Ushuhuda: Mlo mmoja kwa siku ndiyo mpango wa Maisha. Prof. Janabi yuko sahihi

Prakatatumba abaabaabaa

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
2,317
Reaction score
7,808
Nilishtuka baada ya Kila mtu kuniambia nimenenepa sana, ikabidi niende kupima uzito, sukari, pressure n.k Kwasababu nilikua nikitembea kidogo nachoka, na mapigo ya moyo yanadunda kwelikweli.

Kufika hospital daktari akanipima uzito nikawa na 94kg, sukari ikasoma 5.5 mmol/l kabla sijala, pressure ikasoma 150/92 mmHg, daktari akaniambia sio mbaya lakini nikiendelea na mtindo huu itakua mbaya ukizingatia umri Bado Niko kwenye 30's.

Ikabidi nianze kukagua na kuangalia ninapokosea, nilikua mtu wa kula hovyo hovyo, juice ya miwa litre 1, nagonga karibu kila siku, juice ya embe, soda, chips,wali, maharage, karanga, naweza kununua ndizi 10/5 na nikala zote kwa wakati mmoja,

Ikabidi nianze kuchukua jukumu la kukata sukari pamoja na wanga, na nimejipa jukumu la kupunguza kilo mpaka 75kg, alafu ndio ni maintain hapo hapo.

Ikabidi niingie mtandaoni nikakutana na mbinu mbali mbali,
1. Intermittent fasting: 16:8 au 18:6, yaani unakula ndani ya masaa 8( window period) na unafunga masaa 16, profs janabi ndio huwa anaiongelea sana, mfano unafungua kinywa saa 6/8 mchana then mlo mwingine unakula kabla ya saa 2 usiku, then unauacha mwili ukae kwa masaa 16,...ili Mwili utumie mafuta kama source of energy..

2. OMAD: yaani one meal a day, unachagua kula mara moja kwa siku mfano, unakula saa 12, then mpaka kesho saa 12, vyakula vya kula hapa ni, nyama,protein, mboga za majani, viazi vitamu, tango, parachichi, wataalamu wanasema ivi ni vyakula ambavyo havipandishi sukari kwenye damu sukari ya haraka.

3. Warrior fasting: hii sikushauri maana ni ngumu balaa, lakini ni njia nzuri kwa matibabu, ya cancer, sukari, n.k yaani unafanya fasting ya maji tu, maji unachanganya na chumvi ya mawe kidogo (wanasema electrolyte )...

Mimi nikaenda na hiyo no 2, yaani OMAD, nimepanga niifanye ndani ya mwezi then niingie kwenye intermittent fasting ya 16:8, wakuu Leo ni siku ya 10 tokea nimeanza, nikasema niende kupima uzito maana nguo naona zilianza kuachia..

Kufika uzito nikawa na 89kg, yaani nimepunguza kilo 5, sukari ikasoma 4.9mmol/l ambayo ni normal zaidi, pressure ikasoma 136/84 lengo langu isome 120/80..

Nimekua surprised sana, nimekua sisikii njaa hovyo, nimekua na energy wakati mwingine nilikua naona kama ninaweza kukaa hata masaa 48 (siku mbili kula)..

Nilikua mtu mwenye kusita kufanya maamuzi, nikiwa na jambo huwa na overthink sana, na kutanguliza uoga mbele na kulipuuzia, sasaivi sioni ambacho kitakachonizuia kufanya kitu, nimekua focused zaidi...

Bado Niko naendelea,..chagua njia yako ambayo ni sahii ishi nayo, Nimegundua njaa tunayoisikiaga mara nyingi Huwa ni fake, ukinywa maji utaona kabisa njaa inaondoka, ukisikia kiu ya soda piga maji...

Kula kula inasababisha insulin spike kubwa kinoma, watalamu wanasema unapokula hovyohovyo, KONGOSHO INATOA HORMONE YA INSULIN KUSHUSHA KIWANGO CHA SUKARI, HUJATULIA UNAGONGA TENA CHAPATI, INSULIN INASHUSHA SUKARI, HUJATULIA UNAGONGA WALI SAHANI NZIMA, mtu kama Poor Brain , siku nzima kongosho inafanya kazi kushusha msosi aliopiga, ..akitembea kidogo juice ya miwa, akikaa mandazi na soda, korosho zikipita anaruka nazo, watembeza barafu wakipita yumo, supu ya pweza na kachori yumo, hapo unakuta tokea asubuhi mpaka usiku, kongosho inatumikishwa kinoma, hapo ndio mtu anaingia katika stage ya pre- diabetic
 
Na kingine wakuu, kabla ya mlo hakikisha kuna mboga za majani za kutosha, pamoja na avocado, au protein wanasema wataalamu hizi ni fibre ambazo hazisababishi insulin spike kubwa, glucose inafyonzwa kwenye damu pole pole, hata kama mlo wako pendwa ni wali maharage kama Mimi, hakikisha kunakua na mboga za majani, avocado, then ushushie huo wali, hapo utakua umeupa wali fibre, kwahiyo haitasababisha insulin spike kubwa.
Maamuzi ni yako.
 
Nikipiga machungwa yangu fresh km 10 au 12 yalijaa maji ya kutosha saa 8 hio napiga tena menu usiku kabla ya saa 2, usiulize kwanini machungwa katika matunda nayapenda ni machungwa zaidi na machungwa yale yaliyolala km siku 2 au 3 hivi yanakua na ladha fulani ya kipekee sio yaliyochumwa mtini siku hio hio
 
OMAD(one meal a day) ni kwa ajili ya kusaidia mwili kutumia mafuta ya ziada kwenye mwili kama nishati hivo mafuta huchomwa kupatikana nishati nguvu

however hii sio ya kufanya kila sku kwan unadhoofisha mwili, Janabi yeye anafanya 2 meals a day ila anaongeza na mazoezi which is the best
 
Insulin spike kubwa kinoma, watalamu wanasema unapokula hovyohovyo, KONGOSHO INATOA HORMONE YA INSULIN KUSHUSHA KIWANGO CHA SUKARI, HUJATULIA UNAGONGA TENA CHAPATI, INSULIN INASHUSHA SUKARI, HUJATULIA UNAGONGA WALI SAHANI NZIMA, ...unakuta siku nzima hormone ya insulin Iko juu kazi yake ni kushusha takataka ambazo tumeziwekea, inafika kipindi, kinatokea kitu kinaitwa insulin resistance yaani, yaani insulin unayoitoa haishushi kabisa sukari yako, hapo ndio mtu anaingia kwenye pre diabetic.
 
Europe na ,marekane usually wanagonga 4 mnyuz na bado wana afya njema. Miaka ya nyuma walifikiri obesity ni laana kwao lakini walipogundua umuhimu wa mazoezi na kuzingatia balanced diety milo minne ni kawaida kwao.
1. Heavy breakfast before saa moja asubuhi.
2. Light breakfast saa 4 asubuhi
3. Launch saa saba mpka nane mchana.
4. Dinner/supper saa moja mpaka 3 usiku.

Kinachozingatiwa ni kula na ku-burn calories through mazoezi
 
Vipi ku
Vipi kuhusu vidonda vya tumbo maana chanzo cha hii shida ni tumbo kuwa empty kwa mda mrefu, hii imekaaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…