Ushuhuda wa uwepo wa mali za Kijerumani

Ushuhuda wa uwepo wa mali za Kijerumani

Mtoto wa Golden Paste

Senior Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
166
Reaction score
120
Habari wana Jf

Kwa muda mrefu sasa nilikuwa nikifuatilia ndani na nje ya JF kuhusu mali alizoacha mjeruman kipindi anaondoka nchini miaka mingi iliyopita. Kila mtu alitoa mtazamo wake juu ya mali kale zilizoachwa katika sehemu mbalimbali ndani ya nchi yetu.

Wapo waliosema kuwa mzungu hawezi kuacha mali lazima aliondoka nayo,wengine wakasema kuwa hiyo ni ndoto hakuna kitu kama hicho,wengine wakaenda mbali zaidi wakihusisha mali zilizoachwa na ushirikina na wengine wakasema hiyo ni ndoto na hakuna kitu kama hicho kuhusu mali zilizoachwa na wajerumani.

Kwa miaka mitatu ambayo nilitaka kujua undani wa jambo hili ikiwemo na kutembelea sehemu mbalimbali ikiwemo mkoa wa TABORA na SINGIDA hatimae nimeweza kubaini ni kweli wajerumani waliacha mali zao nchini mwetu na uwezekano wa kuzipata upo.

Siku ya tarehe 9 julai 2020, nilitembelea site moja iliyopo mkoa wa Singida wilaya ya Ikungi na kufanikiwa kuonana na vijana ambao wamefanikiwa kupata hazina hizo za mjerumani kama moja ya mapambano ya kutafuta ridhki.

Kiukwel sikuwahi kuamini kama kuna ukweli wowote juu ya uwepo wa mali hizi za kijerumani ila nimeweza kujionea mwenyewe kwa macho yangu baadhi ya vitu walivyofanikiwa kuvipata katika moja ya site iliyokuwa vimehifadhiwa vitu hivyo.

NB;Lengo la post hii ni kutoa ushuhuda tu kuwa mali za kijerumani zipo na si uongo wala mambo ya kishirikina, sijaweka post hii kwa lengo lolote lile tofauti na kutoa ushuhuda pekee.
Screenshot_20200713-152159_1594664051028.jpeg
 
Sijaona rupia hapo zaidi nimeona makorokoro tu.
Hizo nguvu,nia na pesa mnazozitumia kutafuta rupia ya kale ya mjerumani mngezielekeza kwenye maisha ya kila siku si mngekuwa maili mia mbele kimaisha.
 
Ungetuambia sasa hizo mali ni mali za namna gani na thamani yake ni ipi? Hapo naona mawe, udongo, vitu mfano wa vyuma etc, ndio mali zenyewe???
Sio chuma mkuu,hizo ndizo mali kale ambazo zilikuwa zimehifadhiwa ardhini kwa muda mrefu na vyote vimetengenezwa kwa madini ya Uranium na Diamond.
Kuhusu thamani yake bado hawajajua maana wanatafuta soko.
 
Duu! Umenikumbusha pigo la yoashi na issue ya ku track simu story zilianza hivihiv!
Dah una akili san.
Si kila anaeleta uzi anania ya kumtapeli mtu,siko hivo nimeleta uzi kama ushuhuda pekee si katika jambo jingine zaidi ya hapo. Wazeni vile akili zenu zinawapeleka
 
Wajinga huwa hawakosekani, watapigwa hapo hadi wakome, PM itakua imeanza kujaa.
Ukiona uzi uko jukwaani basi ujue si kila anaeleta uzi amekuja kufanya akili yako inachokutuma,najielewa na naheshimu sana wadhifa nilionao katika serikali hii.
 
Back
Top Bottom