SHUHUDA: HATIMAYE AMETIKI (
based on my true story)
6th epsode
... Nikaamua siku hiyo nisiwe mvivu inatakiwa Nimutolee uvivu yaani niliamua kumtusi kua anavyo jiona na anavyo ishi nilianza kumshushia Nondo.
Kama hizi [emoji116]
"Ujue ukipendwa usjipe kiburi hvyo hata kama mtu humpendi.
Kwani wewe ni mtu wa kwanza kutongozwa yaan kisa hukunipenda ndio ujione kua wewe
ni wewe"
Nilimwambia mambo mengi nikamfundisha jinsi maisha yanavyo enda.
"Usiwe na akili za darasani tu jaribu kua na akili extra zikusaidie maisha".
Alijaribu kujitetea lakini nilizidi kumuwakia
"Yaani ujue unajion sana wewe.
Ni kama sifa kumblock mtu mara kwa mara.
Hivi ungepewa nafasi ya kuwa na mamlaka duniani ingekuwaje.
Yaani unatumia nguvu ya mzungu je ungekua Nayo wewe sasa"
Nilimwambia maneno mengi makali
"Ujue unaweza kua na maisha mazuri leo pia na ndugu wenye maisha mazuri.
Tabia hiyo itakufanya kuwadharau wengine lakini ipo siku unacho jivunia itatoweka"
"Ujue naumia sana unap jiona wewe ni wewe na kupenda kumzarau mtu yaani unamshusha kana kwamba yeye si kitu kwako"
Nilizidi kuporomoka
"Sawa leo unaniona mimi si kitu kwako ila amini ipo siku tabia kama hii utakuta kwa watu wengine.
Hebu jaribu kuishi na watu vizuri"
Maneno mengi sana nilimuwakia.
Yalivyo muingia akajibu tena kwa herufi kubwa
"OKAY, INATOSHA YALISHAISHA NA YALISHAPITA" "OKAY YAISHE"
Moyoni nikasema hapa hapa nikazie hizi zalau zimuishe
Nilimwambia tena maneno mengine
"Sawa ila endelea sina thamani kwak ila ninathaman kwa mtu fulani" akaanza kujibu kwa upole kuwa "Yale yote yaliyotokea nyuma nimeyasahau" na mimi nikasema hapa hapa ameanza kujirudi.
Nikaendelea kumchana na yeye alijibu kwa upole sana "Hayo nlishayapokea" likaendelea kumpa somo akasema ameelewa ila si kama ninavyo taka mimi. Akaanza kueleweka kidogo na mimi kuniomba "sawa isiwe kesi ila ukiendelea na zile tabia zako hatutoelewana hata kidogo" na mimi hapa hapa ndo nipitie kwenye hii mada nikiwa namuelekeza huku natupia kamba mara nikaona tukauli twake tunajirudi "ndo mnavyo danganyaga watoto wa watu,japo watoto wa watu hatunaga akili ila nyie mnachangia pakubwa sana. Kwakuwa watoto wa watu cheap kwaiyo ndo mnaitumia iyo nafasi"
Nikamuelekeza maisha yalivyo nikamwambia jinsi nilivyo mpenda yaani uongo mwingi ili kunogesha maongezi ili ajue anapendwa.
Nilimuelekeza sana mara akaanza kusema "apana ndo naanza kupata picha halisi kumbe ndo mlivyo yaani mnajua kudanganya" na mimi nakazia hapo hapo naona anajileta nikamuelekeza zaidi mara akaanza kuniuliza na mimi "kwamba ndo tuanze kuiga maisha ya watu wengine" nilijitahidi sana kuteka hisia zake siku hiyo. Nikamwambia aniamini mara ohhh "we siwezi kukuamini kwa chochote" nikamsomesha mtoto Mungu si asumani mtoto akatiki akasema "Sawa nimekuelewa basi nisamehe kwa yote yaliyo tokea nyuma tuanze maisha mapya lakini usije niumiza" na mimi moyoni yes nikajua tayari mtoto kaingia King kwahiyo nacheza popote.
Ilikua ni chating kuanzia saa3usiku tulivyo anza kuzodoana hadi inafika muda wa saa nane usiku ilikuwa siku ya kuamkia j'pili.
Hivyo ndo mkeka wangu ulitiki.
Note: Kumbe sometimes si kuwabembeleza ni kuwafokea na kuwabembeleza tena(Yaani kwa lugha nyepesi ni kung'ata na kupuliza).
Hivyo ndio binti Adelina alivyo ingia kwenye mikono ya mtu mzima
kasomi kipindi hicho.
Shuhuda: Hatimaye Ametiki