Ushindi wa Uhuru Kenyatta ni ushindi wa CHADEMA

Ushindi wa Uhuru Kenyatta ni ushindi wa CHADEMA

Paul Alex

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2012
Posts
4,351
Reaction score
9,838
CCM wataongea weee ila Unaweza kuwajibu hamadi kibindoni.
Unaweza pia kuwajibu Kimfaacho mtu chake!

Mimi nasema Hongera Uhuru , hongera CHADEMA.

Kwanini hongera CHADEMA?

Ni upuuzi, Actually ni wapuuzi tu wanaoweza kuubeza ushindi wa kimkakati wa CHADEMA kuwa na rafiki anayeongoza uchumi mkubwa kuliko yote Africa Mashariki.

Kenya ni kubwa karibu kila nyanja Africa Mashariki;
☞Ndio wenye uchumi mkubwa kuliko yote Africa mashariki .
☞Wana jeshi kubwa na la kisasa.
☞Wana kambi pekee ya Special Forces ya USA- Camp Simba hapa Africa mashariki.
☞Ni demokrasia iliyokomaa ukilinganisha na zote hapa Africa Mashariki.

Kuna msemo usemao, Ukitaka kumfahamu mtu basi waangalie marafiki zake.
Ukitaka kumfahamu Magufuli na CCM basi muangalie;
☞Paul Kagame
☞Yoweri Museveni
☞Nkurunzinza

Na Ukitaka kumfahamu Lowassa na CHADEMA basi muangalie Uhuru Kenyatta!

Leo nimejikumbushia kidogo miaka nikiwa Seminari na nikamkumbuka Yesu na familia ya kina Martha na Lazaro ambayo Yesu aliipenda sana. Unaweza kusema familia rafiki kwa Yesu.

Basi wakati Lazaro ameugua sana, Martha dadaye alituma ujumbe kwa Yesu kuwa rafiki yako anaumwa sana, hawezi tena.
Nakumbuka Yesu alimjibu kuwa, 'Ugonjwa huu sio kwaajili ya Mauti ila kwaajili ya utukufu wa Mungu'.

Naomba kwa leo niwaache na neno hilo hapo juu ndugu zangu!
 
ni kweli mkuu.....

upande mmoja Odinga alikuwa anatumia jina la Magufuli wazi wazi kabisa kwenye kampeni. sema tu Magufuli asingeweza kumpigia debe Odinga kwa vile taratibu za kidiplomasia ya kimataifa haziruhusu.

upande wa pili, Lowasa alikuwa anampigia kampeni ya wazi kabisa Uhuru. Uhuru asingeweza ku-appreciate in public hii gesture ya Lowasa kwa sababu hizo hizo.
 
Siasa haina uadui wala rafiki wa kudumu. Ila huyu wa kwetu hajui hilo na amekuwa mtu wa visasi

Sasa tusubiri moto ila watakaoumia ni sisi. Wanasema jambo linapotokea wenye akili hujipanga ila wenye uelewa mdogo wanakurupuka.
 
Abadan Kenya ,Afrika kusini na Tanzania upinzani watashinda kwa miaka 100 ijao

Ushindi wa Uhuru hauna effects yeyote kwa Chadema na kushindwa kwa Raila hauna effects yeyote kwa Magu ,

Ila mtambue wapinzani nchini Kenya ,South na Tz Abadan hawawezi kushinda kila chaguzi lowassa ,Raila wataishia kujikomba komba tu ila hawatoshinda kamwe kwangu mm Raila na lowassa wanapoteza muda tu
 
Tusije Kuwa Na Chati Na Watu Waliotoroka Milembe Oooooh!
 
Hii ni aibu. Ushindi wa Kenyatta leo ni ushindi wa Chadema, could CDM go lower than this?

Kama hiyo inawafariji endeleeni kufarijiana. If anything cha kujifunza toka kwenye uchaguzi wa KE ni kuwa wananchi wanataka maendeleo sio maneno, hiyo ingepaswa kuwaonyesha Magufuli atashinda 2020 sababu anasukuma maendeleo Kama afanyavyo Kenyatta na si maneno. Na mkishindwa mchukue big L mtulie kama Odinga

TZ haijawahi kuingilia uchaguzi wa nchi yeyote Bali ni rafiki wa nchi zote. Kuna tofauti. Odinga kutumia jina la Magufuli kwenye kampeni zake haimaanishi kwamba TZ Kama nchi inamsapoti Odinga.

Hongereni CDM kwa kuendelea kushika dola KE ila ya TZ mtaendelea kuisikia kwenye bomba.
 
Hahah Kenyata unahisi 2020 atakua na mchango gani kwa CHADEMA kwenye uchaguzi?
 
Hii ni aibu. Ushindi wa Kenyatta leo ni ushindi wa Chadema, could CDM go lower than this?

Kama hiyo inawariji endeleeni kufarijiana. If anything cha kujifunza toka kwenye uchaguzi wa KE ni kuwa wananchi wanataka maendeleo sio maneno, hiyo ingepaswa kuwaonyesha Magufuli atashinda 2020 sababu anasukuma maendeleo Kama afanyavyo Kenyatta na si maneno.

TZ haijawahi kuingilia uchaguzi wa nchi yeyote Bali ni rafiki wa nchi zote. Kuna tofauti. Odinga kutumia jina la Magufuli kwenye kampeni zake haimaanishi kwamba TZ Kama nchi inamsapoti Odinga. Kibaya zaidi leo TEF na Makonda wameamua yaishe, basi ndio wanachanganyikiwa kabisaa.

Hongereni CDM kwa kuendelea kushika dola KE ila ya TZ mtaendelea kuisikia kwenye bomba.
Hawa jamaa sasa wameamua kula ugali kwa kulumangiza na harufu ya mchuzi. Na hivi leo TEF na Makonda wameamua yaishe basi ndio wamechanganyikwa kabisaa.
 
Ivi we ni mpinzani afu unasapoti chama tawala kishinde, ukitegemea kilete effect kwenu!

Nilidhani kilipaswa kushinda chama pinzani ili tuje tutoe mfano wa kenya, wakati wa kampeni.

Nakumbuka hata mahakama ya kadhi inapodaiwa, kuna mifano ya nchi jirani hutolewa ili kujenga hoja, sasa cha ajabu, Chadema wao wanategemea eti hii technic ita wa-boost.
 
Hii ni aibu. Ushindi wa Kenyatta leo ni ushindi wa Chadema, could CDM go lower than this?

Kama hiyo inawariji endeleeni kufarijiana. If anything cha kujifunza toka kwenye uchaguzi wa KE ni kuwa wananchi wanataka maendeleo sio maneno, hiyo ingepaswa kuwaonyesha Magufuli atashinda 2020 sababu anasukuma maendeleo Kama afanyavyo Kenyatta na si maneno.

TZ haijawahi kuingilia uchaguzi wa nchi yeyote Bali ni rafiki wa nchi zote. Kuna tofauti. Odinga kutumia jina la Magufuli kwenye kampeni zake haimaanishi kwamba TZ Kama nchi inamsapoti Odinga.

Hongereni CDM kwa kuendelea kushika dola KE ila ya TZ mtaendelea kuisikia kwenye bomba.
Kumbe msiojua siasa tanzania mko wengi hivii???!!!
 
Abadan Kenya ,Afrika kusini na Tanzania upinzani watashinda kwa miaka 100 ijao

Ushindi wa Uhuru hauna effects yeyote kwa Chadema na kushindwa kwa Raila hauna effects yeyote kwa Magu ,

Ila mtambue wapinzani nchini Kenya ,South na Tz Abadan hawawezi kushinda kila chaguzi lowassa ,Raila wataishia kujikomba komba tu ila hawatoshinda kamwe kwangu mm Raila na lowassa wanapoteza muda tu

Tafadhali mkuu kenya haipo kwenye msafara huu. chama tawala kimeshakufa siku nyingi bado mazishi tu. Kenyatta siyo wa chama tawala cha enzi za ukombozi.
 
Ivi we ni mpinzani afu unasapoti chama tawala kishinde, ukitegemea kilete effect kwenu!

Nilidhani kilipaswa kushinda chama pinzani ili tuje tutoe mfano wa kenya, wakati wa kampeni.

Nakumbuka hata mahakama ya kadhi inapodaiwa, kuna mifano ya nchi jirani hutolewa ili kujenga hoja, sasa cha ajabu, Chadema wao wanategemea eti hii technic ita wa-boost.
Uko nyuma sana !
 
Naomba kama ulifuatilia uchaguzi wa Marekani unikumbushe jinsi Putin alivyo tip scale ya uchaguzi towards Trump?
 
umeharibu kuingiza mambo ya biblia ambayo hayajawahi kutokea sababu biblia ni uzushi wa wazungu
 
Uko nyuma sana !
We jidanganye chadema walibadili msimamo wa wakenya, chadema waliangalia upande wenye ganda la ndizi.
Au unadhani mange nae kachangia ushindi! mwambie aweke account yake ya bank basi.
 
Back
Top Bottom