Likiwa jukwaa la ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea, BRICS inabeba jukumu la kutatua changamoto ya umaskini inayokabili nchi zinazoendelea na kutimiza maendeleo endelevu. Kwa kuwa Afrika ni bara lenye nchi zinazoendelea nyingi zaidi, ushirikiano wa BRICS umeiletea fursa mpya.
Afrika Kusini ni nchi mwanachama wa kwanza wa upanuzi wa BRICS, na tangu kujiunga na BRICS, nchi hiyo imeimarisha ushirikiano na nchi zilizoibukia kiuchumi duniani, haswa China ambayo ni nchi ya pili kwa ukubwa wa uchumi duniani, na kuhimiza maendeleo ya uchumi. Baada ya China kutoa pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, Afrika Kusini imezidisha ushirikiano na China katika biashara na uwekezaji kupitia utaratibu wa BRICS, na kuhimiza ujenzi wa miundombinu, pamoja na maendeleo ya sekta za uzalishaji za viwanda, zikiwemo vifaa vya nyumbani, magari, vifaa vya ujenzi, na vifaa vya nishati ya jua.
Ushirikiano wa BRICS si kama tu umehimiza maendeleo ya Afrika Kusini, bali pia umetoa fursa pana ya ushirikiano kwa nchi nyingine za Afrika. Katika miaka ya hivi karibuni, nchi za Afrika zimeshiriki kwa hatua madhubuti katika utaratibu wa ushirikiano wa BRICS kupitia tawi la Benki Mpya ya Maendeleo ya BRICS barani Afrika. Maendeleo endelevu ni msingi wa mikakati ya maendeleo ya kikanda ya Afrika kama vile Ajendaya 2063 ya Umoja wa Afrika, na Ajenda ya Pamoja ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika. Kuanzishwa kwa tawi la Benki Mpya ya Maendeleo ya BRICS barani Afrika kunamaanisha kuwa huduma za benki hiyo zinapatikana kwa nchi za Afrika. Hadi sasa, nchi nyingine za Afrika ikiwemo Misri zimetangaza kujiunga na Benki hiyo, na nchi nyingi zaidi za Afrika zitapata mikopo kutoka Benki hiyo katika siku zijazo. Wakati wa kutoa huduma za kifedha, tawi la Benki Mpya ya Maendeleo ya BRICS barani Afrika pia ni njia ya nchi nyingine ya Afrika, na mashirika ya kikanda ya Afrika kushiriki katika ushirikiano wa BRICS.
Licha ya uchumi, uratibu wa sera pia ni njia muhimu kwa nchi za Afrika kushiriki na kufaidika na mfumo wa “BRICS+”. Katika miaka ya hivi karibuni, nchi za Afrika zimebadilishana maoni na kuratibu misimamo na nchi za BRICS katika mikutano ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa kuhusu masuala muhimu mbalimbali yakiwemo mabadiliko ya hali ya hewa, mazungumzo ya WTO, na kutoa sauti ya pamoja ya nchi zinazoendelea duniani.