Ushuhuda wadada: Ulijisikiaje siku mpenzi wa zamani alipooa wakati wewe bado hujaolewa?

Ushuhuda wadada: Ulijisikiaje siku mpenzi wa zamani alipooa wakati wewe bado hujaolewa?

dah nyie acheni tu,naweza kusema ni zaidi ya kuumia kupenda ni mtihani nyie.Mie nilikaa week kama chizi yani dah,acha tu mtu anakuja anaingia moyoni mnakuwa mnapendana na kuzoeana then mwisho wa siku ana change unaweza kujinyonga,thanks god niko salama lakini kwa kilichonikuta dah mungu ndo anajua
 
Wakuu,

Hapa ninavyoandika ni kuwa harusi inanguruma kanisani na ni karibu na maeneo ya shoga yangu kipenzi.

Alinipigia simu nikambembeleze maana mwanaume aliyekuwa naye alimuacha kwa kuwa alimnyima 'utamu' .

Ananiambia huyo jamaa walikaa mwaka mzima bila kufanya mapenzi ila jamaa alikuwa anataka abebe mimba ndio amuoe.

Dada wa watu ni mlokole akamwambia asubiri kwanza mpaka wafunge ndoa.

Jamaa akamuacha akaanza mahusiano na mtu mwingine kwa siri. Akapewa tamu mimba ikaingia.

Jamaa fasta kamvisha pete na leo ndio ndoa yenyewe.

Dada alipo hapa anamwaga chozi...
Mwambie muda sio rafiki....

Mwanamme mwingine akijitokeza mwambie atoe utamu la sivyo ndoa ataishia kuziona kwenye bango kipindi kinachorushwa TBC
 
Huyo hakuwa wake.....Mungu hakupi unachotaka anakupa unachostahili,..ningekuwa mm ndio yeye ningepiga goti madhabahuni na kutoa sadaka ya shukrani kwasababu tumeambiwa tushukuru kwa kila jambo,.

Mungu akawe mfariji wake.
Teh kwa kweli sadaka muhimu.
Wababaishaji huwa wana masharti kama waganga, waoaji akhaaa
 
Inauma kwa muda tu then atapoa tu, kuna ile mtu ulimpenda + mazoea ndo yanaumiza. Inawezekana kabisa yeye angebeba mimba na hata asiolewe, akaishia kuwa single mom tu. Wapo wanawake wengi tu walikuwa wanabembelezwa wazae, now hawaamini kilichowakuta after kubeba mimba; kuzaa sio kuolewa.

Kama anachokifanya, anakifanya kwa ajili ya Mungu wake, she is doing the best thing na Mungu anayemtumania wala hatomuacha aaibike. God has something very amazing in store for her, awe tu mvumilivu, atalia machozi ya furaha na kusema Mungu ahsante nilipita tu kule. Nampa hongera, maana wengi wetu huwa tunachagua tamaa zetu, tunamuweka Mungu wa pili; na huwa tunavuna tunachopanda kwa kweli



Mnaleta ulokole kwenye mapenzi hahaha mtaishia kupamba madhabahu
 
Tena avumilie tu siku zote mungu amuachi mja wake ni jambo la kitambo kidogo tu,sema itauma sababu ni hukutarajia ila baadhi ya me si watu wazuri.
 
Back
Top Bottom