Pole sana mkuu hapo kwa mama,
Yote hayo sababu ya malezi hata hiyo iliyokuwa sifa yako kubwa, na Waafrica tunadhani kupiga ndio malezi japo sio kweli,
Huwa naumia sana pale mzazi/au mtu yoyote anapompiga/tukana mtoto akidhani anarekebisha kumbe anaharibu bila kujua huku akipandikiza/kutengeneza kitu ambacho ni sawasawa na timebomb au nyoka aliyekatwa mkia,
Ninachoamini maneno/(malezi) ni silaha nzuri ukiitumia vizuri, pia ni silaha mbaya ukiitumia vibaya,
Binafsi naamini kwamba, binadamu ni kiumbe/mnyama aliyebarikiwa vingi, kimoja wapo ni akili/uelewa mpana sana ambao ndio unaendesha kila kitu katika maisha ya binadamu, tofauti na wanyama wengine,
Na ninachojua binadamu anapozaliwa uelewa/akili yake inakua haina chochote,
Ni sawasawa na shamba ambalo halijalimwa chochote ila utakachopanada ndio hicho,hicho kitakachoota/utakachovuna
Na hicho ndio kinachonifanya mimi niamini kwamba maneno/(malezi) ni kitu chenye nguvu sana katika maisha mwanadamu, maneno(malezi) yanaweza kupita moja kwa moja mpaka kwenye akili/uelewa wa mtoto ambapo ndipo panaongoza kila kitu katika maisha ya huyo mtoto,
Hivyo mtoto anapofanya kitu ambacho mzazi hakubaliani nacho,
hilo ni kosa la mzazi sababu yeye ndicho alichopanda, na anapompiga ndivyo anavyozidi kubomoa, ataishia kupiga mwili tu na sio kubadirisha nafsi yake, Ila kama angepanda mahindi sidhani kama zisingeota bangi.
Kiufupi Mama yenu aliwakosea sana.
Huu ni Muono wangu.
Naona faida ya malezi haya niliyoandika
Hata niwajengee nyumba angani bado haitowatosha.