Ushirikiano kwenye sekta ya kilimo kati ya China na Afrika, unaweza kuinua maisha ya wakulima wengi wa Afrika

Ushirikiano kwenye sekta ya kilimo kati ya China na Afrika, unaweza kuinua maisha ya wakulima wengi wa Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
rBABDGAXWnCAVlFZAAAAAAAAAAA564.400x281.jpg

Ile zama ya vyama na serikali kuwa wadau pekee wa uhusiano kati ya China na Afrika sasa imepita. Mageuzi makubwa ya kiuchumi yamefanyika nchini China na maendeleo makubwa yamepatikana, hali hii imefanya serikali isiwe mdau pekee wa ushirikiano. Tangu China ianzishe ushirikiano wa kimkakati wa pande zote na nchi za Afrika, tunaona wadau wa ushirikiano wameongezeka na kuhusisha watu binafsi na makampuni binafsi.

Tukiangalia maana halisi ya maneno “ushirikiano wa kimkakati wa pande zote”, kwa ufupi maana yake ni kuwa uhusiano kati ya China na nchi za Afrika sasa unagusa maeneo yote, na mdau yoyote kutoka pande hizi mbili anaweza kuwa sehemu ya ushirikiano, na bidhaa yoyote inaweza kuwa kitu cha ushirikiano. Hali hii imefanya wigo wa ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika kuwa mpana zaidi, na kuhusisha watu wa kawaida kabisa, tofauti na zamani wakati serikali na makampuni ya serikali ndio walikuwa wadau wakubwa.

Tukiangalia sekta ya kilimo, tunaweza kuona kuwa kwa sasa ndio sekta inayoajiri au inagusa watu wengi zaidi barani Afrika, na tayari kumekuwa na ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika kwenye eneo hilo. Lakini ikilinganishwa na maeneo mengine kama ujenzi wa miundo mbinu, ambayo wadau wakubwa ni serikali za nchi za Afrika na makampuni ya ujenzi ya China, tunaweza kuona kuwa ushirikiano kwenye sekta ya kilimo bado uko nyuma sana ikilinganishwa na ujenzi wa miundo mbinu.

Uzuri ni kwamba, licha ya kukosekana wadau wenye nguvu wa ushirikiano kwenye sekta ya kilimo, kilichopo sasa ni kuwa kuna wadau wengi sana katika kila upande, na kufanya eneo hili liwe na mustakbali mzuri sana kwa maendeleo ya moja kwa moja kwa nchi za Afrika.

Kwa sasa tunaweza kuona wachina katika miji mikubwa wanakunywa maelfu ya tani za kahawa kila siku, wanakula maparachichi, korosho, wanatumia kwa wingi bidhaa za kilimo kama maharage, ufuta, na hata mvinyo kutoka Afrika. Ikumbukwe kuwa kuna orodha ndefu sana ya mazao ya kilimo yanayoruhusiwa kuingia kwenye soko la China bila ushuru wa forodha, na kumekuwa na mfululizo wa makubaliano yanayosainiwa kati ya serikali ya China na nchi za Afrika kuingiza mazao na bidhaa za kilimo kwenye soko la China. Hali hii ni neema kubwa kwa wakulima wa nchi za Afrika.

Lakini mbali na wachina kutumia bidhaa za kilimo kutoka Afrika kwa chakula, tunakuwa kukumbuka kuwa viwanda vya China ambavyo sasa vimekuwa na uwezo mkubwa wa uzalishaji, pia ni mtumiaji mkubwa wa malighafi zinazotokana na sekta ya kilimo. Wakulima wa mazao ya biashara kama mkonge, muhogo, mawese, nk bila shaka wanaweza kuwa na soko la uhakika nchini China.

Kwa sasa tatizo kubwa lililopo kwenye eneo hili, ni changamoto zilizopo kwa wakulima wa Afrika kukidhi mahitaji. Si mara moja au mara mbili, makampuni madogo madogo ya China yanapoagiza bidhaa fulani ya kilimo kutoka nchi za Afrika, kinachoonekana ni kuwa wafanyabiashara au walizalishaji wanashindwa kuwa na mzigo wa kutosha kukidhi oda. Mara nyingi kunapokuwa na oda, wazalishaji au wafanyabiashara wanatakiwa kuthibitisha kuwa wanaweza kuleta bidhaa kwa mwaka mzima na kwa kiasi kinachotakiwa, bahati mbaya ni kuwa wengi wanashindwa kukidhi matakwa haya, na wachache wanaoweza wananufaika sana.

Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na mazungumzo kuhusu kuhimiza ushirikiano kwenye kujenga uwezo wa uzalishaji wa bidhaa za kilimo na bidhaa nyingine barani Afrika, ili kuweza kukidhi mahitaji ya soko la China. Kuna dalili za maendeleo kwenye eneo hilo, mifano ni pamoja na kuwepo kwa watalaam wa China wanaotoa elimu kwa wakulima kusaidia kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo kwa hekta. Hali hii ikienezwa wakulima wengi wa Afrika watanufaika.
 
Ile zama ya vyama na serikali kuwa wadau pekee wa uhusiano kati ya China na Afrika sasa imepita. Mageuzi makubwa ya kiuchumi yamefanyika nchini China na maendeleo makubwa yamepatikana, hali hii imefanya serikali isiwe mdau pekee wa ushirikiano. Tangu China ianzishe ushirikiano wa kimkakati wa pande zote na nchi za Afrika, tunaona wadau wa ushirikiano wameongezeka na kuhusisha watu binafsi na makampuni binafsi
Enzi zile ziara za mafunzo zilikuwa kichekesho, badala ya serikali kuwapeleka wakulima kujifunza walipeleka wanasiasa waliporejea nchini waliishia kusimulia uzuri wa mitaa ya huko ughaibuni
 
Back
Top Bottom