Aisee..
Miaka ya mwisho ya tisini, nilijiingiza kwenye biashara ya mchele, unakusanya maeneo ya Kagongwa, wilaya ya Kahama, halafu unapeleka kuuza Rwanda, miaka hiyo Faranga 1 ni sawa na shillingi 2 za TZ,
Nlianza na tu Tani tuwili tu, sababu Rwanda wananunua vigunia vya sandarusi vya kilo 50, kwao ndio standard ya manunuzi
Hapo na tugunia 40, usafiri ni unamlipa dereva wa semi trela anavipanga nje juu ya kontena.
Nimefika Kigali maeneo ya Majerwa ambapo ndio magari yote yanasimama, naisubiria Semi ifike, nimekaa gesti siku mbili, na ugeni ule natumia tuu, burusheti na Primus kwa sana, kumbe nakula hela ya ziada na sijui lini nitauza mchele, baada ya mchele kufika, nikachukua sample kama kilo 5 nazungusha kwenye maduka, duuh noma kweli naonekana mgeni kabisa mpaka wajeshi wakanibabatiza mjini miaka hiyo, maana kumbe wananiangalia naingia duka hili natoka mara duka hili nikakalishwa chini, nikahojiwa na nikatoa passpoti na kujieleza huku na kibegi changu cha sample ndio wakaniamini na kuniachia.
Nikampata Mzee wa kinyarwanda anataka vigunia 25, nikamletea lakini bei hata sio hivyo nzuri, hapo nimeshachoka nikakubali, sasa mbinde kuifata hela kila siku, zaidi ya wiki nafuatilia hela, gharama ndio zinazidi, na nikamalizia vigunia vingine kwa Mama mwingine wa Kiganda, kwa hasara tu, nikasema sirudii tena ndio ikawa mwisho kufanya biashara hizi hazieleweki.......
Sijui kwa sasa biashara ikoje kupeleka mchele Rwanda...