuhudia wavulana wa kilo 66 wakiruka ruka na kudonoana na hakuna kukalishana chini halafu tukubali kuwa ni pambano la karne! Hili lilikuwa ni dili la karne! Nimependa ulivyoiweka, chai imeungwa chumvi! Ni kweli mabondia ni wazuri lakini si Kivile!
 

Pac ni mtoto
 
hahahaha kuna lingine la kitambo jamaa huyu mei weza kashinda kwa majority decision



Ni Sawa na ushindi wa siti mtemvu


hashimu lundega decision
 

Acha kupotosha watu, hakuna sheria kama hiyo. Kwenye ngumi huwa kuna majaji watatu, ukisikia bondia kashinda kwa "unanimous decision" (kama Mayweather jana)maana yake ni kuwa majaji wote watatu wamempa ushindi aliyeshinda. Ikitokea mmoja kati ya majaji akampa ushindi bondia mwingine na wawili wakampa bondia mwingine yule aliyepewa ushindi na majaji wawili anakuwa ameshinda kwa "split decision".

Haiwezekani majaji wawili wampe ushindi bondia mmoja halafu yule ambaye amepewa na jaji moja awe ndio mshindi, hakuna kitu kama hicho.
 

Mkuu uko sahihi kabisa, Mourinho na Mayweather wako sawa kabisa. Kwao haijalishi wanachezaje, cha msingi ni kushinda tu. Mbinu za Mourinho zinajulikana kama "anti football", kwa hiyo Mayweather naye ni "anti boxing".
 
Sasa ndio umemwaga utorojo gani huu. Si umejaza server za jf bure wewe?

Nilijua kuna watu kama wewe ambao hamtanielewa; mtaduwaa tu! hizo ni hard facts kuhusu ushindi wa floyd Mayweather; amesinda fair and square! server ya Jf is there for that purpose; solid minds zinazojua kitu na kutafiti kitu zibadilishane mawazo na kuweka records straight; sio server ijae opinions ambazo ni "emotion na infatuation" based! Bs
 
Yuko live on ESPN right now. Keshaanza visingizio eti aliumia bega kabla ya fight!
Anakiri kuwa amepigwa kihalali.
Mfilipino kazi yake ni kuchoma viazi Na sio boxing
Mtakula maneno yenu leo. Mayweather ndio dume


Wow! Hapo kwenye red sidhani kama Oscar De La Hoya, Ricky Hatton, Antonio Margarito, Miguel Cotto, Timothy Bradley, Brandon Rios na wengine watakubaliana na wewe.
 

Mkuu ulitegemea fantastic punches kutoka kwa nani, Mayweather?? Either ulikuwa naive au ulikuwa hujawahi kumuona akipigana. Watu wengi walikuwa hawajawahi kuwaona mabondia hawa kabla ya hili pambano. Promo kubwa iliyofanywa na kuliita kuwa "pambano la karne" ndiyo ikasababisha watu watake kuliona lakini wale wapenzi wa ngumi ambao wanafuatilia na wameshawahi kumuona Mayweather akipigana walijua jinsi atakavyopigana.
 

Ukumbi upo Las Vegas, Judge 1 na 3 wanatokea Nevada, Judge 2 anatokea Conectcut. Wamarekani mashuhuri wote walikuwepo pale. Unategemea nini. MAY alijihami ili asipigwe KO tu maana hiyo ndio wangeshindwa kutudanganya.
 
Hii ni kutokana na uchambuzi wa Idd Seif na kwamba wanatumia mtambo ambao unasoma points na katika kutoa uamuzi kulikuwa na sehemu ambayo ina rangi ya blue na nyekundu. Kwahiyo basi sehemu ya Manny ikasomwa kwa May na vice versa. Waligundua tayari mshindi ametangazwa. Manny alipoulizwa akasema basi yameisha yeye anamuachia Mungu.

Source: BBC Dira ya Dunia
 
Kwa kifupi pac alishinda hilo halina ubishi
 
Kweli hii saa mbovu. Idi Seif kaelezea kwa kiswahili na bado umeshindwa kumuelewa. Je angeelezea kwa kinngereza si ndio ungepotea kabisa na uswahili wako huo.
 
Boxng is business lyk other busines nani alishinda does'nt matter.what matter? Who is marktble for future.
Kati ya huyo mflpino na mywether nani ana generate income klko mwngne
 
Nimeskia taarifa ya bbc michezo saa tatu usiku,imenidikitisha sana kuwa majaji walichanganya na kumpa point kimakosa weather et sababu ya rangi za bukta
 
Kweli hii saa mbovu. Idi Seif kaelezea kwa kiswahili na bado umeshindwa kumuelewa. Je angeelezea kwa kinngereza si ndio ungepotea kabisa na uswahili wako huo.

Lakini kumbuka na wewe ni ARV. Wengine wanakubali inamaana nao hawaelewi kiswahili? Labda huelewi wewe.
 

Natamani team Manny wasome hapa na kuelewa badala ya kupiga tu mikelele isiyo na maana, Jamaa kashinda kwa kujua mbinu za ushindi na sio mashabiki wanataka nini, na hiki ndio kinawashinda wengi.
 

Watu wanaangalia ngumi nyingi za Manny zilizokuwa zinatua kwenye mikono ya Maywether ambazo hazina point, hawaangalii zile donoa donoa zake usoni za mkono wa kushoto zilizo kuwa zinampata Manny hapo ndio huwa Maywether huwa anachukulia ushindi.
 
Mmmmmmhhhhh kashachukua mpunga sasa hivi anauguza mapengo mwenzenu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…