Ushirikina unaongezeka kwa kasi kubwa duniani

Ushirikina unaongezeka kwa kasi kubwa duniani

Mafanikio ya huu ulimwengu ni ushirikina uliokubuhu. Ili uamini, nabii Issa alipopelekwa mlimani na shetani alionyeshwa ufalme na utajiri wa dunia kama mali ya shetani. Ukitaka utajiri ni lazima upitie kwake! Huo ndio ushirikina.
 
Mafanikio ya huu ulimwengu ni ushirikina uliokubuhu. Ili uamini, nabii Issa alipopelekwa mlimani na shetani alionyeshwa ufalme na utajiri wa dunia kama mali ya shetani. Ukitaka utajiri ni lazima upitie kwake! Huo ndio ushirikina.
Wengi hili hawalifahamu na hata ukiwaambia habari za mkuu wa anga wanaweza kukubishia mpaka basi
 
Usiku huu tuna kazi moja tuu kuhakikisha uto kesho wanalala chali.. Cha ajabu nao huko wanafanya yao..
 
2 Kor 5:17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
Aaamen [emoji1545][emoji1545][emoji1545][emoji1534]
 
Changamoto za maisha zinazidi kuikumba dunia. Kisiki cha ajira ni mfupa uliowashinda hata mataifa yaliyoendelea sana kiuchumi
Shortcut nyingi za madawa, silaha, vikundi vya kigaidi na umafia wa namna zote vimedhibitiwa kwa kiwango kikubwa. Ni kama sasa dili zile kubwa kubwa zimetoweka na hata kama zipo kwasasa zinahitaji akili kubwa na mtaji mkubwa na watu wachache kuzitekeleza
Huko kwa wenzetu sasa ni mwendo wa makafara kupitia vyama vya giza vilivyobatizwa majina ya freemason, satanism nk

Huku kwetu mmh, hali ndio mbaya kabisa. Walio nacho kidogo wanawindwa na kila mtu
Wanawindwa na vibaka
Wanawindwa na wezi
Wanawindwa na tozo
Wanawindwa na chumaulete
Wanawindwa na wachawi ama kuwaharibia ama kuwafanya watumwa wao kwenye kipato. Kazi unafanya wewe mapato wanachukua wengine

Jaribu kuangalia trend ya watu wanaoanguka kibiashara kwa sasa
Jaribu kuangalia trend ya watu ambao biashara zao zinavyozorota
Angalia watu wanavyofilisika na kuharibu maisha yao kutokana na ulevi ama kufilisiwa na mabenki kutokana na mikopo

Tunaweza kutumia korona kama kigezo cha haya yote lakini nyuma yake kuna msingi mkubwa wa ushirikina unafanya kazi. Imefika mahali huko mtaani hata ukionekana na nguo mpya ni shida. Utawangiwa na kuchawiwa usiku mzima.

Kwa bahati mbaya kabisa hao waganga tunaowaendea kutafuta suluhu ndio hao hao wameendewa na wabaya wetu kutuumiza
Yaani ni sawa na double taxation kwenye tozo na miamala. Ukituma unakatwa, akipokea na kutoa anakatwa! Mganga anachukua kwako kumbe kachukua pia kwa mbaya wako.

Tunaibiwa sana kwakweli halafu tunaumizana sana kwakweli, hatutaki kuona wengine wanapata na kujikwamua kimaisha. Tunasema mioyoni mwetu. BORA TUKOSE WOTE! roho ya kwanini hii! Yaani kati yetu kuna ambao wanaona kushindwa kwao kumesababishwa na wewe. Kukosa kwao wewe ndio sababu.

Changamoto za maisha zinatufanya tuwe na roho mbaya sana tunateketea na kumalizana wenyewe. Ukiniuliza suhusu ninini nitakwambia hata mimi sijui[emoji31][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827] ila tu watu wanarogana sana sasa hivi
Mshana, ulishafatwa na watu wanataka uwasaidie kwenye hizo ishu??
 
Back
Top Bottom