Ushuhuda: Biashara ya mchele ni ngumu mno!

Ushuhuda: Biashara ya mchele ni ngumu mno!

Nenda kwa mamantilie jaribu kuongea nao pengine wanaweza kununua kutoka kwako. Au jaribu kusikilizia wapi kuna shuhuli ya ubwabwa unaweza kuwapelekea wakaununua.

Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
Wale wanachukua Mchele wa 1300-1400 hawawezi kuchukua Mchele wa 1700_2000 eti kisa unatokea mbeya au unanukia mkuu
 
Mkuu kama hutojali naomba mawasiliano yako au nikucheck DM mzigo wangu huu wa Mchele ukiisha nikafate mtama. Leo nimeshinda hapo Mwananyamala kuanzia asubuhi mpaka jioni gunia zangu 5 zilishushwa hapo wakawa wananiambia kwa mtaji wangu hii biashara itanishinda na nitaona ugumu wake, wakanishauri nijaribu kwenye mtama au kunde, choroko pia alinambia Maharage japo mtaji wake ni Mkubwa. Niliulizia meza hapo Sokoni gharama yake ni kubwa Mara mbili ya mtaji wangu Kesho Mimi nitakua hapo nione sample mzuri inayohitajika Sokoni ili weekend hii nikatafute mtama kiongozi.

Nakupa maneno ya akiba ukiona mfanyabiashara anakwambia Bora biashara ya mtama wakati yeye anauza mchele huyo mwanga usoni na moyoni mchawi. Yaani jiulize wewe kwake kama nani hata akupe mchongo huo na yeye asifanye?

Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Nakupa maneno ya akiba ukiona mfanyabiashara anakwambia Bora biashara ya mtama wakati yeye anauza mchele huyo mwanga usoni na moyoni mchawi. Yaani jiulize wewe kwake kama nani hata akupe mchongo huo na yeye asifanye?

Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
Yeye auzi Mchele anauza nafaka zingine kama mtama n.k kaorodhesha hapo.
 
Pole sana mkuu!!hiyo biashara ina hitaji uzoefu mkubwa sana!!mala ya kwanza napeleka DRC, nilikuwa na kama tani 30!!kidogo niukimbie mzigo, kwani fitina niliyokutana nayo kutoka kwa wabongo wenzangu, uchanganye na lugha ya lingala na French, zinazozungumzwa huko, ilikuwa balaa, huku faranga, kule dola!!!utambue dola halali/fake!!ila nilipambana hadi nikatoboa!!siku ya kwanza niliuza kama faranga milioni 2, kuzibeba kwenye begi la mgongoni hadi bega linauma, kuzihesabu mate yalikauka, nikatafuta bakuli la maji ili kuhesabu.
Wenye mitaji mikubwa ndio wanafaidika mkuu
 
Mkuu kama hutojali naomba mawasiliano yako au nikucheck DM mzigo wangu huu wa Mchele ukiisha nikafate mtama. Leo nimeshinda hapo Mwananyamala kuanzia asubuhi mpaka jioni gunia zangu 5 zilishushwa hapo wakawa wananiambia kwa mtaji wangu hii biashara itanishinda na nitaona ugumu wake, wakanishauri nijaribu kwenye mtama au kunde, choroko pia alinambia Maharage japo mtaji wake ni Mkubwa. Niliulizia meza hapo Sokoni gharama yake ni kubwa Mara mbili ya mtaji wangu Kesho Mimi nitakua hapo nione sample mzuri inayohitajika Sokoni ili weekend hii nikatafute mtama kiongozi.
sawa haina shida... wewe ukifika sokoni ulizia kwa Mwarabu wanapouza nafaka utanikuta najulikana sana kwa kuuza nafaka za jumla nipo upande wa fremu sio sokoni mule ndani... ukiulizia utanipata fasta tuu...
 
Biashara rahisi kwenye makaratasi tu lakini ukifika field ndo unaona sasa moto wenyewe. Niliwahi kujitosa kwenye biashara ya mbao milioni 5 kweupe zikayeya ila baadaye nikapata watu wazuri wakongwe wa hiyo biashara wakanielekeza mambo ya muhimu sana ndo kidogo nikapata kaunafuu na baadaye nikafanya vizuri. Hakikisha hapo unaondoka na mafunzo yatakayokusaidia huko unakoenda. Hata kwenye kilimo usifikiri mambo ni rahisi kihivyo. Ongea na watu walioko huko utapata wenye roho njema watakupa ABC za hilo zao unalotaka kulima. Kwa umri huo ukiendelea hivi kutoboa is only a matter of time...future millionaire [emoji122][emoji122][emoji122]
Kweli aisee mambo ni mazito mno
 
Ukinunua mchele usiende kuuza sokoni, wale madalali nao wanataka wapige cha juu, shusha mzigo wako kisha ingia kitaa jwa wenye maduka ambao ndio wauzaji wa mwisho
Nimefikiria hvyo lakini nimepiga hesabu nimejikuta nitapata hasara...maduka hapa yako mbali mfano upeleke mzigo kimara gharama tu ya kusafirisha mzigo ndio faida yangu mkuu
 
Nenda Kwimba Mchele Huo Ulioweka Kwenye Picture Wao Wanauza Kilogram 1 Tshs 1200/=
Waki~Grade Yaani Kuchambua Kwenye Mashine Mzima Unauzwa Kilogram 1 Tshs 1300/=
 
Nenda Kwimba Mchele Huo Ulioweka Kwenye Picture Wao Wanauza Kilogram 1 Tshs 1200/=
Waki~Grade Yaani Kuchambua Kwenye Mashine Mzima Unauzwa Kilogram 1 Tshs 1300/=
Sasa hizo gharama ndio nimechukulia mbeya mkuu?...mfano niuchukulie kwimba kwa hiyo 1300 huku dar nitauza shingapi? Ondoa gharama zote za usafiri n.k
 
mimi nipo mwananyamala kwenye biashara za nafaka ila sio mchele ni mahindi mtama kunde na vitu kama hivyo.... kuhusu mchele wewe umejichanganya kwenda mbeya kununua mchele uje umuuzie mtu ili na yeye auze dukani kwake... kwasabab mimi nipo hapa sokoni najua jinsi biashara hiyo inavyoenda... fanya hivii tafuta ubao sokoni mwananyamala halafu uuze mchele wako wewe mwenyewe ukimaliza unaenda tena mbeya pale unamuacha kijana... sio kama unavyofanya wewe ila mtaji wako mdogo huwezi biashara hii ya mchele ungetakiwa uwe angalau milioni 20 ... fanya hivi nenda dodoma kanunue mtama kwa laki 7 yako utapata gunia 10 za mtama niletee mimi nitanunua
Vizuri
 
Imekuchukua muda gani tangu kuanza biashara hadi kukata tamaa!?

Unadhani kuna biashara ambayo ni rahisi kwamba utaanza leo kesho uone faida?

Kwenye kuanza biashara inatakiwa uvumilivu, kuna changamoto huwa hazikwepeki hasa kwa biashara mpya.

Kutokujua sehemu ya kuchukua mzigo, unapataje wateja na unafanyaje ili mteja atayenunua leo na kesho aje, huchangia ugumu wa biashara mwanzo.

NAKUSHAURI chagua biashara Moja na upambane nayo iwe jua iwe mvua.

Hata hao unawaona Wana mitaji mikubwa na wanapata faida walishapita hiyo stage ambayo wewe upo wakavumilia ndio unaona wapo hapo walipo.

MWISHO asije kukudanganya mtu kuwa kuna biashara rahisi, biashara ni rahisi ikiwa kwa mwenzio, kinachoonesha urahisi wa biashara ni uvumilivu, uzoefu na ubunifu mpya kila kukicha.

La SIVYO utakuwa mtu wa kuanza biashara mpya na kuacha
Umemshauri vizuri sana
 
mimi nipo mwananyamala kwenye biashara za nafaka ila sio mchele ni mahindi mtama kunde na vitu kama hivyo.... kuhusu mchele wewe umejichanganya kwenda mbeya kununua mchele uje umuuzie mtu ili na yeye auze dukani kwake... kwasabab mimi nipo hapa sokoni najua jinsi biashara hiyo inavyoenda... fanya hivii tafuta ubao sokoni mwananyamala halafu uuze mchele wako wewe mwenyewe ukimaliza unaenda tena mbeya pale unamuacha kijana... sio kama unavyofanya wewe ila mtaji wako mdogo huwezi biashara hii ya mchele ungetakiwa uwe angalau milioni 20 ... fanya hivi nenda dodoma kanunue mtama kwa laki 7 yako utapata gunia 10 za mtama niletee mimi nitanunua
Safi Sana, Ubarikiwe
 
Back
Top Bottom