SoC02 Ushirikishwaji wa Wananchi katika utekelezaji wa maamuzi ni nguzo ya Utawala Bora

SoC02 Ushirikishwaji wa Wananchi katika utekelezaji wa maamuzi ni nguzo ya Utawala Bora

Stories of Change - 2022 Competition

Samwel John banzi

New Member
Joined
Jul 31, 2022
Posts
1
Reaction score
2
UTAWALA BORA huusisha ushirikishwaji wa wananchi wote walioko ndani ya jamii au nchi kiujumla juu ya utekelezaji wa maamuzi pendekezwa na viongozi Kwa ajili ya maendeleo ya wananchi ndani ya jamii na taifa kwa ujumla kwa kuzingatia haki na usawa wa kila mwananchi aliye ndani ya jamii husika katika ngazi za halmashauri,

Ushirikishwaji wa wananchi katika utekelezaji wa maamuzi Huwa chachu ya maendeleo katika taifa na jamii Kwa kuzingatia Demokrasia, Haki na usawa bila kujali itikadi za wananchi

Nguvu kubwa ya maendeleo ya taifa hutoka Kwa wananchi wenyewe wakisaidiwa na Viongozi waliowachagua kwa hiari zao wenyewe bila ya kusukumwa au kushurutishwa na mtu yeyote

UTAWALA BORA huzingatia zaidi ushirikishwaji wa wananchi katika mikutano mbalimbali ya kiserikali katika ngazi mbalimbali ikiwemo halmashauri ya jamii husika

UTAWALA BORA huzingatia Demokrasia uhuru wa wananchi katika kuwachagua viongozi wanaowalenda Kwa hiari zao Kwa kufanya uchaguzi wa viongozi

UTAWALA BORA pia huzingatia Haki na usawa katika utekelezaji wa majukumu na viongozi huchaguliwa na wananchi kwa lengo la kuwatumikia wananchi na kutimiza majukumu yao kwa kuzingatia haki na usawa wa kila mwananchi ndani ya jamii na taifa kwa ujumla

Viongozi wanatakiwa kutimiza majukumu yao kwa kufuata Utawala wa Sheria uliowekwa nchini kinyume na hapo hatua za kisheria zitafuatwa kwani hakuna UTAWALA BORA huzingatia na kufuata UTAWALA wa Sheria ya nchi.

Mwisho kabisa misingi ya UTAWALA BORA hujitoa zaidi katika kupambana na kuzuia rushwa kwenye jamii na taifa,kwani rushwa ni adui wa haki na huleta dosari nyingi na kukwamisha utekelezaji wa maendeleo katika jamii Kwa kutokuzingatia haki na usawa wa Kila mwananchi nchini,

Hivyo basi UTAWALA BORA ushirikishe wananchi katika utekelezaji wa maamuzi pendekezwa na viongozi
 
Upvote 2
Hongera kwa makala nzuri.
Unaweza kupitia andiko langu pia ili kulipigia kura.

 
Back
Top Bottom