Ushuhuda: Biashara ya mchele ni ngumu mno!

Good
 
Biashara ngumu sana aisee, mimi nilijaribu mara moja mwaka 2014 na nilinunua mchele wa mils 14 ubaruku mbeya.
Nikauleta kwanza nilikuwa nauza kwa jumla kwa wafanyabiashara faida iliyopatikana ndogo.
Nikaona work done, muda na mtaji na faida iliyotoka haviendani nikaachana nayo.
Wengine wanakopa kukulipa inachukua muda sana.
 
Pole ndugu ila ,MUNGU ni mwema utapata wateja urudishe hela yako , mbeya kuzuri na fursa ni nyingi sana kama unaweza rudi mbeya , kafanye research za biashara yoyote jiwekeze , ila ishi huko huko utakuja kunishukuru badae , tatizo graduates wengi mnapenda kubanana mjini na biashara za wakubwa zenu , walioanzia vijijini , leo wako mjini baada ya mabonde na milima.
 
Huu ushauri nimeuchukua, tatizo Mbeya sina ndugu sijui a,b c za huko Mimi Mchele niliagiza tu.
 
Maisha ni mapambano, Mimi nimepoteza hadi sasa jumla ya milioni 250 kwa biashara tofauti 15 lakini sijakata tamaa naamini zitarudi tu nipo kwenye mapambano makali
Maisha ni mapambano, lakini Mkuu nikuulize hiyo million 250 ulianza from scratch kama Mimi ? Au ulipata booster?..
 
Maisha ni mapambano, lakini Mkuu nikuulize hiyo million 250 ulianza from scratch kama Mimi ? Au ulipata booster?..
Hapana kidogo kidogo kwa project tofauti mfano nilianzisha biashara ya kupasua mbao ndugu yangu akanipiga mbao akalala mbele hapa ikapotea milioni 8,nilinunua chainsaw milioni 1.5 kwa kuhamasika takuletea elf 30 kwa siku niliambulia laki 20 tu na mashine ikafa huku niliyemkabidhi kapata zaidi ya milioni ,sikuwa na uzoefu wa magari niliingia kichwa kichwa kununua used nikaingia gharama za kubadili KILA kitu gari ilishinda zaidi garage kuliko barabarani mfano ya mizigo nilipambana nayo ikasimama dereva akaenda nayo porini ubishi wake akapiga mzinga akaicha porini imepasua injini so gharama ya kununua injini mpya au kuivuta kuleta mjini nikaiuzia huko huko porini kwa hasara,nikanunua daladala mbili ni kama nilinunua jini la kula pesa KILA siku natoa garage gari zimesimama corona imeingia level siti biashara hailipi nimezipaki mwaka mzima kusubiria hali kwenda kuwasha hamna kitu parking nao wanadai karibu milioni plus madeni ya nikauziuza kwa hasara hata mia sikupata nikalipa madeni.plus biashara zingine nyingi tu ikiwemo kilimo plus kutapeliwa viwanja unanua kwenye kampuni tumepigwa kesi ipo mahakamani utalipwa lini, kingine nimenunua kwa mtu kakiuza tena mtu mwenyewe mchovu hata kumi ya kukupa hana imebaki madai.
But Mimi nashukuru nimepata shule tosha kuhusu uwezekazaji na maisha. Kwa jumla nipo kwenye mapambano zitarudi tu.
Kukata tamaa ni hadi siku ya mwisho
 
Andika Kitabu cha maisha yako na hassle zako..., ingawa huenda usiambulie pesa ila publishing ebook ni bure..., kwa elimu hii utasaidia wengi na utabalance mizani ya kuonyesha uhalisia wa hii struggle...

Indeed Struggle is the Duty..., ila kama unapenda unachofanya hizi challenge zinapungua makali.

Tatizo kubwa la Bongo kwa sasa ni Utapeli na watu kukosa uaminifu..., bila kona kona ni ngumu sana ku-make it
 
Ameen
 
Lipia tangazo lako la biashara sasa kwani lishawafikia wateja wako
 
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… daaah eti lazima mji ukufurahishe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…