Ushirikishwaji wa Wananchi katika mipango ya maendeleo ndio chachu ya maendeleo

Ushirikishwaji wa Wananchi katika mipango ya maendeleo ndio chachu ya maendeleo

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Inaelezwa kuwa utendaji wa viongozi wa vijiji umekuwa ukikabiliwa na changamoto mbalimbali kutokana na viongozi wengi kutokuwa tayari kushirikisha wananchi katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali. Hali hiyo inadaiwa kusababisha kukosekana kwa uwazi katika masuala la mapato na matumizi na utekelezaji wa shughuli za maendeleo.

Dhana ya ushiriki na ushirikishwaji ni pana kwani inahusisha wananchi katika upangaji na utekelezaji wa maendeleo na kushiriki kuibua miradi na mikakati ya utekelezaji katika kijiji au mtaa. Wananchi wafahamu kwamba maendeleo hayaji kama miujiza

Mara nyingi viongozi wa vijiji wakichaguliwa kwa kipindi cha miaka mitano hakuna mafunzo yanayofanyika. Hali hiyo hufanya viongozi wengi kuongoza kwa kubahatisha na hivyo husababisha migogoro mingi vijijini.

Baadhi ya wanakijiji wamekuwa wakisusia mikutano na vikao vya Serikali za vijiji vyao kutokana na kutopewa taarifa za mapato na matumizi ya kijiji. Hilo limesababisha baadhi ya wanakijiji kuwakataa viongozi wao,

Kujengwa sekondari nyingi za Kata kumesababisha vijana wengi wanaomaliza sekondari kutaka kuona uwazi na ukweli hivyoushirikishwaji ni msingi mkubwa sana katika kuimarisha utawala bora vijijini kwani itafanya hata mapato na matumizi yaweze kusomwa mbele ya wananchi vijijini na hata kufanya demokrasia iimarike katika maeneo hayo.

Serikali za vijiji ndiyo msingi wa serikali zote Tanzania, msingi ukiwa mbovu na utawala utakuwa mbovu. “Viongozi wa vijiji ndio serikali, msingi ukiwa mbovu hakuna nyumba na ninyi mkisambaratika hakuna serikali lakini mkiwa imara mipango yote inakwenda vizuri

Viongozi wanatakiwa kwenda kuimarisha utawala bora, demokrasia na ushiriki wa wananchi katika uendeshaji wa serikali zao na kuhakikisha suala la mapato na matumizi linakwenda kwa uwazi na ukweli kwani kificho kidogo kinaweza kuleta tatizo. Viongozi pia wanapaswa kutambua umuhimu wa ushiriki wa kinamama katika serikali za vijiji unakuwa mkubwa.

Je, wewe unashiriki katika mipango ya maendeleo ya eneo unaloishi?
 
Back
Top Bottom