mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,778
- 7,145
Wana JF.
Katika pita pita zangu nimeweza kudadisi kudadisi ni kwanini kumeibuka ujenzi wa kasi namna hii iliyopo hasa maeneo ya kanda ya ziwa hususani Kagera na Geita. Ningeweza kusema Kagera tu lakini kile kipande kilichochotwa na kupeleka Geita kimebadili stori.
Kwanini mchwa ndio chanzo? Sababu ni kwamba watu wa zamani walidhani kujenga nyumba ya udongo ni bei nafuu mno kwani vitu vingi unavipata bure. Haya yalikuja kubadilika baada ya ukataji miti hovyo imara na ya asili, hivyo vijiji vingi vilijikuta hakuna miti ya kujengea tena, hakuna misitu ya kukata miti kama tulivyozoea.
Miti inayochukua muda mfupi nayo haiwezi kuimili vishindo, wadudu watafunao miti, mchwa. Kilichofuata nyumba nyingi zilizojengwa kwa miti dhaifu zote zilidondoka, ndipo wakatokea wabunifu wa kupasua mawe na wengine kuanza kufyatua tofari kwenye mashamba yao.
Katika harakati za kukimbia mdudu mchwa kukatokea dharura ya kutakiwa wataalum zaidi wa kufyatua tofari za udongo na kuchoma. Haijaishia hapo, hadi kuna wataalum wa kupima udongo kama unafaa kufyatua tofari. Ajira nyingi zikatokea sababu ya mdudu mchwa.
Haikuishia hapo wakatokea wataalum wa kubuni ramani za ndani na wengine wakaongeza ujuzi zaidi wa kuremba paa, tena kwa ujenzi wa gharama nafuu wa mbao za mtindo mmoja wa 2 kwa 2. Vijana hawa wapya wamekuwa tishio kwa mafundi wa zamani, tena wenye kisomo cha juu.
Kwa sasa watu wanaojenga mjini wanawafuata vijana wa vijijini kuja kuezeka nyumba Dar na Arusha kutoka Bukoba na Geita. Vijana hawa wameleta mvuto kwa jamii, kwani ni wepesi kumaliza kazi, ni watu waaminifu na hesabu zao za nyenzo wako vizuri, kwani hawazidishi vitu ili kupata cha juu.
Kama watu hamwamini. Tembelea Kagera, Geita, Kahama ujionee kasi ya ujenzi wa nyumba bora zenye ufanisi wa paa imara zisizoezuliwa na upepo.