Ushuhuda kutoka kwa Shehe Omari Mnyeshani

Mwendelezo wa masimulizi ya tambiko la Lindi
 
Attachments

  • PART16_MWENYEKITI_WA_WACHAWI_TZ__SHEKHE_ALIEOKOKA_NILIUA_MKE_NA_KUISHI_NAE_TENA_UCHAWI__NIMESO...mp4
    43.1 MB
Wazee wa bagamoyo walimfata shetani mapangoni kumuomba msaada awaondoe wakoloni.
Shetani akawapa sharti wataondoka lakini mtakuwa masikini yaani umasikini ndio uwe kafara.
Kafara ni sadaka unayompa shetani ili afurahi.
Wazee wakakubali kuliko maendeleo yalitwayo na wakoloni ni heri tuwe uhuru ndani ya ufukara
Thus baada ya uhuru mwalimu pesa alizorithi kwa wakoloni badala ya kuzifanyia maendeleo akazichezea kwenye ukombozi wa nje zingine na zilizobakia akazitumia kumuondoa Iddi amini ili amrudishe Obote kwenye kiti,akaja na masera ya kimasikini mfano ujamaa,uhujumu uchumi,kuwazuia watz wasipate exposure ya kusafiri nje ya nchi kwa kuweka mashart magumu kupata passport.
 
Uchawi unafanyika sana tena mwingine ni wa nia za ovyo kiasi ya kwamba ukiambiwa utashangaa, lakini always kuna nguvu fulani ya asili huwa inaleta ukinzani. Na wachawi wanaelewa kwamba uchawi hauwezi kutawala dunia kwa asilimia 100
Dah
 
Nimeamua kuuandika kwa vile upo YouTube, lakini sikubaliani wala kupingana na msimuliaji.

Ni ushuhuda wa bwana mmoja anayejiita Shehe Omari Mnyeshani, Mchawi wa "zamani".

Anadai kuwa kabla ya kuukimbia uchawi, alikuwa Mwenyekiti wa wachawi Tanzania na nje ya Tanzania.

Ikiwa anayoyaongea yana ukweli, basi nchi yetu inahitaji "ukombozi" wa Kimungu. Lakini ikiwa tu ayasemayo ni ya kweli.

Anadai kuwa kabla ya kuachana na uchawi, kuna mwaka walifanya tambiko la Kitaifa la kuizindika nchi, tambiko ambalo lilifanyikia mkoani Lindi. Shughuli hiyo iliwahusisha wachawi wote wa Tanzania. Nafikiri ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya 90, kama sijakosea.

Katika hilo tambiko, waliazimia mambo kadhaa, ikiwemo la Waziri Mkuu wa Tanzania kutokushika madaraka ya Urais.

Kwamba, haijalishi Waziri Mkuu atajitahidi kiasi gani, haitakaa itokee awe Raisi wa JMT. Akishaushika tu Uwaziri Mkuu, na Urais anakuwa ameshaukosa. Kama ndivyo, na ikiwa nguvu kubwa kuliko ya wachawi haitaingilia kati, Majaliwa hayakuwa Rais wa JMT. Vile vile, isingewezekana kwa John Malecella, David Msuya, Frederick Sumaye, Edward Lowassa na Mizengo Pinda kukushika Urais wa Tanzania. Wote hao walishashika nafasi za Uwaziri Mkuu.

Hilo tambiko lilikuwa na athari kwa mkoa wa Lindi, kwamba watu wake hawatakuwa na uwezo mzuri kiakili.
Ardhi ya Lindi ilitolewa kama kafara kufuatia hilo tambiko la kichawi kufanyikia huko.

Inasemekana kuna kipindi Serikali iliweka jitihada ya kuwasisitiza watu wa huko kutumia chumvi ya viwandani ili kuwaongezea uwezo wa kufikiri, kwa kudhaniwa kuwa ni ukosefu wa madini muhimu ndiyo uliokuwa ukiwapelekea watoto wa huko kuwa chini kimasomo. Lakini kwa mujibu wa huyo mchawi wa zamani, ni kwa sababu Lindi ilitolewa kama Kafara wakati wa hilo tambiko.

Wachawi wa Lindi walijulishwa kabla ya hilo tambiko kuwa hayo madhara yatawatokea wana Lindi, na wakataka likafanyikie Tanga au Tabora lakini wachawi wa hiyo mikoa wakajitetea kuwa nao walishatoa michango yao siku za nyuma. Wachawi wa Lindi japo hawakutaka mkoa wao uwe duni, walishindwa kulikwepa hilo la tambiko kufanyikia kwao.

Jambo lingine aliloliongelea ni uchaguzi wa 1995. Anadai kuwa katika rada yao ya kichawi, waligundua kuwa mtu aliyekuwa amekusudiwa na Mungu awe Rais wa Tanzania kipindi hicho ni Jackson Makweta. Lakini walipobaini kuwa Makweta anaweza akawa kero kwao, waliamua kupambana naye kwa kumwondolea wazo la Urais, na wakafanikiwa.

Aliyeyasema hayo ni Shehhe Omari Mnyeshani!

Japo sijakubali wala kukataa, nina maswali kadhaa kuhusu hayo madai yake.

1. Ni kweli kuwa watu wa Lindi wana uwezo mdogo kiakili? Mbona Mama Salam Kikwete na marehemu Bernard Membe ni watu wa Lindi lakini wako vizuri upstairs?

2. Unafikiri kwa hoja yake kuwa katika tambiko la mwisho la kuisindika Tanzania kichawi walikubaliana kuwa mtu aliyeshika nafasi ya Uwaziri Mkuu asifanikiwe kuwa Rais wa JMT, inaweza kuwa na mashiko?

3. Kwa mujibu wa simulizi yake, Makweta ndiye aliyekusudiwa na Mungu awe Rais wa JMT 1995. Unafikiri Makweta angefanya vizuri kumzidi Mkapa?

4. Japo masimulizi yake hayawezi kuthibitishwa Kisayansi, unafikiri nguvu za giza zina nafasi kwenye utawala wa Tanzania?

Hapo chini ni moja ya shuhuda zake

Part 14 inaelezea chimbuko la mbio za mwenge Tanzania, na part 15 inahusiana na zindiko la Lindi

Part 16 ni mwendelezo wa masimulizi ya tambiko la Lindi
Hivi kumbe it is a formal institution kabisa na uongozi katika ngazi ya taifa na mikoa. Je criteria ya kuingia, vigezo ni nini jamani tuelimishwe...
 
Personal digest!

1.ccm ni chama Cham wachawi !

2.vyama vingine ni vyama vya kichawi vidogo vidogo!

Sawa!!

Inamaana wanachama wote wa hivi vyama na mimi nikiwemo ni wachawi!!SI ndio!!?
 
Hivi ndo vile vipindi wanaendeshwaga watu kuwa anapelekwa pangoni kuongea na mizimu, kumbe wahuni wametangulia wametulia nyuma ya mimawe na speaker...

Anapangwa pangwa pale na maneno na maagano ya uongo na kweli.

Kisha anaambiwa atoe hela zisomewe ili akirudi nazo mjini zikazae maradufu.... wanakuwa wameshajua kabisa amekuja na sh ngapi maanaawasiliano yanaanzaga na simu.

Watu wanambadilishia bag kijanja janja, kisha anapewa sharti la kutofungua bag mpaka afike nyumbani kwake.
 
Kutokana na maongezi ya Shehe Mnyeshani.
Watu waliohudhuria katika Kafara la Bagamoyo walikuwa Wachawi Nguli wafuatao.

1. Mzee Forojo Ganze Master

2. Mzee Primus Mubanga Julius

3. Mzee Shaibu Kalole Mtiga

4. Shehe Yahaya Hussein

5. Mzee Mfaume Golo Tumbo

6. Mzee Muhammedi Abubakari
Musindamba

7. Shehe Muhammedi Mwinyi Mnyeshani Jibulani (msimuliaji)

Hao ni Vigogo watupu walio fanya zindiko kwa kuongea na Shetani Lusifer ana kwa ana.
Lucifer aka shauri Julius Nyerere aitwe Baba wa Taifa, na Pia Mwenge ukimbizwe ndani ya Nchi.

Eti ulete
Tumaini pasipo Tumaini
Upendo mahali penye Chuki
Na Heshima palipo jaa Dharau.

Bado nafuatilia mazungumzo.
 
Nimeamua kuuandika kwa vile upo YouTube, lakini sikubaliani wala kupingana na msimuliaji.

Ni ushuhuda wa bwana mmoja anayejiita Shehe Omari Mnyeshani, Mchawi wa "zamani".

Anadai kuwa kabla ya kuukimbia uchawi, alikuwa Mwenyekiti wa wachawi Tanzania na nje ya Tanzania.

Ikiwa anayoyaongea yana ukweli, basi nchi yetu inahitaji "ukombozi" wa Kimungu. Lakini ikiwa tu ayasemayo ni ya kweli.

Anadai kuwa kabla ya kuachana na uchawi, kuna mwaka walifanya tambiko la Kitaifa la kuizindika nchi, tambiko ambalo lilifanyikia mkoani Lindi. Shughuli hiyo iliwahusisha wachawi wote wa Tanzania. Nafikiri ilikuwa mwanzoni mwa miaka ya 90, kama sijakosea.

Katika hilo tambiko, waliazimia mambo kadhaa, ikiwemo la Waziri Mkuu wa Tanzania kutokushika madaraka ya Urais.

Kwamba, haijalishi Waziri Mkuu atajitahidi kiasi gani, haitakaa itokee awe Raisi wa JMT. Akishaushika tu Uwaziri Mkuu, na Urais anakuwa ameshaukosa. Kama ndivyo, na ikiwa nguvu kubwa kuliko ya wachawi haitaingilia kati, Majaliwa hayakuwa Rais wa JMT. Vile vile, isingewezekana kwa John Malecella, David Msuya, Frederick Sumaye, Edward Lowassa na Mizengo Pinda kukushika Urais wa Tanzania. Wote hao walishashika nafasi za Uwaziri Mkuu.

Hilo tambiko lilikuwa na athari kwa mkoa wa Lindi, kwamba watu wake hawatakuwa na uwezo mzuri kiakili.
Ardhi ya Lindi ilitolewa kama kafara kufuatia hilo tambiko la kichawi kufanyikia huko.

Inasemekana kuna kipindi Serikali iliweka jitihada ya kuwasisitiza watu wa huko kutumia chumvi ya viwandani ili kuwaongezea uwezo wa kufikiri, kwa kudhaniwa kuwa ni ukosefu wa madini muhimu ndiyo uliokuwa ukiwapelekea watoto wa huko kuwa chini kimasomo. Lakini kwa mujibu wa huyo mchawi wa zamani, ni kwa sababu Lindi ilitolewa kama Kafara wakati wa hilo tambiko.

Wachawi wa Lindi walijulishwa kabla ya hilo tambiko kuwa hayo madhara yatawatokea wana Lindi, na wakataka likafanyikie Tanga au Tabora lakini wachawi wa hiyo mikoa wakajitetea kuwa nao walishatoa michango yao siku za nyuma. Wachawi wa Lindi japo hawakutaka mkoa wao uwe duni, walishindwa kulikwepa hilo la tambiko kufanyikia kwao.

Jambo lingine aliloliongelea ni uchaguzi wa 1995. Anadai kuwa katika rada yao ya kichawi, waligundua kuwa mtu aliyekuwa amekusudiwa na Mungu awe Rais wa Tanzania kipindi hicho ni Jackson Makweta. Lakini walipobaini kuwa Makweta anaweza akawa kero kwao, waliamua kupambana naye kwa kumwondolea wazo la Urais, na wakafanikiwa.

Aliyeyasema hayo ni Shehhe Omari Mnyeshani!

Japo sijakubali wala kukataa, nina maswali kadhaa kuhusu hayo madai yake.

1. Ni kweli kuwa watu wa Lindi wana uwezo mdogo kiakili? Mbona Mama Salam Kikwete na marehemu Bernard Membe ni watu wa Lindi lakini wako vizuri upstairs?

2. Unafikiri kwa hoja yake kuwa katika tambiko la mwisho la kuisindika Tanzania kichawi walikubaliana kuwa mtu aliyeshika nafasi ya Uwaziri Mkuu asifanikiwe kuwa Rais wa JMT, inaweza kuwa na mashiko?

3. Kwa mujibu wa simulizi yake, Makweta ndiye aliyekusudiwa na Mungu awe Rais wa JMT 1995. Unafikiri Makweta angefanya vizuri kumzidi Mkapa?

4. Japo masimulizi yake hayawezi kuthibitishwa Kisayansi, unafikiri nguvu za giza zina nafasi kwenye utawala wa Tanzania?

Hapo chini ni moja ya shuhuda zake

Part 14 inaelezea chimbuko la mbio za mwenge Tanzania, na part 15 inahusiana na zindiko la Lindi

Part 16 ni mwendelezo wa masimulizi ya tambiko la Lindi
Inaelekea huu upole wa WaTz ni kazi ya nguvu za giza! Yaani hadi chaguo la Mungu wamelishinda? Je huyo mtu ccm? Naona wanaifaidisha ccm tu na wezi wake.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom