USHUHUDA: Nilivyonusurika kufa kwa kujirusha Jengo la Mwanjonde, Malimbe Cumpus

USHUHUDA: Nilivyonusurika kufa kwa kujirusha Jengo la Mwanjonde, Malimbe Cumpus

2 of Amerikaz most wanted

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2023
Posts
1,328
Reaction score
3,718
Ni miaka kadhaa imepita baada ya kunusurika kujitoa uhai wangu.

Chanzo cha hayo yote ni maisha duni Niliyoyapitia kipindi nipo pale cumpus, nilikuwa naipambania Diploma yangu ya kwanza.

Sasa baada ya kukosa msaada home yani kama nilisuswa hivi hasa ikanibidi niingie mtaani kusebenza nipate chochote kitu na hapo ikumbukwe nadaiwa kodi ya chumba pia college fees Sina.

Nikawa napita chumba by chumba kukusanya nguo chafu na kuziosha ili nipate ujira, sema sikutoboa msoto ulikuwa heavy ikapelekea mpaka kunijia wazo la kujiua.

Ili niepukane na kikombe cha msoto nikachagua njia mbili ya kwanza ni kwenda kujitupa ziwa Victoria na la pili ni Kujirusha Jengo La Mwanjonde pale Malimbe. Sema nikaona Kufa maji uongo, Nikaona bora nikajirushe kwa gorofa.

Bwana wewe nikatoka zangu ghetto boy mida asubuhi moja kwa moja mpaka Mwanjonde hadi floor ya mwsho tayari kwaajiri ya zoezi, lakini punde si punde baada ya kutana chini ile distance nilinyong'onyesha kila kitu na kuna kisauti kikawa kina "niaambia mkushi unaenda kuwa chapati dakika kadhaa".

Nikaona sio kweli nikasitisha zoezi na kuapa ya kwamba nitapambana na Hali yoyote ila sio kujiua.

Najiuliza hivi hawa wenzetu wanaokatika uhai wao Wanakuwa na ujasiri wa aje?🤔

NB: kujiua ni Unyonge kataa Unyonge

_20230525_181444.JPG
 
Ni simple sana wewe piga zako konyagi kubwa 1 changanya na safari kubwa 2 afu nenda pale mdogomdgo mbona unajirusha kama kitenesi tu
 
Kuna wengine matarajio yao huwa hayatimii na wanajikuta wamekuwa walemavu ..
 
Ni sup za papaa mulongo zilikushinda au ni maisha tu yalikuwa magumu?
( Build the city of God)
 
Mwanza unakosaje hela ya kula,, nyie watoto mchele mchele nini,,
 
Hua hawafanyi hvoo mkuu, wenzio wanjirusha tu bila kutizama chini.

Nikama anajirusha swimming Ili adive ila hii inakua Aerialdiving.

Kabla hajafika chini Kuna ka flavor unapata japo sekunde kadhaa unageuka ujii.

Swali la kujiuliza ukipona ila ukajikuta umevunjika MIGUU utajutia au laa.
 
Ni miaka kadhaa imepita baada ya kunusurika kujitoa uhai wangu.
Chanzo cha hayo yote ni maisha duni Niliyo yapitia kipindi nipo pale cumpus, nilikuwa nai pambania Diploma yangu ya kwanza...

Duuu
 
Uwa naamini nijia nzuri ya kujiua ni kufumua bichwa kwa risasi.
 
Back
Top Bottom