Ushoga: Benki ya Dunia yasitisha mkopo kwa Uganda

ng'wandu

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2011
Posts
333
Reaction score
105
Benki ya dunia imesitisha mkopo wake wa dola million tisini kwa Uganda kwa sababu ya sheria mpya inayopiga vita mapenzi ya jinsia moja iliyopitishwa hivi karibuni nchini Uganda.

Maafisa wa benki ya dunia wanataka kwanza kuhakikishiwa kuwa miradi ambayo mkopo huo ungelielekezwa haitaathiriwa vibaya na sheria hiyo. Mkopo huo ulikuwa unalenga kuboresha huduma za afya nchini Uganda.

Sheria hiyo tayari imekosolewa sana na nchi za Magharibi, huku nchi wafadhili kama Denmark na Norway zikisema kuwa misaada yake ambayo ilikuwa imekusudiwa kupewa serikali ya Uganda sasa itaelekezwa kwa mashirika ya misaada.

Naye John Kerry, waziri ya Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani, akiita sheria hiyo kuwa ni ya mauaji. Yeye pamoja na mshindi wa tuzo ya Nobel kutoka Afrika ya Kusini, Desmond Tutu waliilinganisha sheria hiyo na sheria za wanazi wa Ujerumani na ile ya ubaguzi wa rangi ya Afrika ya Kusini.

Msemaji wa Benki ya dunia alisema kuwa wameamua kusitisha mkopo huo hadi hapo watakapojiridhisha kwanza kuwa miradi iliyokuwa imekusudiwa haitaathiriwa vibaya na sheria hiyo.

Uamuzi wa Benki ya Dunia kusitisha mkopo huo inakuwa ni pigo kubwa kwa serikali ya Uganda tangu ilipopitisha sheria hiyo mapema wiki hii.

Rais Yoweri Museveni wa Uganda alitia saini muswada huo na kuufanya kuwa sheria kamili licha ya upinzani kutoka jumia ya kimataifa.

Hata hivyo maafisa wa serikali ya Uganda waliunga mkono uamuzi huo wa rais na kusema rais Museveni alitaka kuonyesha uhuru wa Uganda kujiamulia mambo yake yenyewe bila ya kusukumwa na mataifa ya Magharibi.

=========
Source: http://www.aljazeera.com/news/afric...d-uganda-over-gay-law-201422874410793972.html
 
Bongo VP maana sisi kilacku tuko kwao huko.sijui kama kweli mkulu atamkatalia obama
 
Wapuuzi sana hawa wazungu. Wanakuchagulia hadi namna ya kujamiiana. Duh!!!!
 
Huu ni wakati muafaka wa afrika kusimama pamoja dhidi ya udhalimu huu kwa mwafrika. Leo ni uganda na keaho ni tanzania. Tusikubali kuhalalisha us.en.ge na u.sa.gaji hata kama upo kwenye jamii yetu.

Problem ya Afrika ni unafiki umoja wetu upo midomoni lakini kimatendo ni zero. Mfano mzuri ni vita vya Libya vya kumuondoa Ghadaffi tuliishia kutoa matamko tu
 
Wapuuzi sana hawa wazungu. Wanakuchagulia hadi namna ya kujamiiana. Duh!!!!

Sisi waafrika ndio wapuuzi kwa kuendekeza ufisadi na nchi zetu kuendelea kuwa maskini na kupelekea kuwa ombaomba kwao. Ukisha kuwa ombaomba tegemea utakuwa mtumwa daima
 
Maana yake ni kwamba la ukubali nikufile au hupati ela yangu...
 
Mashirika mengi ya misaada hua nayaona yamekaa kinafiki. Wakienda tofauti na rais bas wanatishia kusitisha misaada. Sasa hua najiuliza hivi wanapositisha hiyo misaada wanamkomoa Rasi au hao wananchi wanojifanya wanawahudumia? Up.uuzi huu kutegemea misaada ya wanafiki.
 
bongo vipi maana kila kitu huku ni IMF kuanzia barabara, visima ,madaraja ina maana ss tumekubali kulana midume kwa midume au mijike kwa mijike...daaaaaah hichi kimya cha bongo kina nitisha sana.......maana kwa waislamu ukienda kuposa mwanamke then mwanamke ataulizwa kame amekubali au la....akiitika ndio au akikaa kimya inamaanisha amekubali......Sasa kwa hii ishu ya ndoa za jinsia moja TZ imekaa kimya kumaanisha kwamba imekubali...
 
sidhani kama USA/UK au nchi yeyote imelazimisha watu kuwa MASHOGA. Lakini kama mtu ni SHOGA au ameamua kuwa SHOGA aachwe aishi atakavyo na sio mumpangie au mumuue au kumfunga kwa sababu AMEAMUA kuwa shoga.

Huo ndio msimamo wao na haki za binadamu. Mimi binafsi sipendi USHOGA/MASHOGA lakini mtu akiamua kuwa shoga hainihusu afanye ushoga wake hayo ni maisha yake.wanachopinga USA na wenzao ni PERSECUTION dhidi ya mashoga,waacheni waishi watakavyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…