Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 12,675
- 25,924
- Thread starter
-
- #41
kuna watu wengi sana wanakuja DM wanaandika msg wakielezea matatizo yao na wanataka niwape pesa. Ninajua ni kweli mnaweza kuwa kwenye matatizo, lakini hamtakiwi kuniomba mimi, mwombe Mungu huyo ndiye anaweza kutatua tatizo lako jumla. mwanadamu hawezi kukusaidia. hata mimi nitakusaidia kama nikiguswa na Mungu. kuna watu wengine wanapitia kwenye majangwa kwasababu Mungu anawapitisha kuwafundisha maisha ili atakapowabariki wakumbuke. au ni njia tu ya shule anawafundisha.
ila wengine wanapitia kwenye matatizo kwasababu wamegombana na Mungu na wanapata adhabu. hakuna mtu anaweza kukuokoa kutoka kwenye mkono wa Mungu kama ameamua kukushughulikia. unachotakiwa ni kutengeneza uhusiano wako na Mungu akusamehe na kukuondolea tatizo lako. kuna watu mmeua, mmezini, mmeiba na kuumiza mioyo ya watu, watu hao wamelia kwa Mungu na Mungu ameshuka kuwapambania and you think mwanadamu anaweza kukurescue toka mikononi mwa Mungu? No. cha ajabu ni kwamba, Mungu ni Mungu wa rehema, huwa anasamehe kila anayekuja kwake kutubu.
ila kwa wale wote ambao kiukweli wanapita tu kwenye jangwa, Mungu labda anawafundisha, usimwombe mwanadamu chochote. utapita kwenye jangwa hilo hadi utakapomaliza mtihani wako ndipo Mungu atakuondoa kwasababu labda Mungu ana makusudi. na pengine unapita hivyo kwasababu ameona unaweka macho yako kwa wanadamu, msaada wetu hautoki kwa wanadamu, unatoka kwa Mungu. msaaada wa mwanadamu haudumu, ila msaada toka kwa Mungu hata kama ametumia mwanadamu kukubariki unadumu na hauna majuto. jua kwamba, Mungu hubariki kwa kutumia wanadamu pia, lakini ni mpaka hao wanadamu waguswe na Mungu kufanay hivyo nandio maana utukufu unatakiwa kwenda kwa Mungu kwasababu ni yeye ametoa kwa kupitia mwanadamu. hata mimi leo hii Mungu akinielekeza kwa namna atakayojua yeye nitoe kitu, nitatoa, ila asiponielekeza siwezi.
Kama vile Musa alivyomwinua nyoka wa shaba ndivyo Mwana wa Adam alivyoinuliwa ili kila amwaminiye apate uzima wa milele. mwangalie Yesu, huyo ndiye msaada wako, ukiangalia wanadamu na kutegemea misaada toka kwa wanadamu ni dharau na tusi kwa Mungu.
katika maisha yangu nilishapita kwenye majangwa mara nyingi, kuna kipindi nilikuwa nategemea wanadamu na elimu na kazi. Mungu akaona kumbe sijamwelewa vizuri, akaweka ugumu mioyo kwa wanadamu (ndugu zangu ambao ni matajiri), nilipita kwenye tatizo ambalo hakuna mwanadamu aliyekuwa msaada, nilichekwa na kudharauliwa hadi na watoto wadogo. ndugu zangu walikuwa tayari kusaidia watu wengine ila sio mimi. wale niliowasaidia wakafanikiwa sana ndio walikuwa wakwanza kunicheka na kunitupa. hadi pale nilipoondoa macho yangu kwenye elimu, ndugu na wanadamu, nikawa nimebaki mimi na Mungu tu, nilipoangalia macho yangu kwa Mungu tu ndipo alikuja kuniokoa mazima. that was 12 years ago. nikajifunza kuwa kumbe hatutakiwi kuangalia au kutegemea msaada toka kwa wanadamu. hata hili fungu la kumi naongelea, ni kwamba nilishawahi kubarikiwa, nikawa natoa fungu, nilipokuja kusimama miaka kadhaa ndio milango ikafungwa, hadi mwishoni mwa mwaka jana na mwezi januari mwaka huu 2022 nilipoazimia kuanza. na nimejifunza kitu kwa vitendo, hakuna mtu atakuja kunidanganya tena.
nitayainua macho yangu nitazame milima, msaada wangu utatoka wapi? msaada wangu utatoka kwa Bwana, aliyeziumba mbingu na nchi, asiuache mguu wako usogezwe, asisinzie akulindaye, Bwana ndiye mlinzi wako.
mwenye kunielewa amenielewa, asiyenielewa kuna siku atautafuta ukweli huu.