Ushuhuda Kwa tuliowahi kupata mauza uza kwenye maisha

Kabla sijaleta stori yangu, kila ambaye mtu wake wa karibu (mke/Mme/ndugu/rafiki/mfanyakazi) ambaye huwa unamsaidia Mambo mengi kuanzia ushauri fedha na kumwambia Siri zako nyingi za maisha kama mipango yako ya maendeleo kama kununua Kiwanja/ gari/ nyumba kupata kazi na baadae kukugeuka Kwa kukufanyia madhilla Kwa kwenda Kwa mganga au kufanyia uchawi ili kuugua magonjwa ya ajabu kama ukichaa, uvimbe, kufukuzwa kazi, kufilisika, kupata ajali, kuibiwa, kuunguliwa na nyumba/gari, tupeane ushuhuda ulichomokaje kwenye Hilo jaribu na kama unaendeleza nalo ni hatua zipi umeshachukua na unaendeleza kuchukua.

True story kuna rafiki yangu alikuwa na kazi nzuri kwenye ofisi za madini , alikuwa akipata hela sana na kuweza kusapoti ndugu jamaa na marafiki, Ila baada ya muda alipata ugonjwa uliomsababishia akashindwa kufanya kazi kabisa, baada ya hapo kaachishwa kazi akaanza kuhudhuria sehemu mbalimbali za maombi hapa Tanzania kwa muda wa kama miezi sita Ila hakupata majibu.

Baadae akapata nafasi kwenda Kwa nabii mmoja nje akapona na kuambiwa akirudi Tanzania akazane na maombi maana huko urudipo utapata Vita kubwa sana kama hutosimama, baada ya hapo akarudi akaanza tafuta sehemu ambayo ni ya kiroho akaanza kuwa anaomba kweli kweli, Hana kazi na mume Hana kazi wanakomaa wote anaitwa kwenye usaili kwenye taasisi kubwa ikifikia wakati wakumaliza dili anaachwa, siku Moja yupo kwenye maombi makali akasikia sauti inamwambia mfanyakazi wa ndani, ikabidi ibada inayofuata aende na mfanya kazi wake kanisani, anafika Tu muda wa maombi mfanyakazi kaanza kufunguka.

Mimi ndo ninatumiwa na rafiki yako kuhakikisha hupati kazi, ndo tulikuwekea ugonjwa Ila tokea umetoka nje unaomba sana hatukuwezi, hata kazi ukiomba tunajua ila tunazuia usipate kwani tunateka fikra za waajiri kila inapotokea unataka kusaini dili tunazuia, mwisho WA siku akawa amefunguliwa na mfanyakazi akafunguliwa rafiki anaogopa kumtafuta, maisha yamerudi vizuri anapata madili ya maana, usafiri anao tayari na wote na Mme wake Kwa SASA Wana kazi na maisha yanaenda vizuri.

Stori yangu inakuja Karibuni Kwa ushuhuda wa jinsi ulivyoweza ruka viunzi na hatua ulizochukua kuweza kushinda Mambo ambayo hayaeleweki kwenye maisha.

Nilichojifunza mpaka sasa usijiweke karibu na watu wanaweza kujua mipango yako na njia zako za maisha kumbuka hii ni Africa, (Africa ni sehemu pekee MTU anaweza kutaka kuomba mkopo ili ajue mashambulizi ya uchumi wako yanafika?, Au anakupgia simu kukujulia Hali ajue ugonjwa aliokutumia umeupata?)
Mkuu asante sana.nitumie number inbox nitashukuru sana.
 
Haya mambo mpaka yakukute ndo utaelewa matomaso ni wengi, lengo ni kuelimishana...

Mtoa mada nimekuelewa, ila haya mambo yako complex, unamaanisha watu wote hapa duniani, waliokosa kazi baada ya kumaliza chuo, ni kwamba hao wote wamelogwa wasipate kazi, au ni kwamba nafasi za kazi zilizopo ni chache lakini wahitimu ni wengi Manifestation
 
Sio wote Mkuu, Ila wapo ambao fahamu zao zinashikwa wanakuwa hawana mudi ya kutafuta kazi na ni msomi mzuri tu, au unapata kazi misukosuko inakuja usiyoelewa, nk
 
Kuna mambo huwa yananitatiza. Wengi wananishauri kwamba mara nyingi mipango yangu ya maendeleo niifanye siri,hata kwa rafiki zangu. Sasa nitajuaje changamoto za hiyo mipango? Mimi naona kama nikiwashirikisha kama wanaweza ongezea input fulani.
Chagua rafiki zako Kwa busara, unaweza ukashangaa Una rafiki ambao hawana input zozote kwako, zaidi ya kupiga majungu na kukutumia kwelikweli
 
Bila shaka hujaelewa maana ya mstari huo niliotoa.

By the way, hakuna sehemu ambapo huo mstari umesema hatutapatwa na mabaya, ila unasema Yesu alishatupatia amri juu ya mabaya. Ukitaka yakutawale ni uchaguzi wako.
Sawa Mkuu, Imani yako ni nzuri Ila yakiamua kukufuata kama hujasimama utaomba po mwenyewe, changamoto ya watu wengi tunamichanganyo sana
 
Kweli ukiwaza nje ya box ni kama huu ushauri unaotolewa na hawa watu ni kama lengo ni kuwatenga watu na kuondoa ushirikiano miongoni mwao
Endelea kukumbatia watu, Ila chagua watu Kwa busara, sikiliza sana nafsi yako inakushahuri kabla hujapeleka Kwa watu, watu ni hatari kuliko unavyodhani iko siku utakumbuka hili...Ila pia watu wanaweza kuletea faida n kuwa nao makini tu
 
Walokole ndio binadamu wana maisha magumu sana, walokole ndio makazi ya stress, mtu akiokoka anatenganishwa na kila mtu eti ni watu wabaya, mlokole anasikiliza zaidi mchungaji kuliko baba, mama, au mke/mume wake
Wanajazwa mawazo ya ajabu ajabu sana

Tutawasaidia tu na wakitudhuru tutapambana nao, hatuwezi kuishi kwa kujitenga kwa hofu ya kurogwa
 
Kabla sijaleta stori yangu, kila ambaye mtu wake wa karibu (mke/Mme/ndugu/rafiki/mfanyakazi) ambaye huwa unamsaidia Mambo mengi kuanzia ushauri fedha na kumwambia Siri zako nyingi za maisha kama mipango yako ya maendeleo kama kununua Kiwanja/ gari/ nyumba kupata kazi na baadae kukugeuka Kwa kukufanyia madhilla Kwa kwenda Kwa mganga au kufanyia uchawi ili kuugua magonjwa ya ajabu kama ukichaa, uvimbe, kufukuzwa kazi, kufilisika, kupata ajali, kuibiwa, kuunguliwa na nyumba/gari, tupeane ushuhuda ulichomokaje kwenye Hilo jaribu na kama unaendeleza nalo ni hatua zipi umeshachukua na unaendeleza kuchukua.

True story kuna rafiki yangu alikuwa na kazi nzuri kwenye ofisi za madini , alikuwa akipata hela sana na kuweza kusapoti ndugu jamaa na marafiki, Ila baada ya muda alipata ugonjwa uliomsababishia akashindwa kufanya kazi kabisa, baada ya hapo kaachishwa kazi akaanza kuhudhuria sehemu mbalimbali za maombi hapa Tanzania kwa muda wa kama miezi sita Ila hakupata majibu.

Baadae akapata nafasi kwenda Kwa nabii mmoja nje akapona na kuambiwa akirudi Tanzania akazane na maombi maana huko urudipo utapata Vita kubwa sana kama hutosimama, baada ya hapo akarudi akaanza tafuta sehemu ambayo ni ya kiroho akaanza kuwa anaomba kweli kweli, Hana kazi na mume Hana kazi wanakomaa wote anaitwa kwenye usaili kwenye taasisi kubwa ikifikia wakati wakumaliza dili anaachwa, siku Moja yupo kwenye maombi makali akasikia sauti inamwambia mfanyakazi wa ndani, ikabidi ibada inayofuata aende na mfanya kazi wake kanisani, anafika Tu muda wa maombi mfanyakazi kaanza kufunguka.

Mimi ndo ninatumiwa na rafiki yako kuhakikisha hupati kazi, ndo tulikuwekea ugonjwa Ila tokea umetoka nje unaomba sana hatukuwezi, hata kazi ukiomba tunajua ila tunazuia usipate kwani tunateka fikra za waajiri kila inapotokea unataka kusaini dili tunazuia, mwisho WA siku akawa amefunguliwa na mfanyakazi akafunguliwa rafiki anaogopa kumtafuta, maisha yamerudi vizuri anapata madili ya maana, usafiri anao tayari na wote na Mme wake Kwa SASA Wana kazi na maisha yanaenda vizuri.

Stori yangu inakuja Karibuni Kwa ushuhuda wa jinsi ulivyoweza ruka viunzi na hatua ulizochukua kuweza kushinda Mambo ambayo hayaeleweki kwenye maisha.

Nilichojifunza mpaka sasa usijiweke karibu na watu wanaweza kujua mipango yako na njia zako za maisha kumbuka hii ni Africa, (Africa ni sehemu pekee MTU anaweza kutaka kuomba mkopo ili ajue mashambulizi ya uchumi wako yanafika?, Au anakupgia simu kukujulia Hali ajue ugonjwa aliokutumia umeupata?)
Sahihi kabisa
 
Back
Top Bottom