USHUHUDA: Kuku wa kienyeji (Pure) - Biashara kichaa isiyo na tija

Kanda ya ziwa msitusahau, mimi nipo mwanza kwa mdau mwenye idea ya hawa chotara anipe abc pls
 
Mkuu naomba utujuze huo mchanganyiko wa msosi mpka kuku wa kienyeji wanataga non stop.
 
Mimi nakubaliana na Ginner. Mambo makubwa anayoyaeleza: 1) tufuge kuku chotara 2) biashra ya mayai ya kuku kienyenyi au chotara sio biashara nzuri, 3) tunaweza kuapata faida zaidi kama mfugaji atatotolesha mayai ya kuku chotara kwa mashine ya kutotolea vifaranga (incubator). Mimi ni mfugaji wa kuku tangu mwaka 2006. Nakubaliana naye.
 
Mkuu naomba utujuze huo mchanganyiko wa msosi mpka kuku wa kienyeji wanataga non stop.
search kwenye web ya hawa jamaa wameweka mchanganuo wa vyakula vya kuku aina zote na kinafanya kazi kweli sema wengi huwa hatuamini hizi vitu bila kujaribu
www.rldc.co.tz
 
Mkuu hao kuku chotara hapo tazara ulichukua kwa bei gani pamoja na ukubwa wao nataka kupata jogoo mkubwa na tetea wawili angalau wale nitakua ndo uzao wa kwanza msaada tafadhali maana Kuna watu hawajibu ukiwauliza
wanauza vifaranga hawauzi wakubwa bei ni 500 kwa kifaranga wakati niliponunua mwezi wa 3 mwaka huu nazani hawajapanda kama wamepanda c ghali sana
 
Nimesoma makala yako kwa undani but mengine si kweli.n imegundua pia unavutia biashara yako pia!
Kwa mfano mm nilianza na kuku 3,majike 2 na dume 1 wa kienyeji.ilikua mwisho wa mwezi wa 12 mwaka jana 2015. But mpaka mwez wa sita mwaka huu nilikuwa nimepata kuku zaid ya 60. Kuku wangu wanataga wastan wa mayai 15-18. Na kila baada ya miezi miwili ni lazima watoto.ninachokifanya vifaranga nilikua nabitunza mwenyewe toka siku ya kwanza kutotolewa .
Kuku wangu wanataga kila baada ya wiki 2 baada ya kutotoa.
Tena nimegundua njia nzuri ya kuku wa kienyeji kutotoa vifaranga kuanzia 20-24. Kwa wakati mmoja na kwa kuku mmoja.
Kuku wa kienyeji wanalipa kama itaamua kukomaa na kufuata maelekezo.
Ufugaji wa kuku wa kienyeji una changamoto zake japo zinaweza tatulika pia.
 
wanauza vifaranga hawauzi wakubwa bei ni 500 kwa kifaranga wakati niliponunua mwezi wa 3 mwaka huu nazani hawajapanda kama wamepanda c ghali sana
Mmnh sawa mkuu shukrani sana kingine nilikua nauliza kwa hapa ninao kuku wa nne wanaatamia na mwingine anataga je hao vifaranga vipya naweza kuvichanganya katika kuku wapya watakaototolewa Bila madhara yoyote kwa hao vifaranga chotara
 
Mmnh sawa mkuu shukrani sana kingine nilikua nauliza kwa hapa ninao kuku wa nne wanaatamia na mwingine anataga je hao vifaranga vipya naweza kuvichanganya katika kuku wapya watakaototolewa Bila madhara yoyote kwa hao vifaranga chotara
yah unaweza kuwachanganya hawana shida,,,muhimu waweke sehemu yenye joto la kutosha na isiyofikiwa na wadudu wakali kama paka.....utakapo wachukua siku ya kwanza hadi ya saba unawapa maji uliyochanganya glucose na antibiotic ya OTC 20% ili kuwakinga na maambukizi yanayoweza tokea hadi siku ya saba unawachanja chanjo ya newcastle.....
 
Ahsantee mkuu nakusumbua ila naamini Kuna wengine wanapata somo pia sasa kama nitawachanganya si watalelewa pamoja na hawa waliototolewa maana yake joto atapata kupitia huyu tetea au Kuna namna nyingine ya kuwapatia joto
 
Mkuu. Njia gani hiyo unayoitumia mpka kuku wa kienyeji wanataga mayai 20-24. Msaada tafadhali mkuu
 
Umeongea uhalisia mtupu,

1. Mfugaji anaetaka maendeleo kutokana na ufugaji wa kuku hawezi kumuacha kuku alee vifaranga kwa miezi 3 inabidi ajifunze kulea vifaranga kwa njia mbadala

2. Ni kweli kuku ukimnyang'anya vifaranga baada ya wiki 2 anataga upya

3. Si lazima kuku akitaga atamie mwenyewe, kwani kuku mkubwa anauwezo wa kutamia hadi mayai 20+, hivyo unaweza ukachagua kuku wenye maumbo makubwa wakawa wanatamia mayai yao pamoja na yanyongeza utakayoyatoa kutoka kwa kuku wengine


Kwa nyongeza tu, ukiwa na kuku 20(mitetea), unaweza ukajizalishia vifaranga 100+ kila mwezi....
 
Mkuu. Njia gani hiyo unayoitumia mpka kuku wa kienyeji wanataga mayai 20-24. Msaada tafadhali mkuu
Mkuu nimesema kuku wangu hutaga wastan wa mayai 15-18 hivyo mayai mengine hua nanunua kukamilisha lengo langu.kwa hio kama atakuwa ametaga mayai 15 hapo naongeza mayai 10 ili niweze pata vifaranga 20+.
 
Kuna jamaa yangu mmoja alinielekeza namna nzuri ya kuku kutotoa mayai yote bila kuacha. Ni kwamba aliniambia ninunue vile vibeseni vidogo vya kunawia then ndan unaweka mchanga kiasi halafu weka mayai yako tayari kwa kuliwa na kuku. kiukweli njia hii nilitumia na imefanikiwa. kwa wafugaji wenzangu jaribuni muone maajabu yake.
Kitu kingine ni utunzaji wa vifaranga baada ya kutotolewa napo hapa kuna changamoto wakati wa usiku kutokana na barid kwa vifaranga hasa kwa wafugaji wa hali ya chini,mm mwanzo nilihangaika but nikapata njia nyingine bora ya kutunza vifaranga wakati wa usiku,nilitenga sehm ya kuwalaza. Hapa unaweza chukua hata box kubwakubwa la kuwatisha vifaranga then nikatafuta chungu!! Nikaweka majivu ndani kwa hio kila usiku nilikua unaweka mkaa wa moto mle ndani ya chungu na kufunika na majivu!! Nakwambieni ndugu zangu wafugaji vifaranga hawapati barid kabisaaa! Na huo moto ulioko ktk hilo jivu utaukuta mpka asubuhi na utatumia kwa kuwashia moto hapo kwa nyumba yako. jaribuni na njia hii muone mafanikio yake na si kukaa ohhh nitanunua vifaranga 500 nianze hapana anza hata na kuku 2 au 3 baada ya mda utakuja nambia. Yangu ni hayo labda hujaelewa uliza tupeane maujuzi.
 
Getting interesting. Hata mm mfugaji mtarajiwa wa kuku napata masomo hapa.
 
Asante kwa elimu nzuri uliyotoa nimekuelewa mkuu.
 
wanauza vifaranga hawauzi wakubwa bei ni 500 kwa kifaranga wakati niliponunua mwezi wa 3 mwaka huu nazani hawajapanda kama wamepanda c ghali sana
Wapi naweza kupata vifaranga chotara kama 200
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…