Ushuhuda wadada: Ulijisikiaje siku mpenzi wa zamani alipooa wakati wewe bado hujaolewa?

Ushuhuda wadada: Ulijisikiaje siku mpenzi wa zamani alipooa wakati wewe bado hujaolewa?

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,772
Reaction score
22,598
Wakuu,

Hapa ninavyoandika ni kuwa harusi inanguruma kanisani na ni karibu na maeneo ya shoga yangu kipenzi. Alinipigia simu nikambembeleze maana mwanaume aliyekuwa naye alimuacha kwa kuwa alimnyima 'utamu' .

Ananiambia huyo jamaa walikaa mwaka mzima bila kufanya mapenzi ila jamaa alikuwa anataka abebe mimba ndio amuoe. Dada wa watu ni mlokole akamwambia asubiri kwanza mpaka wafunge ndoa.

Jamaa akamuacha akaanza mahusiano na mtu mwingine kwa siri. Akapewa tamu mimba ikaingia. Jamaa fasta kamvisha pete na leo ndio ndoa yenyewe.

Dada alipo hapa anamwaga chozi...
 
Wakuu,

Hapa ninavyoandika ni kuwa harusi inanguruma kanisani na ni karibu na maeneo ya shoga yangu kipenzi.

Alinipigia simu nikambembeleze maana mwanaume aliyekuwa naye alimuacha kwa kuwa alimnyima 'utamu' .

Ananiambia huyo jamaa walikaa mwaka mzima bila kufanya mapenzi ila jamaa alikuwa anataka abebe mimba ndio amuoe.

Dada wa watu ni mlokole akamwambia asubiri kwanza mpaka wafunge ndoa.

Jamaa akamuacha akaanza mahusiano na mtu mwingine kwa siri. Akapewa tamu mimba ikaingia.

Jamaa fasta kamvisha pete na leo ndio ndoa yenyewe.

Dada alipo hapa anamwaga chozi...
Anamwaga chozi?kama kweli mwambie wakeyupo na msimamo ni huo huo hakuna kuonjana mpaka ndoa ndio mpango wa Mungu.
 
Inauma kwa muda tu then atapoa tu, kuna ile mtu ulimpenda + mazoea ndo yanaumiza. Inawezekana kabisa yeye angebeba mimba na hata asiolewe, akaishia kuwa single mom tu. Wapo wanawake wengi tu walikuwa wanabembelezwa wazae, now hawaamini kilichowakuta after kubeba mimba; kuzaa sio kuolewa.

Kama anachokifanya, anakifanya kwa ajili ya Mungu wake, she is doing the best thing na Mungu anayemtumania wala hatomuacha aaibike. God has something very amazing in store for her, awe tu mvumilivu, atalia machozi ya furaha na kusema Mungu ahsante nilipita tu kule. Nampa hongera, maana wengi wetu huwa tunachagua tamaa zetu, tunamuweka Mungu wa pili; na huwa tunavuna tunachopanda kwa kweli
 
Inauma kwa muda tu then atapoa tu, kuna ile mtu ulimpenda + mazoea ndo yanaumiza. Inawezekana kabisa yeye angebeba mimba na hata asiolewe, akaishia kuwa single mom tu. Kama anachokifanya, anakifanya kwa ajili ya Mungu wake, she is doing the best thing na Mungu anayemtumania wala hatomuacha aaibike. God has something very amazing in store for her, awe tu mvumilivu. Nampa hongera, maana wengi wetu huwa tunachagua tamaa zetu, tunamuweka Mungu wa pili; na huwa tunavuna tunachopanda kwa kweli

Tatizo hawa wa kujiita walokole hawana tofauti na watu wengine
Una nia naye ya dhati kabisa kumuoa analeta vikwazo mixer sijui mchungaji kasema kile mara vile kumbe kuna vijemba kanisani vinajipigia tu tena kwa zamu. Kama atakuwa hajatembea na mwanaume na nikathibitisha ntamsubiri miaka 100 ila kama wameshatoboa baaaas hakuna kitu hapo.
 
Tatizo hawa wa kujiita walokole hawana tofauti na watu wengine
Una nia naye ya dhati kabisa kumuoa analeta vikwazo mixer sijui mchungaji kasema kile mara vile kumbe kuna vijemba kanisani vinajipigia tu tena kwa zamu
Kama atakuwa hajatembea na mwanaume na nikathibitisha ntamsubiri miaka 100 ila kama wameshatoboa baaaas hakuna kitu hapo
Wewe ndo unaona tatizo, kwake yeye ndo maisha yake aliyoyachagua. Kila watu wana taratibu zao wanazozifuata ukitaka kuoa/kuolewa kwao, na ni sawa kabisa. Wewe ukiona zinakushinda, tafuta ambaye choices na formalities zake zinaendana na wewe

Kama mtu alisex ila akaona ni ubatili tu akaamua kurudi kwa Mungu wake, who are you to judge her? Tafuta mtu anayeamini kile unachokiamini, ukiona ya walokole huyawezi, kausha tu
 
Wewe ndo unaona tatizo, kwake yeye ndo maisha yake aliyoyachagua. Kila watu wana taratibu zao wanazozifuata ukitaka kuoa/kuolewa kwao na ni sawa kabisa. Wewe ukiona zinakushinda, tafuta ambaye choices na formalities zake zinaendana na wewe

Kama mtu alisex ila akaona ni ubatili tu akaamua kurudi kwa Mungu wake, who are you to judge her? Tafuta mtu anayeamini kile unachokiamini, ukiona ya walokole huyawezi, kausha tu
Sasa wataendelea kupigwa na viongozi wao wa makanisa hamna namna wakifika 35 wataanza kumtafuta yeyote atakayekuja mbele yao
 
Back
Top Bottom