Ushuhuda: Manukato/perfume yasababisha niachwe na mwanamke aliyenipenda

Ushuhuda: Manukato/perfume yasababisha niachwe na mwanamke aliyenipenda

Morg

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2018
Posts
1,301
Reaction score
1,788
Habarini za asubuhi bandugu zanguni hapa katika jukwaa poleni na mvua za Jana haswa maeneo ya jiji la Dar es salaam twende kwenye mada.

Jana ndio siku rasmi niliyoachwa na mwanamke aliyenipenda sana hakika haikuwa siku nzuri sana kwangu mpaka sasa nimehuzunika sana. Ilikuwa ni hivi kuna binti mmoja polite sana mkarimu anajitambua alitokea kunipenda sana tukiwa kwenye relationship kama Two months hivi.

Katika maisha yetu ya uhusiano kwa kipindi hicho cha muda mfupi tulikuwa wenye furaha tabasamu na upendo sana katika hili siku zote nitakumbuka sana .Chanzo cha mvurugano huyu binti alikuwa na mdogo wa shangazi yake walikuwa wamepanga Pamoja sehemu moja, haka kadogo mtu naye alikuwa kashatokea kunipenda sana na yeye hadi kukawa na vita ya Dada mtu na mdogo mtu full kununiana.

Jinsi pafyum ilivyosababisha nikaachwa huyu mdogo mtu akiniomba nionane nae kama mkosi na mimi nikafanya hivyo bila hiyana tukakutana akaniomba nimsindikize mahali nikafanya tukawa tunarole pamoja kama wapenzi hivi . Kumbuka hapo kabla nilimuuliza dada yako yupo wapi akaniambia yupo anapika nyumbani kumbe niliuzwa baada ya kuagana full kukumbatia na kukisiana kumbe nilimwachia harufu ya pafyum ambayo dada mtu ambae ni mpenzi wangu anaitambua vilivyo fika hata upite hatua kumi mbeleni anaisikia.

Kufika ndani akamkuta dada yake anapika sindio kusikia harufu ya pafyum yangu hapo hapo simu ikapigwa ulikuwa wapi na nani nikapinga vilivyo kanibana mpaka kuchukua simu ya dogo na kuanza kupekua na kukuta madudu yote hakika niliishiwa pozi kabisa Jana akaniambia mlikuwa wapi na mmekumbatiana na flani nikajibaragua wee lakini wapi finally kwa majonzi makubwa nikaachwa kuanzia leo mimi na wewe hatujuani. Kiukweli niliumia na nakiri mimi namakosa makubwa.

Wakuu naomba ushauri hapa jukwaani tafadhali nifanye nini ili nimrudishe huyu mwanadada kama mwanzo nitumie njia gani .Najua humu kuna wajumvi sana na watanishauri vyema.

Nawakatia ijumaa njema nyote.

1619777130535.png

 
Mkuuu utafute kazi nakushauri,acha kazi yako ya kubeti utaweza kuishi na mwanamke
 
Jamaaa kazingua kinoma, yani unafanya vitu kama uko secondary tatzo kubwa hapo ni tamaa zako tu maana ukiachilia mbali hyo perfume bado kuna ushahidi mwingine wa madudu yako kwenye simu ya dogo,,. Kwan mapenzi yenyewe yanasemaje?
 
Wavurana mna shida sana, mwanaume hata akutwe kifuani akipewa nafasi ya kushuka tu basi ujue aliekua kifuani sio yeye. Sasa wavurana issue ndogo unakuja kulialia hapa
Mkuu ebu nishauri namna ya kusolve hii ishu ushakuwa big deal
 
Sasa si uendelee na mdogo wake??

Au dogo naye kadengua?? Ilaumu tamaa yako, perfume unaisingizia bure tu..
Dogo kajaa kinouma yaani hasikii wala haelewi kitu juu yangu
 
Back
Top Bottom