Ushuhuda wa breakthrough!

Ushuhuda wa breakthrough!

Hebu tueleze ukweli kuhusu hizo pesa ambazo hujui hata zilipotokea. Je, uliziokota njiani au kuna mtu tualikupa pesa hizo au uliamka ukazikuta nyumbani kwako? Tukishapata hiyo taarifa ambayo umeificha sana katika maelezo yako, na sisi tutafuata ushauri wako.
unaweza kuwa hujanielewa, au ninaweza kuwa sijafanikiwa kufafanua vizuri, kuna namna ya kufafanua kila mtu ana kiwango cha uwezo wake. kama sikukwambia, ni kwamba, pesa hizo zimetoka kwa mtu ninayemfahamu, ambaye sikuwa namdai, ambaye sikuwa nategemea kuwa angeniwekea hizo pesa kwenye account, na yeye amesukumwa tu na Mungu aweke hizo pesa. sina cha zaidi kuongea. kwangu mimi hilo naona ni muujiza kwasababu sikustahili na haikutokea zamani. kwetu sisi watu wa kiroho, tukisema milango imefungwa tunaelewa na tukisema milango imefunguliwa tunaelewa. we feel it in our hearts, ni kama kuna mazungumzo moyoni, sio mwilini. ndivyo hivo pia hata mawasiliano yetu na Mungu huwa tunafanya wakati mwingine, hatakuja kwa sauti kubwa ila kwa sauti ya ndani utajua kila kitu kwamba hapa sio mkono wa mwanadamu, hapa huyu mwanadamu hajafanya mwenyewe, amesukumwa na Mungu. kuna watu wenye shida kuliko mimi hao watu wangewapa pesa hizo, lakini wakanipa mimi. huoni kama ni muujiza huo? na kwanini utokee sasaivi baada ya fungu la kumi? na moyoni nashuhudiwa kuwa Mungu ndio amenipa hizo pesa kupitia hao watu, na hata wao hawana explanation yeyote, wamesema wamekaa wametafakari wakaamua kufree some of the monies in their account kuweka kwangu. na ni familia iliyostaafu (though ni wastaafu wa ulaya). kama una swali lingine uliza.
 
"Siku utakapokuja kugundua kuwa ulipoteza muda sana kuamini bikira maria , it will be late for you "

Yanii hadi nimelia niliye mdogo kwake ambaye si stahili kuona hata uso wake

JE YEYE AMBAE KUPITIA YEYE AKATULETEA MWANA KONDOO AMBAE KILA AMWAMINIYE ANA UZIMA MILELE sijui ata kuwa amelipokeje neno hilo

Sent from my Infinix X559C using JamiiForums mobile app
Yesu Kristo hajaletwa na maria, Yesu Kristo alikuwepo kabla ya Maria, alikuwepo kabla ya Musa, alikuwepo kabla ya Ibrahim. acheni kuabudu mwanadamu ambaye amekufa na hajafufuka. achani kuabudu wafu. ni ajabu unasema umetetemeka kwa kuona kana kwamba nimemdharau maria, are you serious? Yesu ndiye alikufa kwa ajili yako, sio maria. soma kitabu cha isaya 53.
 
Unamtolea Mungu kwa wrong reasons, kwamba akupe vitu vya mwilini? Earthly things ndo zinakusukuma kutoa na sio kwamba unampenda Mungu? Kornelio alitoa ili apete vitu? Je dorkas alitoa sadaka nyingi na kusaidia watu ili apate faida bnafsi za dunia hii? Soma vizuri biblia yako
No, ninamtolea Mungu kwa kufuata neno lake. and its not a wrong reason. Mungu ameweka baadhi ya principles ili kupima uchoyo wa mioyo yetu, na wengi wamefeli mtihani huu. simtolei Mungu kwasababu namdai, simtolei Mungu ili kununua vitu toka kwake, simhongi ili anipe vitu, kwasababu kama ni hivyo Yesu alishamaliza kila kitu. ila pamoja na uwepo wa Neema ndani ya Kristo Yesu, bado Mungu amepreserve principles ambazo anataka tufuate, fungu la kumi ni moja wapo, nimekuwekeeni vifungu, bishana na vifungu. tunatoa kutimiza Neno, kwasababu usipotoa anasema unamwibia, ni agizo sio hiari. na ukitimiza Neno, Mungu anasema tumkumbushe, tujadiliane ili atupatie haki zetu. wenye ufahamu wanaelewa, wasio na ufahamu wataendelea kuishi kwa kumwibia Mungu na kuishi katika laana ya Malaki.
 
aliyesalia kwa bikira maria hajaona muujiza wowote, hakuna muujiza maria anaweza kutoa, ameshakufa, na ameoza. Yesu Kristo pekee ndiye alifufuka na ndiye yu hai hadi leo. wanaoabudu maria wanaabudu sanamu, wanaabudu wafu na ni dhambi.
Unambishia aliyedai kaona muujiza kwa Bikira Maria. Vipi kwa nini nawe nisikubishie kwamba hizo hela unazodai sio muujiza. Na Waislamu, Buddha, Hindu, SDA hawana miujiza?
 
r
Unambishia aliyedai kaona muujiza kwa Bikira Maria. Vipi kwa nini nawe nisikubishie kwamba hizo hela unazodai sio muujiza. Na Waislamu, Buddha, Hindu, SDA hawana miujiza?
ruksa kunibishia hata mimi, sio lazima ukubaliane. lakini leo hii mimi na wewe tufinge, wewe kaombe kwa maria, mimi naenda kuomba kwa Yesu Kristo, tuone nani atajibiwa maombi yake. Yesu mwenyewe kuna siku aliambiwa ndugu zako (which included his mother, maria) wanakutafuta, akasema ndugu zangu ni hawa wanaosikia Neno langu. hakuna njia nyingine ya kumwona Mungu katika maisha yetu ila kwa kupitia Yesu Kristo, hata katika Maombi Yesu hajawahi hata siku moja kukosea kusema kuwa tuombe kwa kupitia maria, alisisitiza tuombe kwa Jina lake yeye Yesu. alisema mimi na baba tu umoja.

Yesu Kristo ndiye Mungu mwenyewe katika utatu mtakatifu. Maria ni mwanadamu. mwanadamu ambaye amekufa na hajafufuka hawezi kuwa suluhisho kwa mwanadamu mwingine. tuonyeshe wapi Yesu alisema tumfuate maria au tuombe kwa maria. angalia ni wapi mitume wale 12 hata kina paulo waliposisitiza kwamba tuombe kupitia maria, kwanza hata hawakujua amepotelea wapi. wapi ulishamwona maria kuanzia pale siku ya pentecost walipompokea Roho Mtakatifu? wapi maria alishawahi kutajwa? she was/is not a priority, haokoi,haponyi.

kitu pekee Yesu alimwambia yule mwanafunzi (na sio wanafunzi wote), ni kwamba, mama mwangalie mwanao, na mwana mwangalie mama yako. alijua anaenda kufa na ataenda mbinguni, hivyo alikuwa anamwacha mamake kwenye uangalizi (kibinadamu) wa Yohana. Yohana aliandika pia vitabu vile vya waraka wa Yohana (huyu ndiye yule mwanafunzi Yesu alimpenda sana na alimwacha amtunze maria kwa kusema amwangalie mamake), katika nyaraka zake zote hakuwahi kumwongelea wala kumwabudu au hata kumheshimu maria. ninyi catholics hii kitu mmetoa wapi?
 
Mada sasa imetoka fungu la kumi na kuelekea kuidhalilisha Catholic.
 
Unambishia aliyedai kaona muujiza kwa Bikira Maria. Vipi kwa nini nawe nisikubishie kwamba hizo hela unazodai sio muujiza. Na Waislamu, Buddha, Hindu, SDA hawana miujiza?
Kaekeza hapo juu kwamba hizo pesa katumiwa na mstaafu mmoja toka huko Ulaya. Hamfahamu na wala hakuwahi kuwasiliana naye. Huo ndo muujiza anaouzungumzia.
 
Kaekeza hapo juu kwamba hizo pesa katumiwa na mstaafu mmoja toka huko Ulaya. Hamfahamu na wala hakuwahi kuwasiliana naye. Huo ndo muujiza anaouzungumzia.
Sasa anapata wapi ujasiri wa kudai ya kwake ni muujiza ila ya wengine sio miujiza kisa ni wakatoliki. Huu ni ujinga huo, yani anaamini yeye ndio mmiliki wa Mungu kwa kidini chake hicho cha wapiga yowe. Dini zote hakuna yenye assurance 100% ni ya Mungu, muujiza hata mganga wa jadi anao
 
I second you .

Mwaka jana mwezi kama huu nilipata sapraizi kubwa sana toka kwa MUNGU muumba

Niligonga hela 3 times ya my monthly salary within few days

Hela yenye wala sikuitolea jasho halafu ilikuja na viburudisho juu yake.

Nadhani ilitoka na kuwasaidia watu fulani fulani ambao hata siwakumbuki maana ni ka desturi kama kusaidia watu hasa watu baki.

Nadhani fungu la 10 ni ibada uwe unaenda kanisani au huwendi fungu la 10 ni ibada.
 
Mada sasa imetoka fungu la kumi na kuelekea kuidhalilisha Catholic.
ndio ukweli, wenye kusikia kuhusu ten percent wameshasikia, ila kuna jamaa ameingiza hoja yake ya catholic humu, wakati ukweli ni kwamba catholism leads people to hell. huu ndio ukweli na sina budi kuwaambia.
 
I second you .

Mwaka jana mwezi kama huu nilipata sapraizi kubwa sana toka kwa MUNGU muumba

Niligonga hela 3 times ya my monthly salary within few days

Hela yenye wala sikuitolea jasho halafu ilikuja na viburudisho juu yake.

Nadhani ilitoka na kuwasaidia watu fulani fulani ambao hata siwakumbuki maana ni ka desturi kama kusaidia watu hasa watu baki.

Nadhani fungu la 10 ni ibada uwe unaenda kanisani au huwendi fungu la 10 ni ibada.
Mungu anataka tuishi hivyo hivyo. kitabu cha Luka 6:38 Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.

kuna principle nimejifunza maishani, ukitaka uguse moyo wa Mungu fanya yafuatayo:-

1. Okoka, wanadamu wengi sasaivi wanaelewa, ukisema uokoke anajua unamaanisha nini na ukasali wapi. jitakase pia everyday.
2. toa fungu la kumi la kila unachobarikiwa na Mungu. usitoe zao la uovu na usitoe kama unamhonga Mungu, toa kwa moyo wa kupenda.
3. toa malimbuko. malimbuko ni first fruit ya kila unachokipata, kabla haujala unampa Mungu kwanza aonje. you only give once.
4. Wape watu vitu/charities. Luka 6;38, na usijionyeshe wala kuhitaji wakushukuru, wambie shukurani wampe Mungu sio wewe.
5. invest in the Kingdom of God (wezesha kazi ya ufalme wa Mungu, seminars, mikutano,ujenzi etc).

Kumbuka, Neno la Mungu linasema, Mtu akinitumikia, Baba atamheshimu. ukimtumikia Mungu, ameahidi kukuheshimu, Mungu si mwanadamu hata aseme uongo. trust me, ukifanya hayo hapo juu, Utakuwa mboni ya Jicho la Mungu kwasababu atakuheshimisha na kukupigania, atawatawanya maadui zako hata kabla hawajafika kwako, na utakula mezani pa Mungu. huu ni ushauri wa bure.

God is the lifter of men. kuna wakati wanadamu wanaweza wakawa wanakuona kama haustahili kufika mahali, wakakutelekeza, wakakudharau na kukucheka, lakini Mungu akiamua kukuheshimisha, huwainua wanyonge toka mavumbini, na wahitaji toka jaani awaketishe pamoja na wakuu wakakiridhi kiti chake cha enzi. Mungu anao uwezo kuinua, mtumianinini yeye tu kwaajili ya kuinulia kwasababu baraka zake hazina majuto. bora nipate baraka toka kwa Mungu ambazo zitanipa furaha na uzima wa milele kuliko maelfu ya maelfu ya baraka za kishetani ambazo hazidumu na zina majuto matupu.

wale wanaotegemea magari, farasi (askari na mavifaru etc kwa siku hizi au chochote), na pia watu wanaokataa wokovu jueni ya kwamba, amelaaniwa yeye amtegemeaye mwanadamu amfanyaye kuwa kinga yake na moyoni mwake amemwacha Bwana. wapende wasipende, Mungu akiamua kukuinua au kukukumbuka, hakuna wa kuzuia, Makusudi yake hayawezi kuzuilika. wakuchukie, wafanye figisu au wasipende, Mungu akiamua ameamua.

imeandikwa Mungu humrehemu yeyote anayeamua kumrehemu, na humkazia yeyote amanyeamua kiumfanyia hivyo na mwanadamu hana mdomo wa kumjibu na kumuuliza maswali kwasababu yeye ni Mungu na hivyo ndivyo alivyoamua, kwani chombo kilichofinyangwa chaweza kumuhoji yeye aliye mfinyanzi kwamba kwanini umenifinyanga hivi au kwanini yule unamfinyanga vile? No. sifa na utukufu apewe yeye aliye juu, shahidi wa milele, alfa na omega, wa kwanza na wamwisho, yeye aishiye milele na milele, amina. sifa na Utukufu kwa Yesu Kristo, yeye ndiye yule MwanaKondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu, na ameshinda hakika na kulipa deni letu lote, ni sisi tu kumwamini na kumfuata.
 
Naomba niweke hapa ushuhuda huu, hata akiusoma mtu mmoja tu kwangu inatosha, unaweza kubadilisha maisha yake kwa namna moja au nyingine. ni juu ya yale Mungu amenitendea leo hii, siwezi kunyamaza.

kwa muda wa miezi kadhaa nimekuwa nikipitia kwenye kipindi fulani cha jangwani, na januari hii ikaja kuongeza makali yake. hii inatokana na kuyumba fulani kwenye biashara yangu fulani, na ilitokana na makosa niliyoyafanya ya kupeleka pesa nyingi kwenye ujenzi wa nyumba Dodoma na viwanja viwili besides ya hiyo nyumba (namshukuru Mungu kwa hilo pia). na niwe muwazi, nilishaachaga kutoa fungu la kumi (zaka) zamani tu pamoja na kwamba nilikuwa nasali.

kutokana na ujenzi na manunuzi ya viwanja, niliyumba sana kipesa na nikapitia wakati mgumu sana. Mimi nimeokoka, ninasali kanisa la kilokole lakini sio hayo ya mafuta na manabii wa kisasa.

nilipita kwenye mitandao nikakutana na mchungaji mmoja anahubiri kwamba fungu la kumi ni lazima kutoa na kwa kutoa fungu hil (Malaki 3:10-12) ni njia ya kumjaribu Mungu, Mungu ametangaza agano ambalo hawezi kutengua kwasababu yeye sio mwanadamu hata aseme uongo, kwamba kwa mtu anayetaka kumjaribu ili amwone kama hatafungua madirisha ya mbinguni, atoe fungu la kumi (hata kama kuna sadaka zingine) ili kiwemo chakula katika nyumba yake.

as soon as nilipoamua moyoni kuwa mtoaji, nikapita sehemu tena mchungaji mwingine akawa anafundisha kwamba fungu la kumi lilikuwa kwa ajili ya agano la kale tu, wakati wa agano jipya hatulazimiki kutoa, lakini nilishasoma pia Mathayo 23:23 na Luka 11:42, Yesu aliwaambia mafarisayo kuwa besides wanayotakiwa kuyafanya, hawatakiwi kuneglect fungu la kumi. hivyo nilikuwa kwenye njiapanda, na nilivyo mdadisi, mchungaji mmoja anasema fungu la kumi ni agizo la Mungu, mwingine anasema sio lazima kwa sasa. ila nikaazimia moyoni lazima nipate ukweli kwa kufanya practical. Mungu alinijalia fedha fulani kufikia kam 4m ambayo iliisha hata sikujua iliishaje ni kama ilipitia kwenye mfuko uliotoboka, lakini ikatakiwa nitoe fungu la kumi lake sasa mwishoni mwa mwezi wa kwanza huu kwasababu nilidhamiria kujaribu kurudi kule awali ambako nilikuwa natoaga fungu. actually, zamani nilipokua natoa fungu la kumi nilikuwa sijawahi kuishiwa pesa sasa nafikiri sikuwa najua kama ndio zilikuwa baraka za Mungu nikaachana nalo na ukiacha kuja kuanza tena ni mbinde kwasababu shetani hataki uanze kwasababu anajua ukianza kutoa tu utabarikiwa.

kupunguza maneno mengi, nilichodhamiria kufanya ni kuanza kutoa fungu la kumi sambamba na Neno la Mungu linavyosema ili nimjaribu Mungu kama alivyosema tumjaribu, sio kwasababu Mungu ananidai, bali kwasababu Mungu amesema tufanye hivyo kama namna ya kumjaribu ili tuone kama hatafungua madirisha ya mbinguni na kutumwagia baraka hata isiwepo nafasi ya kutosha. nikatoa fungu la kumi kwenye 4m hiyo, tena nilikuwa nahitaji sana hiyo potion na tayari nilishaitumia hivyo nikahisi mwisho wa mwezi nipate pesa nitoe, nikapata ile inayotosha fungu la kumi tu, ikabidi nitoe kwa imani ili mimi nibaki na Mungu tukiangaliana usoni.....

baada ya kutoa fungu linalouma na ambalo wakati huo nilikuwa nalihitaji mno, nikaanza kuangalia Mungu atafanyaje, I was like testing to see whether Mungu bado anahitaji sisi katika agano jipya tutoe au la, manake kama Mungu angereact in accordance with his word ni uthibitisho kwamba anataka tutoe, kama singereact nisingefuata. hivyo nilimjaribu Mungu kama yeye alivyosema tumjaribu.

wandugu, baada tu ya kufanya hivyo, ndio kipindi kigumu kilizidi, nilipita kwenye jangwa moja hatari ambalo nilishawahi pitaga miaka 12 iliyopita, na nilikuwa sioni njia kabisa, akili yangu yote ilishindwa kupata suluhisho, elimu, marafiki, career, ndugu n.k vilishindwa. nikaingia kwenye maombi na kuanza kumuuliza Mungu mbona sasa huonekani kama ulivyoahidi kwenye Neno lako wakati mimi nimekujaribu? au hukuwa unamaanisha nilivyofanya? nilivyomaliza tu maombi, nikakutana na clip moja ya mchungaji anatoa ushuhuda kwamba, UKIWA UMEOMBA UKAONA MUNGU KAMA HATOKEI, Jua kuna mambo mawili. aidha, haupo kwenye njia sahihi hivyo Mungu hajasikia, au kama wewe unaona upo kwenye njia sahihi, jua Mungu ameshajibu, hivyo relax subiri kuona matokeo. gafla moyoni nikashuhudiwa kuwa Mungu ameshajibu na atakushangaza muda si mrefu, kuna sauti ya Roho Mtakatifu yenye uhakikisho huwa inaongea, wale waliookoka wanajua ninachosema. nikaamua kurelax.

SASA LEO majira tarehe 04/02/2022 majira ya saa kumi na moja jioni, Mungu ameamua kunishangaza, amefungua mlango wa pesa mahali ambapo sikutegemea kabisa kwamba pangetoa pesa, sikustahili kuzipata, amenipa tu na wala sikuzitolea jasho, kama huwa unasikia kuwa Mungu alishawahi kutoa maji kwenye mwamba wana wa Israel wakanywa jangwani, ndio imekuwa kwangu, sikutegemea kupata ile pesa, sikustahili kuipata, na sikuitolea jasho, imekuja tu, na kwasababu imekuja siwezi kunyamaza kama haijaja, Mungu ameamua iwe hivyo, naona shetani alikuwa amepafunga tu nilango na madirisha ya mbinguni ya baraka zangu kwa hila zake, Mungu kafumua lango hilo na nimepata millions of money ndugu zangu. sisemi uongo. Mungu amenifanyia sapraizi jamani.

sasa, nina uhakika wa kurevive biashara yangu yote kwasababu hela niliyopewa na Mungu (ambayo hata sikustahili ni neema yake tu na nilikuwa sitegemei kwasabbu sikuifanyia kazi), millions, inatosha kufufua biashara yangu, inatosha kujenga nyumba zingine kwenye viwanja viwili besides ile niliyokuwa najenga, inatosha kuongeza mtaji mkubwa tu kwenye biashara ya mke wangu.

na zaidi ya yote, hata kwa hiyo nayo, nitamtolea Mungu fungu la kumi. Mungu anisaidie nisiache kwasababu hapo ndio nimethibitishiwa na Mungu kwamba ndiko eneo la kumjaribu Mungu. Malaki 3:10-12) anasema leteni zaka kamili ghalani mwangu ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo muone kama sitafungua madirisha ya mbinguni na kuwamwagieni baraka hata isiwepo nafasi ya kutosha, namni nitamkemea yeye alaye na kuharibu mazao yenu..., hivyo kumbe Mungu amemkemea shetani aliyekuwa amefunga milango ya baraka, sasaivi ninaye mkemeaji kwenye biashara yangu, kwenye career yangu etc. Jina la Bwana litukuzwe.

ushauri wangu kwako msomaji, uanze kutoa fungu la kumi, ila toa kwenye udongo mzuri, kwa maana kwamba utoe sehemu ambayo watu wanamwabudu Mungu katika roho na kweli, kwa upande wangu mimi huko huwa naamini ni sehemu ambayo watu wameokoka wanaenda mbinguni (nikiwa muwazi tu) sio sehemu watu wanaabudu dini na Mungu hayupo, utapoteza pesa yako kwasababu haitaenda kwenye kazi/ghala la Mungu. kwa aliyeelewa, usiache fungu la kumbi, usiache fungu la kumi, usiache fungu la kumi ! utakuja kunishukuru.

Sifa na utukufu kwa Mungu. ushuhuda huu ni wa kweli kabisa na umenitokea leo hii, kwa atakayeamini aamini, kwa atakaye neglect aneglect ila mimi nimeshautoa.
Mkuu, umesema tusitoe fungu la kumi mahali ambapo watu wanaabudu dini Mungu hayupo. Je, unaweza kutuambia mahali sahihi, kwa maana ya dini au dhehebu, pa kutolea fungu la kumi? Maana umesema tusipopeleka mahali sahihi, fungu hilo halimfikii Mungu. Tumbie/tutajie mahali sahihi.

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
 
mahali sahihi ambapo watu wanamwabudu Mungu ni pale utakapoona watu wanaabudu kwa namna hii au misingi yao iko hivi:-

1. wanaamini kuokoka kwa kumkiri Yesu Kristro kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha kwa kumaanisha kuacha dhambi.

2. wanaamini ujazo na uongoziwa Roho Mtakatifu. waabuduo halisi imewapasa kuabudu katika Roho na Kweli, manaake Roho Mtakatifu lazima ahusike katika ibada zako zote, ukiimba imba kwa Roho, ukiomba omba kwa Roho, ukihubiri hubiri kwa Roho, Yesu alisema peke yetu hatuwezi lolote, atatuletea msaidizi. ukiona unaenda sehemu watu hawaamini ujazo wa Roho Mtakatifu, hapo hakuna Mungu kwasababu Roho Mtakatifu ndiye Mungu mwenyewe.

3. Hawaabudu sanamu wala mwanadamu au wafu (eg. kuabudu na kuomba kwa wafu kama vile maria na wanaosemekana watatatifu wengine, kuabudu na kupigia magoti yale masanamu yaliyochongwa etc). Trust me, ukipeleka fungu la kumi mahali ambapo hakuna Mungu, umepoteza hela, manake hujapeleka ghalani kwa Mungu, unaweza kuwa umepeleka ghalani kwa wanadamu tu. watu wote wanaoabudu dini, hapo sio mahali utamwona Mungu kwa lolote.

4. watu hawaabudu siku. Bwana Yesu mwenyewe ni Bwana wa Sabato, wale wanaoabudu siku hadi leo hawajaokoka na wanafuata sheria. kwa kufuata sheria hakuna mwanadamu atafanikiwa kumpendeza Mungu.

5. na mengine mengi yanayofanana na hayo.
 
Sasa naanza kupata wasiwasi na uelewa wako, unasema tusiabudu wafu kama Maria, kwani Maria alikufa? Watu kama Petro, ukienda Roma utaonyeshwa kaburi lake, je, unaweza kutuambia (nchi) alikozikwa Maria?

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
 
Sasa naanza kupata wasiwasi na uelewa wako, unasema tusiabudu wafu kama Maria, kwani Maria alikufa? Watu kama Petro, ukienda Roma utaonyeshwa kaburi lake, je, unaweza kutuambia (nchi) alikozikwa Maria?

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
maria alikufa, petro alikufa, paulo alikufa. kipindi petro na paulo na mitume wote wapo hawajawahi kumwabudu au kuomba kwa kupitia maria au wafu. Biblia inasema tuombe kwa Jina la Yesu tu, Mungu anatutambua kwa kupitia Jina la Yesu tu, si jina la wanadamu. ni Yesu tu ndiye alitolewa kafara ili kwa yeye kama ngao tukienda mbele za Mungu asituone sisi moja kwa moja amwone Yesu kwanza ndio atupokee. maria hajawahi kuwa kafara, mwanadamu yeyote hajawahi kuwa kafara, ni Yesu Kristo tu ndiye alizaliwa katika mwili (pamoja na kwamba yeye ni Mungu mwenyewe) ndiye alifanyika mwili ili awe kafara.

ukiabudu mwanadamu au kuomba kwa kupitia mwanadamu nje ya Yesu, haupati kitu na unapoteza muda tu. kama hauamini, Mungu ametupatia mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za shetani, ametuelekeza tuponye magonja na kufanya mengi ambayo Yesu alifanya na hata zaidi ya hayo. amka sasa kesho nenda mtaani kakemee hata pepo tu (pamoja na kwamba najua huko kwenu mnayaogopa though mnaishi nayo) sema "kwa jina la bikira maria toka"uone kama litatoka au litakukodolea macho.

ni kwa Jina la Yesu tu kila goti litapigwa na vitu vilivyoko juu mbinguni, duniani na chini ya nchi, na kila ulimi utamkiri Yesu Kristo kuwa yeye ndiye Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.
 
Unasisitiza Bikira Maria alikufa, nimekuuliza alizikwa nchi gani, hutaki kusema. Sijasema kuwa tunamwacha Yesu Kristo na kumwabudu Maria. Kila mtu anaujuwa ukuu wa Yesu Kristo na ni kwamba yeye ndio daraja linalotuunganisha na Mungu (Baba). Bikira Maria tunamuheshimu kwa kumleta duniani huyu anayetuunganisha na Mungu!

Hata katika akili ya kawaida tu, anapotokea mtu anafanya mambo makubwa na ya kipekee, ya kusaidia jamii, nchi, au dunia kwa ujumla, watu hawaishii kumwangalia yeye tu, bali hata aliyemleta duniani (mzazi wake). Wengine hufikia hata kumzawadia. Tukirudi kwa Bikira Maria, huyu ana ukuu wa kumzaa mwana wa Mungu, je, asiheshimiwe? Huyu alikuwa na vigezo (utakatifu) vilivyokubaliwa na Mungu hata kuruhusu mwanawe (Yesu Kristo) aje duniani kupitia kwake! Unafikiri ni jambo dogo hili?

Sasa kwa taarifa yako (na wengine wenye uelewa kama wako), Bikira Maria hakufa, alipalizwa mbinguni mzima mzima. Mungu aliona mtu aliyemleta mwanae duniani asionje adhabu ya kifo na hatimaye kuzikwa. Sasa usiniulize mbona Yesu alikufa? Sisi wengine (binadamu wengine), tunakufa, tunazikwa, na hatimaye kuozea kaburini, Bikira Maria hakuwa wa kuozea kaburini, kwa kuwa ni mama wa Mungu (najuwa hili la mama wa Mungu litaleta mjadala). Hivyo basi, Bikira Maria lazima aheshimiwe. Kama Mungu mwenyewe anamuheshimu (naomba tuelewe hapa), je sisi ni nani tusimuheshimu Bikira Maria?

comon brother, look at you ! Yesu Kristo hakuletwa hapa duniani na Maria. Yesu Kristo alikuwepo hata kabla ya maria. mitume gani walimheshimu maria? sisemi walitakiwa kumdharau au la, isipokuwa hawakumwona kama mtu tofauti na watu wengine kama mnavyofanya ninyi. Yesu Kristo alikuwa anahubiri siku moja, wakaja watu wakasema ndugu zako na mama yako wanakutafuta wanataka wakuone, yueye aliona wanamsumbua aache mkutano anaohubiri aende kufanya nini? akawaambie ndugu zangu na mama zangu ni hawa wanaonisikiliza hapa kwenye mkutano. hakumaanisha kwamba kweli huo mkutano ni mama yake, alimaanisha kuwa yeye alikuja hapa duniani kabla hata ya hao wanaojifanya kumtafuta/kumwita, na kwamba hapa duniani alikuja kwa kazi ile ya kuhubiri ijili. mmepotea sana kuanzia papa hadi mtu wa kwenye kigango. okokeni, mnapoteza muda kuabudu dini na wanadamu. Yesu anawaita leo, jaribuni tu muone kama tunachowaambia kila siku kama ni cha kweli au cha uongo, mkiona wokovu tunaowahubiria hauna maana basi rudini huko huko, ila nakuhakikishia ukiokoka leo Roho Mtakatifu atafungua macho yako ya kiroho na utajilaumu sana kwanini umepoteza muda na mali kutumikia dini kwa miaka mingi hivyo.

Mungu ni Roho, nao wamwabuduo imewapasa kuwambudu katika Roho na Kweli, Roho Mtakatifu ndiye kiongozi wetu, na hajawahi kutuelekeza kufanya chochote juu ya mfu Maria. ukiwa na Roho Mtakatifu hautaabudu dini, utaongozwa kumwabudu Mungu kiusahihi. Mungu akusaidie.
 
Back
Top Bottom