Ushuhuda mwanaume mwenzenu: Nilioa Single Mother yalioyonikuta ni haya. Nilichukua uamuzi huu.

Wewe umeshaoa?
 
Sisi tuliowahi kuishi na single mother hata hatushangai hayo, ila ngoja single mothers wa humu jf wanavyowehuka kujitetea 😂
 
Kuna single mothers kadhaa wanakuja kwangu kwa kasi ya SGR, mimi moyoni mwangu najisemea tu, hamnipati.

Kuoa SINGLE mother hasa kwa zama hizi ni hatari sana.
 
Nimeusoma ushuhuda wako. Kwa kweli somo kubwa hapa si kwamba single mother wote wako hivi, bali ni umuhimu wa uwazi, mipaka na heshima ndani ya mahusiano.

Kuwa na mtoto si tatizo, lakini mzazi mwenza wa zamani akiendelea kuingilia ndoa bila mipaka na mwenzi wako kushindwa kuweka wazi nafasi yako, hapo migogoro ni rahisi kutokea.

Pia upande wako, kupiga mwenzi wako haikuwa sahihi, hata kama ulikuwa na hasira kiasi gani. Mwisho wa yote, inaonekana uhusiano ulikuwa tayari umeshajaa majeraha, kutokuaminiana na mawasiliano mabovu.

Somo kwa wanaume na wanawake: usiingie kwenye ndoa ukidhani utabadilisha historia ya mtu; elewana mapema kuhusu watoto, wazazi wenza, mawasiliano na mipaka. Kila mtu anastahili kuheshimiwa kwenye nafasi yake.

Pole kwa yote uliyopitia, lakini tusihukumu kundi zima la single mothers kwa kisa cha mtu mmoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…