Sina maana ya kuwa mmbea ama kumkandia dada yangu ila hii ndio hali halisi ya matatizo haya ya sasa yanayofanya ndoa nyingi kubomoka, mimi nimeleta case study.
Mifano ipo mingi sana juu ya wanawake wasomi wa vyuoni kuwa wasumbufu kwenye ndoa ila wacha niweke kisa cha mtu naemjua kabisa wala si wa kihadithiwa.
Ni dada yangu huyu kabisa, aliitafuta sana ndoa na akaipata kimbebe kikawa kwenye maisha halisi ya ndoa.
Dada alikuwa kakariri sana maisha ya miss independent, haki sawa, ndoa za kitamthilia, n.k kwa bahati mbaya ama nzuri mme wake alikuwa hawezi vumilia haya mambo, kapata kazi hapa mjini na ni msomi ila kakulia sana maisha ya kijijini.
Dada alianza kuchoka kumfulia mme wake nguo akashauri watafte house girl, mme wake akamwambia hata wakimleta house girl bado nguo zake haziwezi fuliwa na house girl inabidi afue dada maana ni majukumu yake.
Dada alianza kuchoka kuamka asubuhi kumpashia mme wake maji, anamwambia mme wake apashe, walikuwa wanakorofishana sana.
Dada alitaka kuendelea tabia zake za kukutana na kutoka out na anaowaita marafiki zake wa kiume, mme wake alikataa hii hasa pale alipokuwa anaona ni kama vile bado hajui nini maana ya ndoa.
Vitimbwi vilikuwa ni vingi sana ila kwa moyo wa kipekee wa yule bwana, dada hakuwahi kupigwa hata kibao, ingekuwa hata mimi angekuwa ashachezea sana tu.
Baada ya miezi minne ya ndoa nikaanza kuona dada anapost status za kimafumbo kuashiria anateswa, nikimpigia anadai anatishiwa maisha lakini kwa akili yake navyomjua ni rahisi kumjua anaposema uwongo, nikawa kimya tu.
Alirudi nyumbani na mpaka sasa yupo nyumbani, mzazi hawakuwa na tatizo lolote kwa yeye kuridi na hata anavyoondoka chumba chake kilifungwa asilale mti mwengine.
vikao kama viwili hivi haonyeshi nia ya kurudi, nyumbani karudi na mtoto kuna house girl, anapikiwa, n.k.
Bwana yule anatoa laki 3 ya kumtunza mtoto kila mwezi lakini dada hakuwahi kusema hili alikuwa anasema hapewi chochote, na hii nikaja kugundua ni mbinu ya kumfanya aliekuwa mme wake tumuone ni mkatili nae apate points za kujitetea.
Majukumu ya ndoa kwa mabinti wengi wa vyuoni ni tatizo, wanataka kuendelea na lifestyle za vyuoni ambazo haziwezi kuendana na maisha ya ndoa, wanataka haki sawa bila kutekeleza majukumu yao, wamekuwa brain washed na tamthilia, n.k.