Ushuhuda: Tunaposema Shetani hana rafiki hatudanganyi

Ushuhuda: Tunaposema Shetani hana rafiki hatudanganyi

Halafu 9th December 2019 Zitto anasusia huku CDM wakienda kujipendekeza CCM Kirumba kutaka urafiki na shetani aliyetoka "kuvuruga" uchaguzi wa serikali za mtaa.

Wote ni walewale tu tofauti ni rangi ya "matambara" mnayopeperusha!

Mnalalamika hakuna Uhuru halafu mnaenda kusherekea siku ya Uhuru upi?
Una maono mapana sana bro

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hii biashara mpya ya chama tawala kupanga mikakatii na kutenga fedha za kuwahadaa na hatimaye kuwanunua viongozi kutoka vyama vikuu vya upinzani ni jambo la kuogofya sana.

Na tena uamuzi huu kufanyika kupitia ajenda zinazopitishwa ndani ya Sekretariate ya Kamati Kuu ya chama. Kweli! Hivi inaingia akilini kabisa watu wenye dhamana ya kuiendesha nchi yetu kujifungia ktk kuta nne, tena chini ulinzi mkali ili kupitisha uamuzi kama huu!

Hivi kweli vituko na vioja hivi vinafanyika hata ktk nchi nyingine makini? Kuna kila haja ya kupima afya ya akili za viongozi wetu ambao wanaweza kuaminika kubeba jukumu kubwa lenye kutuhakikishia hatma ya mamilioni ya Watanzania.

Isije ikawa tuna idadi kubwa ya wadau wa hospitali ya Milembe ambao kwa makosa tumeweza kuwabebesha jukumu ambalo ambalo si lao, na kamwe hawataweza kulibeba, na kuishia kuendelea kutufanyia vituko na vioja kutokana na woga wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii siasa ya kununua wapinzani huko nchini kwetu tunaita punieto ya kisiasa sijui hapa Bongo mnaitaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu 9th December 2019 Zitto anasusia huku CDM wakienda kujipendekeza CCM Kirumba kutaka urafiki na shetani aliyetoka "kuvuruga" uchaguzi wa serikali za mtaa.

Wote ni walewale tu tofauti ni rangi ya "matambara" mnayopeperusha!

Mnalalamika hakuna Uhuru halafu mnaenda kusherekea siku ya Uhuru upi?
Tarehe 9 December Chadema walienda ku deliver message.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpeni salaam, habari zake tunazo. Nyumba yake imebomoka atalala wapi
Serikali imepata maficho. Uzuri wake akili za watanzania wengi ni kama za mnyama ngiri. Anapowindwa akakimbia na kumuacha tuseme mbwa, hujisahau na kuanza kula nyasi.
Ndivyo watanzania tulivyo wasahaulifu:
° mivutano ya nchi yetu ilianza mara tu baada ya uchaguzi mkuu,
° ZK ana uwezo gani wa kusababisha tunyimwe mikopo,
° uongo gani aliosema ZK? na
° viongozi wakuu ws nchi wanajichanya:
- mara mabeberu, mara wafadhili,
- tunajenga miradi kwa pesa zetu,
- Tanzania ni nchi tajiri, nk.
 
MSISAHAU Lowasa alikuwa adui na fisadi namba moja kwenye ORODHA YA CHADEMA. Lakini ghafla akaaminiwa akapewa unahodha wa chama na akasifiwa sana "rais wa watu " Leo yuko wapi? The only thing that is constant is change!
 
Halafu 9th December 2019 Zitto anasusia huku CDM wakienda kujipendekeza CCM Kirumba kutaka urafiki na shetani aliyetoka "kuvuruga" uchaguzi wa serikali za mtaa.

Wote ni walewale tu tofauti ni rangi ya "matambara" mnayopeperusha!

Mnalalamika hakuna Uhuru halafu mnaenda kusherekea siku ya Uhuru upi?
Mkuu 'Karne', kama sio kupotosha kwa maksudi, wewe utakuwa umetafsiri vibaya maana nzima ya uwepo wa CHADEMA kwenye sherehe hizo.

Hizo sherehe sio za CCM, ni sherehe za Tanzania. CHADEMA hawawezi hata siku moja wakaigomea Tanzania.

Licha ya hilo, na hasa kama unaona gumu kwako kulielewa; CHADEMA waliitumia vizuri sana fursa hiyo kufikisha ujumbe mhimu kwa waTanzania.

Kama wewe hukuelewa ujumbe uliowasilishwa ni bora ukaomba uelezwe na walioelewa ujumbe huo.

CHADEMA hawakuhudhuria sherehe zile kuwaunga mkono CCM kwa aina yoyote ile. Huo ndio ujumbe mhimu kwako uuelewe; pamoja na kwamba mimi sio msemaji wao.
 
Kwa hii biashara mpya ya chama tawala kupanga mikakatii na kutenga fedha za kuwahadaa na hatimaye kuwanunua viongozi kutoka vyama vikuu vya upinzani ni jambo la kuogofya sana.

Na tena uamuzi huu kufanyika kupitia ajenda zinazopitishwa ndani ya Sekretariate ya Kamati Kuu ya chama. Kweli! Hivi inaingia akilini kabisa watu wenye dhamana ya kuiendesha nchi yetu kujifungia ktk kuta nne, tena chini ulinzi mkali ili kupitisha uamuzi kama huu!

Hivi kweli vituko na vioja hivi vinafanyika hata ktk nchi nyingine makini? Kuna kila haja ya kupima afya ya akili za viongozi wetu ambao wanaweza kuaminika kubeba jukumu kubwa lenye kutuhakikishia hatma ya mamilioni ya Watanzania.

Isije ikawa tuna idadi kubwa ya wadau wa hospitali ya Milembe ambao kwa makosa tumeweza kuwabebesha jukumu ambalo ambalo si lao, na kamwe hawataweza kulibeba, na kuishia kuendelea kutufanyia vituko na vioja kutokana na woga wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu ni maamuzi ya Baraza la mawazili na sio tu unapewa pesa untishwa pia ukikataa utauwawa. Sasa hata kama ni mimi bora nipokee hizo pesa na niokoe uhai wangu.
 
Halafu 9th December 2019 Zitto anasusia huku CDM wakienda kujipendekeza CCM Kirumba kutaka urafiki na shetani aliyetoka "kuvuruga" uchaguzi wa serikali za mtaa.

Wote ni walewale tu tofauti ni rangi ya "matambara" mnayopeperusha!

Mnalalamika hakuna Uhuru halafu mnaenda kusherekea siku ya Uhuru upi?
Sio kweli, CDM walikuwa kimkakati pale CCM Kirumba, dunia iliona na wenye akili waliona!
 
Wakuu mtanisamehe sana kwa kuwarudisha nyuma mwaka 2015 kwenye uzinduzi wa bunge Jipya baada ya Uchaguzi Mkuu ambayo ilikuwa ndio siku ya kwanza kabisa kwa Rais mpya kulihutubia bunge hilo jipya na kulizindua.

Wabunge wote wa Upinzani waliotokana na (UKAWA) walitoka nje kama ishara ya kupinga kuingia ndani ya bunge hilo kwa Dr Shein ambaye aliangushwa kwenye uchaguzi ule na Jabali Maalim Seif na baadaye uchaguzi kufutwa.

Mpinzani pekee aliyebaki ndani ya bunge lile ambalo lilikuwa haramu baada ya kumuingiza Dr Shein kwa cheo cha Rais wa Zanzibar huku akiwa kaangushwa alikuwa Zitto Kabwe. Rais mpya kwenye Hotuba yake akamsifia sana Mh Zitto na kuwaponda wapinzani wote kwa mamia waliomsusia.

Si lengo langu kwa leo kumjadili Zitto Kabwe , maana yaliyopita si ndwele lengo langu ni kuushuhudia msemo wa kweli wa wahenga usemao kwamba " Shetani hana rafiki "

Zitto Kabwe ambaye kwa wakati ule aliunga mkono CCM bungeni , leo CCM ileile aliyoiunga mkono inaitisha kikao ili pamoja na mambo mengine itenge fedha kwa lengo la kuwanunua madiwani wote wa ACT WAZALENDO popote walipo nchini Tanzania , leo wale aliowaunga mkono wamemgeuka ! pamoja na kumpoteza Kanguye lakini bado hawajatosheka , wanamuwinda yeye mwenyewe kama digidigi!

Kwahiyo, kuanzia sasa ni vema maandiko tunayoyaweka humu yasipuuzwe , Shetani ama wakala wake hapaswi kuungwa mkono imeandikwa kwenye vitabu vyote vya dini , haya yanayoendelea nchini Tanzania ni mipango ya Mwenyezi Mungu kuwathibitisha walimwengu kwamba Neno lake liko hai na linaishi.
Mkuu! Hapa ndo huwa sipati jawabu ni kwanini Maalim Seif akajiunga na ACT Wazalendo ambayo kiongozi wake mkuu ni Zitto. Naomba tafakuri ya kina.
 
Kama ni kweli, mpango huu upo na unafanyika ndani ya chama cha CCM, chama hiki na viongozi wake wote watakuwa wapapambanaji wa rushwa?

Hili tu ndilo swali mhimu kwangu, na pengine wengi wengine.

Jambo hili pia tunaweza tukalipeleka mbele zaidi ya hapo; kwamba, akitokea mwanachama/kiongozi huko upinzani akawa hanunuliki kwa bei yoyote, na nafasi yake ikaonekana ni tishio kwa chama hiki cha CCM, itakuwa ni ruhusa kumwondosha kwa njia yoyote hata mauti?
Hii ndio tafsiri pekee inayoweza ikafanyika katika hali ya namna hii.
Nina hofu hata kwa yule meya wa dar huenda jamaaa alikataa kununulika,nnapata hofu huenda pia akawa katikati ya manati
 
Kingine cha kujifunza ni "maskini haaminiki lakini mwanasiasa haaminiki zaidi"... Zito naye alibaki bungeni akichekelea Seif kupokwa ushindi saiv wako pamoja baadae utaskia mengine !!
 
Mkuu! Hapa ndo huwa sipati jawabu ni kwanini Maalim Seif akajiunga na ACT Wazalendo ambayo kiongozi wake mkuu ni Zitto. Naomba tafakuri ya kina.
nimeomba tangu mapema kwamba tusimjadili Zitto , tujadili hoja ya kwamba SHETANI HANA RAFIKI
 
Back
Top Bottom