Inauma kwa muda tu then atapoa tu, kuna ile mtu ulimpenda + mazoea ndo yanaumiza. Inawezekana kabisa yeye angebeba mimba na hata asiolewe, akaishia kuwa single mom tu. Wapo wanawake wengi tu walikuwa wanabembelezwa wazae, now hawaamini kilichowakuta after kubeba mimba; kuzaa sio kuolewa.
Kama anachokifanya, anakifanya kwa ajili ya Mungu wake, she is doing the best thing na Mungu anayemtumania wala hatomuacha aaibike. God has something very amazing in store for her, awe tu mvumilivu, atalia machozi ya furaha na kusema Mungu ahsante nilipita tu kule. Nampa hongera, maana wengi wetu huwa tunachagua tamaa zetu, tunamuweka Mungu wa pili; na huwa tunavuna tunachopanda kwa kweli