Chukwu emeka
JF-Expert Member
- Jan 12, 2018
- 24,314
- 38,919
Nimepita hapa Uwanja wa Taifa kuna kundi la watu linazozana kumbe ni Makomandoo wa Yanga na Simba wamekuja kulinda Uwanja ili kuzuia vitendo vya kishirikina,hizi timu kwa Tanzania imekuwa zaidi ya imani za dini kiasi kwamba kila upande unatumia nguvu nyingi ambazo wangewekeza kwenye mechi za kimataifa timu hizi zingekuwa zinafika hadi fainali.
Ukizaliwa Tz lazima uwe upande mmoja kama si Yanga basi utakuwa Simba mtu akikwambia hana timu kati ya hizi anakudanganya.Basi acha tuendelee kuziabudu tu na porojo za kina Hajji Manara na Dismas Ten.