Ushuhuda wa uwepo wa mali za Kijerumani

Ushuhuda wa uwepo wa mali za Kijerumani

Mkuu wataalamu niliowakuta pale ndiyo waliothibitisha kuwa vito hivyo vimetengenezwa kwa madini ya diamond na Uranium na si mimi,kwa hivyo mantiki niliyopata pale ndiyo iliyotumika kufikisha ujumbe hapa
Uranium haiwezi kuwa exposed hivyo maana ni hatari kwa binadamu, wanyama na mimea na ardhi iliyokuwa exposedkwauranium haiwezi tumika kwa muda. Huu ni utapeli tu
 
Ujinga ni kipawa mwenyez mungu alivyo wajalia. Amen
 
Half-life yake ni 4.5 billion years.

Yaani kama leo hii unayo kilo moja ya Uranium baada ya miaka 4.5 billions hiyo kilo moja itakuwa imepungua kufikia nusu kilo.
Ila wanasayansi hesabu zao zingine zinanichekesha sana.
sasa miaka 4.5 billions si itakuwa hata kiyama kishapita,maana tangu afe yesu ndio kwanza miaka 2020 yaani hata miaka 3000 bado halafu hao wanaongelea miaka bilioni.
 
sinamaana ya diamond baba lao bali diamond madini a.k.a almas eti uipate halafu uiache imelala ardhini unahangaika tafuta soko. Jamaaatapigwa huyu
Jamaa walimfanya zezeta walimuona ni mgeni wakataka wampige pesa wamuachie makanyanga.
 
Ila wanasayansi hesabu zao zingine zinanichekesha sana.
sasa miaka 4.5 billions si itakuwa hata kiyama kishapita,maana tangu afe yesu ndio kwanza miaka 2020 yaani hata miaka 3000 bado halafu hao wanaongelea miaka bilioni.
Hapo Wanasayansi hua wanatudangaya sana. Dunia haijafikisha hata miaka elfu 5 tangu iumbwe.
 
Mkuu, naona unakazia kuhusu hao wataalamu uliowakuta pale. Ila tu nikwambie kuwa ukiwa na madini yoyote ya thamani kama metals (dhahabu, silver etc) au vito (ruby, sapphires, garnets, diamonds etc) huwezi hangaika na masoko, KAMA MALI YAKO NI SAHIHI NA HALALI. Nasema hivyo kwa sababu nimewahi kimbiza biashara ya dhahabu miaka ya 2015. Ukiona mtu ana madini, na miongoni mwa madini yenyewe ni diamonds, na huyo mtu akasema hajui akauzie wapi, then something is wrong somewhere. Smells FISHY
Siwezi kazia sana maana mimi nilishuhudia tu,kuhusu kuuza ni dhamana yao
 
Half-life yake ni 4.5 billion years.

Yaani kama leo hii unayo kilo moja ya Uranium baada ya miaka 4.5 billions hiyo kilo moja itakuwa imepungua kufikia nusu kilo.
Ok asante.!
Mambo ya physics hayo.!
 
Habari wana Jf
Kwa muda mrefu sasa nilikuwa nikifuatilia ndani na nje ya JF kuhusu mali alizoacha mjeruman kipindi anaondoka nchini miaka mingi iliyopita. Kila mtu alitoa mtazamo wake juu ya mali kale zilizoachwa katika sehemu mbalimbali ndani ya nchi yetu. Wapo waliosema kuwa mzungu hawezi kuacha mali lazima aliondoka nayo,wengine wakasema kuwa hiyo ni ndoto hakuna kitu kama hicho,wengine wakaenda mbali zaidi wakihusisha mali zilizoachwa na ushirikina na wengine wakasema hiyo ni ndoto na hakuna kitu kama hicho kuhusu mali zilizoachwa na wajerumani.

Kwa miaka mitatu ambayo nilitaka kujua undani wa jambo hili ikiwemo na kutembelea sehemu mbalimbali ikiwemo mkoa wa TABORA na SINGIDA hatimae nimeweza kubaini ni kweli wajerumani waliacha mali zao nchini mwetu na uwezekano wa kuzipata upo.

Siku ya tarehe 9 julai 2020,nilitembelea site moja iliyopo mkoa wa Singida wilaya ya Ikungi na kufanikiwa kuonana na vijana ambao wamefanikiwa kupata hazina hizo za mjerumani kama moja ya mapambano ya kutafuta ridhki.
Kiukwel sikuwahi kuamini kama kuna ukweli wowote juu ya uwepo wa mali hizi za kijerumani ila nimeweza kujionea mwenyewe kwa macho yangu baadhi ya vitu walivyofanikiwa kuvipata katika moja ya site iliyokuwa vimehifadhiwa vitu hivyo.

NB;Lengo la post hii ni kutoa ushuhuda tu kuwa mali za kijerumani zipo na si uongo wala mambo ya kishirikina,sijaweka post hii kwa lengo lolote lile tofauti na kutoa ushuhuda pekee.View attachment 1505966
Mkuu!
Sijui hata lengo lako ni Lipi la kuanzisha Uzi huu!
Ukweli ni kuwa hivyo Vitu vipo na Ndo maana pale Wizara ya Maliasili kuna kitengo cha Mali Kale, inaonyesha Serikali inatambua uwepo wa hivyo Vitu, na Serikali hutoa Vibari.......

Jf hutopata chochote Positive zaidi ya Hasira za Watu waliopata kutapeliwa, Ndugu ya waliopata kutapeliwa..... Na watu ambao huwa wanasikia hizi story kama ni Utaperi....

Hapo kuna Vitu hujaeleza, Yale Mauzauza, na kama ungeeleza yote, ungeishia kuitwa Majina mabaya hapa!!!

Ni nini lengo la Uzi wako?
Niko na Experience na unachokielezea ILA hapa jf hutopata chochote positive!!!
 
Back
Top Bottom