sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Hiki kitu nimeshuhudia kuna mtoto wa ndugu yangu anasoma shule flani ya msingi darasa la nne, ni shule ya mtaala wa kiingereza ila walimu ni wa hapa kwetu, huwa anafaulu vizuri tu lakini kuna maswali aliniletea nimsaidie ya social studies (maarifa ya jamii) sasa nikawa namweleza swali linamaanisha nini kwa kiswahili ili nione kama kaelewa ndio nimsaidie lakini alikuwa anapata wakati mgumu, ajabu ni kwamba nikimuliza maswali ya homework zake za zamani majibu ananipa vizuri ila nikumuuliza maana ya maswali niliyomuuliza inakuwa taabu kidogo.
Pia katika maswali nimeona kwa level ambayo yupo walimu wao wa hapa kwetu wana complicate sana mambo kwenye lugha hasa kwa kutumia misamiati migumu kidogo kwa mtoto wa darasa la tatu.
Kwa upande wa mtoto wangu, nae yupo darasa la nne shule yao ni ya mtaala wa kiingereza ila walimu wengi wametokea Zambia, kiukweli kwenye lugha hata kunipa tafsiri huwa sio tabu na walimu wao sio kwamba hizi kugha wamejifunzia ukubwani bali ni lugha za nchi yao kwa hio kuna njia rahisi zaidi wanatumia ili watoto waelewe.
kuna siku kulikuwa na mhubiri anaeongea kiingerea ilibidi awe anatafsiriwa na , basi mtoto wangu alikuwa nae anatafsiria wenzake vizuri kabisa kiukweli nilikuwa nafarijika, mtu kama kiingereza kimepanda kutafsiri ni ishu ndogo tu.
Mapendekezo:
Ni bora zaidi kumpeleka mtoto kwenye shule ya kiingereza yenye walimu ambao asili ya nchi zao kiingereza ni mojawapo ya lugha za taifa tangu utotoni mtu anaitumia. kama ni kumpeleka mtoto shule ambazo walimu ni wenye asili ya hapa kwetu ambako wengi huanza kujifunza kiingereza sekondari basi tuwe tunajihakikishia lugha wanaielewa vizuri.