Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 126
- 215
Mkutano wa mwaka 2024 wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utafunguliwa hivi karibuni hapa Beijing. “Ripoti ya Mwaka 2024 ya Uwekezaji wa Kampuni za China barani Afrika” imetolewa Ijumaa wiki iliyopita hapa Beijing. Katika miaka ya hivi karibuni, uwekezaji wa China barani Afrika umeongezeka kwa mfululizo, na mafanikio ya ushirikiano wa uwekezaji kati ya pande hizo mbili yamezidi kudhihirika.
Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2022, uwekezaji wa moja kwa moja wa China barani Afrika umezidi dola bilioni 47 za Kimarekani, na zaidi ya kampuni 3,000 za China zimewekeza na kuanzisha biashara barani Afrika.
Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, uwekezaji wa moja kwa moja wa China barani Afrika ulizidi dola bilioni 1.82 za Kimarekani, ambalo ni ongezeko la asilimia 4.4 ikilinganishwa na mwaka jana kipindi kama hiki.
Kwa mujibu wa Mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika Dakar, mji mkuu wa Senegal, itakapofika mwaka 2035, uwekezaji wa moja kwa moja wa China barani Afrika utafikia dola bilioni 90 za Kimarekani, na kutarajiwa kushika nafasi ya kwanza duniani.
Afrika ni bara lenye nchi nyingi zaidi zinazoendelea duniani, linahitaji uwekezaji wa kigeni ili kuboresha miundombinu iliyo nyuma, kuinua kiwango cha ukuaji wa viwanda, kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa, kutokomeza umaskini, na kuhakikisha usalama wa chakula.
Ikiwa mwenzi wa kuaminika wa Afrika, China imefanya uwekezaji mkubwa barani Afrika. Kwa zaidi ya muongo mmoja uliopita, China imewekeza na kujenga miradi mikubwa barani Afrika, ikiwemo zaidi ya kilomita 6,000 za reli, zaidi ya kilomita 6,000 za barabara, karibu bandari 20, zaidi ya vituo 80 vya umeme, maeneo 25 ya kiviwanda, na zaidi ya vituo 500 vya majaribio ya kilimo.
Zaidi ya hayo, miradi mingine ya kawaida ya uwekezaji kati ya China na Afrika haihesabiki, ambayo ni muhimu sana kwa maendeleo endelevu ya uchumi wa nchi za Afrika. Mbali na fedha, China pia inatoa teknolojia ya juu kwa Afrika. Rasilimali hizi zimehimiza sana ukuaji wa uchumi wa nchi za Afrika. Aidha, uwekezaji wa China barani Afrika pia umeleta nafasi nyingi za ajira kwa watu wa Afrika.
Ushirikiano wa uwekezaji kati ya China na Afrika pia una umuhimu mkubwa kwa China, kwani kwa kupitia ushirikiano huo, China inaweza kuhamisha uwezo wa uzalishaji ambao ni mkubwa zaidi kuliko mahitaji ya ndani, kuboresha mnyororo wa uzalishaji duniani, kuhakikisha usalama wa maliasili, na kuendeleza kampuni zake.