SHUHUDA: HATIMAYE AMETIKI (
based on my true story)
6th epsode
... Nikaamua siku hiyo nisiwe mvivu inatakiwa Nimutolee uvivu yaani niliamua kumtusi kua anavyo jiona na anavyo ishi nilianza kumshushia Nondo.
Kama hizi [emoji116]
"Ujue ukipendwa usjipe kiburi hvyo hata kama mtu humpendi.
Kwani wewe ni mtu wa kwanza kutongozwa yaan kisa hukunipenda ndio ujione kua wewe
ni wewe"
Nilimwambia mambo mengi nikamfundisha jinsi maisha yanavyo enda.
"Usiwe na akili za darasani tu jaribu kua na akili extra zikusaidie maisha".
Alijaribu kujitetea lakini nilizidi kumuwakia
"Yaani ujue unajion sana wewe.
Ni kama sifa kumblock mtu mara kwa mara.
Hivi ungepewa nafasi ya kuwa na mamlaka duniani ingekuwaje.
Yaani unatumia nguvu ya mzungu je ungekua Nayo wewe sasa"
Nilimwambia maneno mengi makali
"Ujue unaweza kua na maisha mazuri leo pia na ndugu wenye maisha mazuri.
Tabia hiyo itakufanya kuwadharau wengine lakini ipo siku unacho jivunia itatoweka"
"Ujue naumia sana unap jiona wewe ni wewe na kupenda kumzarau mtu yaani unamshusha kana kwamba yeye si kitu kwako"
Nilizidi kuporomoka
"Sawa leo unaniona mimi si kitu kwako ila amini ipo siku tabia kama hii utakuta kwa watu wengine.
Hebu jaribu kuishi na watu vizuri"
Maneno mengi sana nilimuwakia.
Yalivyo muingia akajibu tena kwa herufi kubwa
"OKAY, INATOSHA YALISHAISHA NA YALISHAPITA" "OKAY YAISHE"
Moyoni nikasema hapa hapa nikazie hizi zalau zimuishe
Nilimwambia tena maneno mengine
"Sawa ila endelea sina thamani kwak ila ninathaman kwa mtu fulani" akaanza kujibu kwa upole kuwa "Yale yote yaliyotokea nyuma nimeyasahau" na mimi nikasema hapa hapa ameanza kujirudi.
Nikaendelea kumchana na yeye alijibu kwa upole sana "Hayo nlishayapokea" likaendelea kumpa somo akasema ameelewa ila si kama ninavyo taka mimi. Akaanza kueleweka kidogo na mimi kuniomba "sawa isiwe kesi ila ukiendelea na zile tabia zako hatutoelewana hata kidogo" na mimi hapa hapa ndo nipitie kwenye hii mada nikiwa namuelekeza huku natupia kamba mara nikaona tukauli twake tunajirudi "ndo mnavyo danganyaga watoto wa watu,japo watoto wa watu hatunaga akili ila nyie mnachangia pakubwa sana. Kwakuwa watoto wa watu cheap kwaiyo ndo mnaitumia iyo nafasi"
Nikamuelekeza maisha yalivyo nikamwambia jinsi nilivyo mpenda yaani uongo mwingi ili kunogesha maongezi ili ajue anapendwa.
Nilimuelekeza sana mara akaanza kusema "apana ndo naanza kupata picha halisi kumbe ndo mlivyo yaani mnajua kudanganya" na mimi nakazia hapo hapo naona anajileta nikamuelekeza zaidi mara akaanza kuniuliza na mimi "kwamba ndo tuanze kuiga maisha ya watu wengine" nilijitahidi sana kuteka hisia zake siku hiyo. Nikamwambia aniamini mara ohhh "we siwezi kukuamini kwa chochote" nikamsomesha mtoto Mungu si asumani mtoto akatiki akasema "Sawa nimekuelewa basi nisamehe kwa yote yaliyo tokea nyuma tuanze maisha mapya lakini usije niumiza" na mimi moyoni yes nikajua tayari mtoto kaingia King kwahiyo nacheza popote.
Ilikua ni chating kuanzia saa3usiku tulivyo anza kuzodoana hadi inafika muda wa saa nane usiku ilikuwa siku ya kuamkia j'pili.
Hivyo ndo mkeka wangu ulitiki.
Note: Kumbe sometimes si kuwabembeleza ni kuwafokea na kuwabembeleza tena(Yaani kwa lugha nyepesi ni kung'ata na kupuliza).
Hivyo ndio binti Adelina alivyo ingia kwenye mikono ya mtu mzima
kasomi kipindi hicho.
Shuhuda: Hatimaye Ametiki
Amani iwe nanyi ndugu zangu!!!!
Natumaini tunaendelea na majukumu yetu vizuri ,kikubwa ni uhai.
NAKAZIA KWA HII EPISODE YA6
nlikuwa na case kama yako miaka kadhaa nayo mwishoni ikaja kutiki.
Ilikuwa hivi miaka kadhaa iliyopita nipo jeshini mujibu wa sheria, nje ya hanga letu niko na inmate wangu mmoja tukiwaza tunaendaje kuitafutaa saa sita ya mkesha.
Basi wakati tunapiga story hapo hangani mlangoni ,wakawa wanapita makurutu kwenda kwenye kombania zao na kwa kuwa hanga letu ni la kwanza na liko njian kabisa ikawa ni rahic kuwaona watu wakipita.
Basi stories zimeendaa ,akaja dada mmoja ,jamaa yangu akamuita tu amzinguee kama unavojuaa watoto wa kiume mbele ya sketi (joking) ,basi yule dada akaja wakapiga story kadhaaa ......... Maraaa paaaaaap jamaaa akanirushia mtoto niendeleee kumchatisha aaah basi kishingo upande nikapokea usukani...... Kumbe jamaaa alikuwa amemuona manzi wake anakuja hangani kwetu sasa ili kuzuga akaniacha nae mie.
Basi mie story mbili tatu ,tukafahamiana ,akanipa namba yake ....... Sikuwa na simu hapo hivo nkaikariri kichwani ........ Usiku paaaaap nikamcheki ..... Kwanza alishangaaa kuona nimeishika ile namba.
Basi life likasonga sikumtongoza ila nikawa naonesha kama namuhitaji ...... Sikushindwa kumtongoza but kumwambia mtu nampenda ilihali na mtamani tuu huwa siwezi mara nyingi.
Kuna siku nkamuita nlikuwa na pipi ,nikataka nimlishe akagoma ,nkaona sio mbaya nkampa pipi yake akatembeaa.
Siku tunachat nkamuuliza mbona uligomea nkulishe pp, akasema ye cjui anamtu huko kombania yao C mie nlikuwa A coy ya demo ,basi kuanzia hapo nkimhitaji kumuona anaznguaa kujaaa ........ Siku zimeeenda ,tunamalizia kumaliza kozi ...disco nalo liko njian linakujaaa .... Ntapata wapi wa kucheza nae ..nkaona sio mbya nimtafutee huyu dadaaa. Nlifua dafu akawa anasema anamtu wakee, basi ikashindikana.
Kuanzia siku hiyo ambayo alikataa kulishwa pipi ,hadi naondoka sikufanikiwa kumuona hasa ukizingatia nlikuwa kambi moja yenye baridi sana pale 841kj ,kwahiyo kuvaaa mizura na manguo mengi mengi ma pull over yanakufanya ushindwe kumtambuaa mtu vzuri though yalikuwa yanakatazwa lakini kutokana na baridi ya Mafingani palee tukawa tunavaa na maboshori kibishiii..... Ila usidakwe tu na Afande Captain Moshi.
MUHIMU:Kipindi niko jeshini nliibiwa cmu yangu, nimeenda kufoleni master parade,nkaja Nikapigwa cmu muda sana, nkarudi likizo mzee akanipa simu yake niitumiee ilikuwa nokia Lumia na ndio nliokuwa natumia kuchati na huyu mtoto serengeti at that time.
Sasa tuendeleee
Tumerudi kutoka jeshini nikawa namtafuta mtoto wa watu ,akawa anajifanya hanijuii ,nkakitambulisha pale weeee ,kama kawaida yao ,eewwh ulikuwa unassmaje .....nabaki nimeishiwa pozii.. nkaona niifute tu ile namba.
Siku wiki miezi na miaka imepita niko chuo ,nikawa na connect simu yangu nokia niitumie kwa pc , nkaja kuonana na chats zetu .....aaaaah nkamkumbuka ni fulan ,at that ikumbukwe nlikuwa na simu ya whatsapp basi nkamcheki ,kama kawaida maswali yao yale ,namba umetoa wapi,shida yako nk .
Basi nkakitambulisha akasema hanikumbuki but mie nkawa namtajia kila event tulofanya tukiwa jeshini... Stilll hakuwa anakumbuka...
CENTRAL THEME:Kimbembe kikaanzia hapaaa nkaaamua nimtoleee uvivu, yule dada alikuwa mfupi,kadogo dogo, so nkamponda sana siku hiyoo ,nlimuambia maneno makali sana ,naye piaa akawa ananijibu basi tumejibizana matusi makubwa sana ...... Nikamtusiiii weeee then nikamblock ,asireply ,baada ya siku kadhaaa nika unblock.
Kwakuwa mie nlikuwa namjuaaa ,yale yote nlompondea yalikuwa yakweli lakini ye kwa kuwa hajui adui yake yukojee alikuwa anatusi haya matusi mengine hayaa makubwaa though Nlimtumia picha ya selfie.
Basi bhana kwakuwa nlikuwa na hasira sana sikuhiyoo wakati tunatukanana lakin baada ya siku kadhaa nlipowa nkaona sio fair kufight na mtoto wa kike ,nkamuomba radhi kwa kumtukana though na yeye alinitusi sana.
Basi akaanza lalalma palee lakini mie nlitaka tu tuyamalize kila mtu abaki kama zamani kwahio nlikuwa nakubali tu ili yaishe ....dada kuona vilee nayee akaaanza jirudi sasaa.
Naye akaniomba msamaha..... Yakaisha tukaaanza ukurasa upyaaa wa urafiki basi tukafahamiana vzuri, tukaja kuwa best friends sana though tuko mkoa mmoja but cjapata time ya kukutana nae since tutoke jeshini.
HUZUNI: Mwaka huu mwezi wa 2 alifiwa na mama yake, akanambiaa though alichelewa nambia tokana na hali ilivokuwa kipindi tukio latokea , MBAYA ZAID mwezi huu wa nne tena kampoteza baba yake piaaaa.
Akaja nambiaaa Fulani na baba piaa kaniachaaa ,nkampa poleeee paleeeee
Maisha yanaendelea ,lakini kawa rafki yangu mzuri mno.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kazi iendeleeeee.
Nakuja na kisa kingine ,ngoja mkono upoeee kidogoooo....